Yaani Wamarekani wamenikosha na jinsi wanavyozingatia demokrasia. Kila mmoja anazungumza kuhusu umoja wa kitaifa, anazungumzia kutibu majeraha ya kampeni na kuendelea kubaki wamoja. Yaani Amerika kwanza, vyama baadaye. Lakini mapumb... ya huku kwetu yanatanguliza vyama kwanza. Ningekuwa Magufuli mimi ningejiuzulu ili tufanye uchaguzi mpya na kuionesha dunia kwamba tunaweza. Nasimamia uchaguzi huru na wa haki bila kupiga watu mabomu. Hapo ndo ataweka historia ya kweli. Lakini sasa haya mambo ya kusifia demokrasia za wengine huku kwako kumeoza hayajengi kabisa!!