Mandhari ya kuvutia angani - mwezi na sayari = moon among planets

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
279
202
MANDHARI YA KUVUTIA ANGANI - MWEZI BAINA YA SAYARI

(For English version see below)

Kuanzia 29 Oktoba hadi 02 Novemba baada ya Mwezi kutoka kwenye giza ya mwandamo siku ya 28 Oktoba.

Kati ya 29 Oktoba na 02 Novemba, Mwezi utauona unasogea angani ukiangalia upande wa magharibi mara baada ya Jua kutua kuanzia saa 12:30 jioni.

--
Tarehe 29, Jumanne, Mwezi utaanza kuonekana kama hilali nyembamba karibu na sayari Zuhura, ambayo sasa imeanza kuonekana kama nyota inayong'aa mara tu anga likipata giza upande wa magharibi.

Jirani na Mwezi na Zuhura iko sayari ndogo ya Utarid (Mercury) na hizo tatu, Utarid, Zuhura, na Mwezi zikiwa katika mstari mmoja.

29th.png

--
Siku ya 30 Oktoba, Jumatano, Mwezi utakuwa umesogea juu kwa nyuzi 12 na hilali itaonekana kati ya Zuhura na sayari nyingine inayong'aa Mstarii (Jupiter)

30th.png

Tarehe 31 Oktoba hilali ya Mwezi utasogea zaidi nyuzi 12 na utaonekana jirani kabisa na Mshtarii kwa kiasi cha nyuzi moja tu ambayo ni sawa na upana wa Mwezi mara mbili.

31.png

--
Tarehe 1 Novemba hilali kubwa itaonekana kati ya Mstarii na Zohali (Saturn)

01.png

Na siku ya pili tarehe 2 Novemba Mwezi utakuwa karibu nusu na utaonekana juu ya Zohali nyuzi 60 juu ya upeo wa magharibi.

02.png

--
Utaona kuwa sayari zote zimejipanga mstari angani ambao unajulikana kama Ekliptiki na Mwezi unafuata mstari huo wakati unasogea angani siku hadi siku. Mstari wa Ekliptiki unaunganisha Jua pia katika upeo wa magharibi.

Mstari huu unatokana na Mfumo wa Jua kuwa wa bapa moja ambamo vitu vyote katika mfumo huu vinapatikana, kuanzia sayari zote na Dunia na Mwezi na vingine vipo katika bapa moja hii kwa hiyo tunapoona sayari na Mwezi na Jua kwa muono wetu kutoka Duniani vinaonekana katika mstari mmoja.

........
Ukiangalia kwa makini picha hizi zilizotolewa kutoka programu ya Stellarium (Stellarium Astronomy Software), na kufuatilia nafasi za sayari kulingana na nyota za jirani zake utaona kuwa sayari nazo zinasogea juu siku hadi siku ambayo ni kutoka Magharibi kwenda Mashariki.

Hii inaonesha kuwa vitu vyote katika mfumo wetu vinasogea angani kutoka Magharibi kwenda Mashariki.

Mwezi ukisogea 29th to 02 Nov baina ya Zuhura, Mstarii na Zohali.png

ENGLISH VERSION

ENLIGHTENING VIEWS OF MOON AMONG THE PLANETS IN THE SKIES AFTER SUNSET

Very interesting views of the Moon and planets will be seen from 29 October to 02 November after the Moon emerges from darkness of New Moon on 28 October.

From 29th October to 02nd November the Moon shifts is position in the west sky seen soon after sunset from 6:30 PM.

On 29th, the Moon starts off as a very thin crescent close to Venus, which is now seen as a bright star once it darkens a bit in the west.

Close to Moon and Venus there is Mercury with the triplet, Mercury, Venus, Moon appearing in a line.

29.png

On 30th October the Moon will have shifted upwards by 12 degrees and the crescent will be between Venus and another bright planet Jupiter

30.png

On 31st October the crescent Moon will have moved up further 12 degrees and will be seen very close to bright Jupiter separated by only 1 degree which is two Moon widths.

31.png

On 1st November a larger crescent will be between Jupiter and Saturn

1.png

And on 2nd November almost half Moon will be see just above Saturn now nearly 60 degrees above the horizon.

2.png

You will see that the planets lie along a line called the ecliptic and the Moon shifts along that line which also connects to the Sun on the horizon.

This happens because our Solar System is a flat system in which all planets and Earth and the Moon lie in a flat plane and we are observing the flat system from Earth ALONG the flat plane.

If you observe closely the positions of the planets and nearby stars in these pictures obtained using the Stellarium program (Stellarium Astronomy Software) you will notice that even the planets are shifting slightly day by day upward which is away from West towards the East similar to the shifting of the Moon.

This shows that objects in our Solar system are moving in the skies from West to East.

Movement of Moon 29th to 02 Nov among Venus, Jupiter and Saturn=.png
 
MANDHARI YA KUVUTIA ANGANI - MWEZI BAINA YA SAYARI

(For English version see below)

Kuanzia 29 Oktoba hadi 02 Novemba baada ya Mwezi kutoka kwenye giza ya mwandamo siku ya 28 Oktoba.

