Maneno matano ya kutamka kwa mwenza wako

Jan 12, 2021
9
9
Wanandoa wa karne hii wamesahau maneno matano muhimu kwenye ndoa nayo yanaifanya ndoa kudumu. Yafuatayo ni maneno muhimu katika ndoa;

1. NINAKUPENDA
Tafakari jinsi ulivyokuwa unalitaja(tamka) neno hili wakati wa uchumba wako. Sasa jiulize je unalitendea haki katika ndoa yako?. Kama jibu ni hapana umeanza kuua ndoa yako polepole lakini kwa uhakika.

2. POLE
Jihoji ni mara ngapi umemwambia mme wako au mke wako pole?. Kumbuka neno pole linarejesha upendo na faraja pia. Hebu fikiria wewe mwanaume umetoka kazini umechoka halafu umemukuta mke wako nyumbani lakini hakuambia Wala pole na kazi, unajisikiaje?. Tumia neno hili liponye ndoa yako.

3. KARIBU
Wanandoa wanapaswa kukaribishana maana hii ni ishara mojawapo ya upendo. Mtu ambaye umemukuta lakini hakukaribishi huyo anajionyesha kwako kuwa ni namna gani hakupendi. Sasa basi kumkaribisha mwenzi wako ni kuonyesha pendo lako kwake.

4. NISAMEHE
Katika jamii nyingi wanawake ndio wanajitahidi kusema NISAMEHE mme wangu. Tatizo lipo kwa wanaume wanapowakosea wake zao hawataki kusema nisamehe mke wangu kwani wanaona Kama ni kudharauriwa na mke. Laah si hivyo Bali kumuomba mke wako msamaha unapoonekana kumukosea ni jambo la busara Sana.

5. NIVUMILIE
Jambo hili wanaume pia linawakumba Sana kwa sababu wake zao wanapo waomba vitu wakati huo hawana, wanakasirika na kusema kwa hasira kwamba SINA,NITOE WAPI? au USINISUMBUE. Lipo neno la kusema hapa nalo no nivumilie mke wangu au mme wagu.

Fanya uamuzi leo ukatamke maneno haya kwa mwenzi wako.
 
Ndoa gani tena jamani?
255788363637_status_3db06ab39ce34996a4242f528e7a20c7.jpeg
 
ʍkʊʊ ʊʍɛօռɢɛǟ ʄǟċt ........
ռɛռօ ....ռɨֆǟʍɛɦɛ .....ʟɨռǟֆօʟvɛ kɨʟǟ kɨtʊ kառʏ ռɖօǟ......ֆɛʍǟ ռɖօ ɦɨvօ limesahaulika
 
Ahsante ni jambo muhimu sana pia, linamjengea mwenzi wako kuendelea kukufanyia jambo fulani unalofurahia,

Sio unapokea kitu kama buku tu bila kumshukuru, ata ni game pia ukimaliza shukrani ni jambo poa sana
 
ACHANENI NA MAMBO YA NDOA
NYANDUANENI KISHA KILA MTU
ALE KONA AKALALE KWAKE.

KUGANDANA SIYO DILI!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom