Bawabu wa pili
Senior Member
- Nov 14, 2025
- 147
- 432
Nyota wa soka wa Senegal, Sadio Mané, aliwahi kufichua ukweli wa safari yake yenye maumivu, upinzani na ndoto kubwa kabla ya kufanikiwa katika soka la dunia.Mané anasema kuwa akiwa mdogo, mama yake alimwambia wazi kuwa kucheza mpira ni kupoteza muda, akiamini kuwa hakuna njia ya mtoto wa kijijini kama yeye kufanikiwa kupitia soka.
Familia yake ilisisitiza aende shule, lakini moyo wake ulikuwa uwanjani.“Kila asubuhi niliamka na kwenda mtaani kucheza mpira na watoto wenzangu. Niliporudi nyumbani, wakati mwingine nilipigwa kwa sababu ya kukosa shule,” anasimulia Mané.
Upendo wake kwa mpira ulimfanya achukue uamuzi mgumu. Siku moja saa 11 asubuhi, alitoroka kijijini na kuelekea Dakar, akitumaini kupata fursa ya kutimiza ndoto yake. Alikaa huko kwa wiki moja kabla ya familia yake kumtafuta na kumrudisha kijijini.
Baada ya kurejea nyumbani, Mané aliwaeleza wazazi wake msimamo wake kwa uwazi. “Niliwaambia shule si kipaumbele changu kikubwa. Nitasoma kwa mwaka mmoja tu, lakini kama hamtanisapoti katika mpira, nitaondoka tena,” alisema.
Leo tunapozungumza ni Bingwa wa Mataji mawilli ya Afcon, na akiwa na mataji mengine makubwa Duniani katika mpira wa Miguu. Mane aliamua kusimama katika ndoto yake na kutosikiliza kukatishwa tamaa na Familia yake.