Kati ya 29 Oktoba na 02 Novemba, Mwezi utauona unasogea angani ukiangalia upande wa magharibi mara baada ya Jua kutua kuanzia saa 12:30 jioni.

--
Tarehe 29, Jumanne, Mwezi utaanza kuonekana kama hilali nyembamba karibu na sayari Zuhura, ambayo sasa imeanza kuonekana kama nyota inayong'aa mara tu anga likipata giza upande wa magharibi.

Jirani na Mwezi na Zuhura iko sayari ndogo ya Utarid (Mercury) na hizo tatu, Utarid, Zuhura, na Mwezi zikiwa katika mstari mmoja.

View attachment 1246749
--
Siku ya 30 Oktoba, Jumatano, Mwezi utakuwa umesogea juu kwa nyuzi 12 na hilali itaonekana kati ya Zuhura na sayari nyingine inayong'aa Mstarii (Jupiter)

View attachment 1246750

Tarehe 31 Oktoba hilali ya Mwezi utasogea zaidi nyuzi 12 na utaonekana jirani kabisa na Mshtarii kwa kiasi cha nyuzi moja tu ambayo ni sawa na upana wa Mwezi mara mbili.

View attachment 1246751
--
Tarehe 1 Novemba hilali kubwa itaonekana kati ya Mstarii na Zohali (Saturn)

View attachment 1246753

Na siku ya pili tarehe 2 Novemba Mwezi utakuwa karibu nusu na utaonekana juu ya Zohali nyuzi 60 juu ya upeo wa magharibi.

View attachment 1246754
--
Utaona kuwa sayari zote zimejipanga mstari angani ambao unajulikana kama Ekliptiki na Mwezi unafuata mstari huo wakati unasogea angani siku hadi siku. Mstari wa Ekliptiki unaunganisha Jua pia katika upeo wa magharibi.

Mstari huu unatokana na Mfumo wa Jua kuwa wa bapa moja ambamo vitu vyote katika mfumo huu vinapatikana, kuanzia sayari zote na Dunia na Mwezi na vingine vipo katika bapa moja hii kwa hiyo tunapoona sayari na Mwezi na Jua kwa muono wetu kutoka Duniani vinaonekana katika mstari mmoja.

........
Ukiangalia kwa makini picha hizi zilizotolewa kutoka programu ya Stellarium (Stellarium Astronomy Software), na kufuatilia nafasi za sayari kulingana na nyota za jirani zake utaona kuwa sayari nazo zinasogea juu siku hadi siku ambayo ni kutoka Magharibi kwenda Mashariki.

Hii inaonesha kuwa vitu vyote katika mfumo wetu vinasogea angani kutoka Magharibi kwenda Mashariki.

View attachment 1246757

ENGLISH VERSION

ENLIGHTENING VIEWS OF MOON AMONG THE PLANETS IN THE SKIES AFTER SUNSET

Very interesting views of the Moon and planets will be seen from 29 October to 02 November after the Moon emerges from darkness of New Moon on 28 October.

From 29th October to 02nd November the Moon shifts is position in the west sky seen soon after sunset from 6:30 PM.

On 29th, the Moon starts off as a very thin crescent close to Venus, which is now seen as a bright star once it darkens a bit in the west.

Close to Moon and Venus there is Mercury with the triplet, Mercury, Venus, Moon appearing in a line.

View attachment 1246770

On 30th October the Moon will have shifted upwards by 12 degrees and the crescent will be between Venus and another bright planet Jupiter

View attachment 1246772

On 31st October the crescent Moon will have moved up further 12 degrees and will be seen very close to bright Jupiter separated by only 1 degree which is two Moon widths.

View attachment 1246773

On 1st November a larger crescent will be between Jupiter and Saturn

View attachment 1246774

And on 2nd November almost half Moon will be see just above Saturn now nearly 60 degrees above the horizon.

View attachment 1246775

You will see that the planets lie along a line called the ecliptic and the Moon shifts along that line which also connects to the Sun on the horizon.

This happens because our Solar System is a flat system in which all planets and Earth and the Moon lie in a flat plane and we are observing the flat system from Earth ALONG the flat plane.

If you observe closely the positions of the planets and nearby stars in these pictures obtained using the Stellarium program (Stellarium Astronomy Software) you will notice that even the planets are shifting slightly day by day upward which is away from West towards the East similar to the shifting of the Moon.

This shows that objects in our Solar system are moving in the skies from West to East.

View attachment 1246776

Hizi ni picha za sayari zilipigwa leo jioni magharibi mara baada ya Jua kutua saa 12:30 jioni

Hii ya kwanza ni Zuhura (Venus) na Utarid (Mercury) ambayo inaonekana kushoto kwa juu ya Zuhura
Venus and Mercury.jpeg

Hii ya pili inaonesha Zuhura chini na Mstarii (Jupiter) juu
Venus and Jupiter.jpeg

Picha hii inaonesha Mstarii chini na Zohali (Saturn) juu
Jupiter and Saturn=.jpg
 
Back
Top Bottom