Peculiar
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 821
- 689
Dakika za mwisho kabisa za shughuli, kabla kila mtu hajachukua njia yake.
Mama aliniita pembeni na kuniambia,"najua umeshaambiwa mengi sana mwanangu, naomba uyazingatie na haya nitayokwambia pia;
Jambo la kwanza aliloniambia ni hili, 1."usiwe na muda maalumu wa kurudi nyumbani, namna utakayomzoesha mkeo siku ukibadilisha hata kwa dharura italeta matatizo. Ni bora usieleweke muda wako wa kurudi tangu siku ya kwanza ya ndoa, naye atazoea na ataheshimu hivyo.
2. Mpe kipaumbele na msikilize mkeo yeye kwanza kabla ya mwanamke mwingine yeyote, labda niwe mimi mama yako. Mimi sitakusumbua kabisa, labda iwe imebidi. Naona umemnunulia simu kubwa kweli, lile sio pambo, tumia simu yako kuwasiliana na yeye mara kwa mara. Kabla hujamuoa ulishamzoesha kumpigia, kuchati naye, kutaniana naye mara kwa mara ulikua na kazi lakini ulipata muda wa kuchat na kuongea naye kupitia simu. Usiache kuyafanya hayo kwa kisingizio cha ubize.
Hawezi kutumia simu kucheza tu gemu na kuongea na ndugu zake. Anahitaji kuongea na kuchat na wewe kuliko mtu mwingine yeyote.
3.Mpe zawadi. Unajua nini mkeo anapenda, popote utakapokiona kama una kimudu mnunulie, hata kama ni kidogo atashukuru na atafurahi.
4.Wakumbuke wazazi na walezi wake pia. Najua mtakua mnakuja kunisalimia. Lakini pia usisahau kwenda kuwasalimia wakwe zako. Mkeo atafurahi, atajisikia kujaliwa.
5.Unapompa chochote hasa pesa ya matumizi mpe mkononi. Hata kama kalala muamshe umpe, usizoee ukiamka unaacha hela kabatini au mezani. Atakua anaiwaza meza kuliko wewe. Labda kama ni surprise.
6.Mwitikie wito, akikwambia kakumiss, akikuhitaji usichelewe, usimkatili. Usimtafutie sababu za ubize wala nini. Fanya haraka umuone, umsamdie, atulie maana hana mwingine wakumwambia shida zake ila wewe.
7.Muelewe na umvumilie mkeo. Kuna wakati wanawake huwa wanachoka na hawezi kuwa sawa kwa kukuona wewe kila siku. Hawezi kukwambia kuwa kachoka. Usimuhisi vibaya, tafuta safari au yeye mtafutie safari ili aje kwangu au kwa wazazi wake siku mbili tu ashakukumbuka na mambo yanaanza upya.
8.Usiache kumwambia unampenda. Kama ulivyokua unamtakia kabla hujamuoa, endelea na ikiwezekana zidisha kumtakia.
Ikipatikana fursa ya kuongozana naye sokoni, ibadani au popote fanya hivyo. Atajisikia raha na kujivunia wewe hata ukiwa mbali naye.
9.Mfanye mkeo rafiki yako pia msapoti na umsaidie ikiwa anataka kuanzisha au kufanya jambo lolote lenye faida kwake, kwako na familia. Ukifanya hivyo atakuwa muwazi kwako, hatokuficha lolote.
10.Mwisho nataka nikwambie mwanangu. Mwanamke ni mzuri sana katika kulipa, hivyo usimfanyie ubaya kabisa mkeo. Mfanyie wema kadri unavyoweza. Mwanamke yeyote ambaye ni mke,ukimfanyia wema kwa 10% yeye atakufanyia wema kwa asilimia 90%.
Na kwenye ubaya ndio hivyo, ukimfanyia baya asilimia 10% atakulipa kwa kufanyia ubaya 90%.
Na dhambi mbaya katika ndoa ni usaliti. Ukimsaliti na akajua. Utalea mtoto au watoto wasio wako.
Pia usiache kumuomba Mungu ajaalie na adumishe riziki, utulivu na furaha mliyoanza nayo. Nakutakia maisha mema na Mungu awe pamoja nanyi.