Maneno Tisa Yanayovuta Utajiri

Maneno Tisa Yanayovuta Utajiri

Abtali Mwerevu

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2013
Posts
773
Reaction score
668
Dunia ina mengi na unapaswa kuendana na mengi hayo. Katika kuutafuta utajiri zipo njia nyingi na ni vyema kujaribu zile zinazofaa.

Tumekuwa tukisikia matajiri wengi wana siri nyingi, ni kweli kuna ambao wameua ndugu zao, wapo wanaolala na nyoka, wapo wanaolala kwenye jeneza na vioja chungu nzima. Lakini katika hayo yote, wamefanikiwa. Hiyo ni njia waliyochagua. Njia ngumu. Wapo wanaokesha katika nyumba za ibada wakiusaka utajiri, tukiomba ushahidi wa waliotajirika kwa njia hii, watakuja wengi! Kwa hivyo njia zipo nyingi, usichoke kujaribu mpaka uipate inayokufaa.

Pamoja na hayo, ipo njia rahisi lakini inayokutaka uamini kwelikweli kwa moyo wako. Ni njia ya kutumia maneno tisa kuvuta utajiri.

Njia hii ya maneno tisa kuvuta utajiri inaaminiwa na kutumiwa na wengi tena inapigiwa chapuo na daktari nguli na mchunguzi wa ubongo wa mwanadamu Dr. Steven Newton ambaye anaamini njia hii ikishikamana na akili yako, utabadili maisha.

Wengi wanaitumia njia hii na wamefanikiwa kupata utajiri, afya, mahusiano na mafanikio kedekede. Kwa wasomi njia hii siyo ‘meditation’ wala siyo ‘Law of Attraction.’ Njia hii ni ulozi mwema, unanuia maneno yako tisa kisha unalala.

Wanasayansi wanaounga mkono njia hii wanaamini ipo sehemu katika ubongo inayohusika na bahati ambapo kwa wengi huwa imelala. Maneno haya tisa yataiamsha na kukufanya ubahatike kupata unachotaka ikiwemo huo utajiri.

Kuwa tajiri inachukua muda mrefu na bahati. Unao uwezo wa kuiongoza bahati katika maisha yako.

Masharti kabla hujafanya dawa hii

Kabla hujafanya njia hii, kwanza hakikisha unafanya biashara yoyote. kama umeajiriwa, jitahidi ufungue biashara yoyote ambayo unaweza ukaiendesha mwenyewe kwa muwa wa ziada, au ukaweka mtu wa kusimamia. Bahati hii itakuja katika biashara yako wewe binafsi. Ukiifanya huna biashara binafsi, bahati hii itaangukia kwa ‘boss’ wako na utamuona kila siku anazidi kutajirika. Hivyo nasisitiza unapofanya njia hii hakikisha una biashara yako. Biashara yoyote, haijalishi ni ndogo kiasi gani.

Hakikisha unaishi kwa bajeti, fahamu pesa unayoingiza na pesa unayotumia.

Tumia pesa kwa vitu unavyovihitaji tu: mfano, chakula, mavazi na makazi. Vitu kama pombe na starehe nyinginezo punguza, ukiweza acha.

Punguza madeni, wingi wa madeni utafanya njia hii ishindwe kwa sababu ya ubongo kuelemewa na msongo wa mawazo.

Baada ya kuwa na biashara

Hatua ya kwanza: fahamu dawa hii inaamsha sehemu ya ubongo ambayo kwa wengi imelala. Sehemu ambayo huhusika na bahati. Utajiri ni bahati, wakongwe watakubaliana nami, unaweza kuchimba madini miaka ishirini bila kupata kitu, akaja jamaa akachimba siku mbili akapata na kutajirika.

Hatua ya pili: nunua shuka nyeusi. Usiogope, umeamua kuingia katika mapambano ya maisha, hakuna kurudi nyuma.

Hatua ya tatu: fanya mambo yako yote, lakini jambo la mwisho kabla hujalala. Zima taa ndani kuwe giza. Kama umeoa, mfahamishe mke wako akupatie utulivu na asiwe na hofu kwa kile unachofanya. Hakikisha maneno haya tisa umeyakalili, kwani hutaweza kusoma kwa sababu ndani kutakuwa giza, na wewe utakuwa ndani ya shuka jeusi.

Tamka maneno haya tisa ukiwa ndani ya shuka jeusi kila siku kwa muda wa wiki mbili. Ukifanya kwa imani, utaanza kuyaona mabadiliko, utaanza kuyaona mafanikio, utavuta bahati, utatajirika.

“NINATAKA KUWA TAJIRI, LAZIMA NIWE, LAZIMA… MIMI NI TAJIRI.”

Baada ya kutamka maneno haya, usiseme neno lolote mpaka kesho asubuhi. Haya ndiyo yawe maneno yako ya mwisho kutamka kila siku kwa muda wa wiki mbili. Uamkapo asubuhi, chapa kazi kwa bidii na nguvu ukiamini kile ulichokisema usiku. Usikate tamaa, maneno hayo yataufungua mlango wa bahati na mafanikio, hatimaye… utajiri.

Nitafurahi ukinipa mrejesho, nitafurahi ukinifahamisha kwamba sasa umeanza kufanya jambo hilo.

Jiunge katika Group letu la WhatsApp kwa Kugusa Hapa.
 
Da watu Wana chambo za ajabu du maisha haya tutafute hela wazee tuache ngonjera hizi
 
Fanya uone, ingekuwa rahisi kila mtu angekuwa nazo
 
Bado natafuta shuka nyeusi sijapata naona uvivu kwenda kariakoo na mvua hii ya siku 2 noma sana
 
Back
Top Bottom