Huyu jamaa alikuwa T.O mwaka 2014 advance.
Ila U T.O wako hakubahatisha kwa kuwa wahenga wanasema nyota njema huonekana asubuhi,,,Isaack alianza kuonesha Chechen zake tangu yupo shule ya msingi Filbert Bayi ambapo aliongoza mitihani ya taifa darasa la saba.
O Lev alikuwa anapata alama za kawaida sana ,average kama 54-63 ndizo alikuwa anapata ,hajawahi kushika namba moja.
Alimaliza shule ya sekondari alpha iliyopo dar es salaam.
Siku moja tupo kwenye notes board mimi ,Isaack Shayo na kuna jamaa ambaye sitataka kumtaja jina alikuwa anamtania Isaack kwa kumwita T.O wakati hapo kwenye notes board alikuwa wa 11 na alikuwa na average ya 58 .
Isaack soma yake ilikuwa ya kawaida sana ,
Matokeo ya form four yalipotoka alipata one ya 13 huku somo la history akilamba D.
Advance akaenda kusoma St Joseph Cathedral mchepuo wa PCM .
Huko sasa akawa anasoma kama hana akili nzuri .
Alikazania sana elimu na akawa anapata alama za juu sana kuliko kawaida.
Na dalili za kuelekea U T.O zilianza kuonekana walipoanza mitihani ya Mock(Tahosa) Isaack alifanikiwa kupasua vilivyo pepa la physics na kuibuka wa pili kwa dar nzima.
Hata pia kwenye mahafali ya kuhitimu kidato cha sita Isaack aling'aa vilivyo kwa kuongoza masomo mengi na kuibuka best student.
Sasa kilichobaki akawa anasubiri tokeo la necta tu ili kukamilisha yale maneno aliyokuwa anaambiwa toka awali kwa kuitwa T.O
Tokeo lilipotoka kweli akawa T.O kwa kupata Phy B Chem A Maths A na Computer A.
Sasa nikakumbuka ile siku notes boards jamaa alipokuwa anamtania kwa kumuita T O wakati hata top 5 ya darasa kuingia alikuwa hawezi lakini mchizi kweli advance akawa T.O na nikaamini ule msemo kwamba maneno huumba.......