Mandela Road: Barabara iliojengwa kwa viwango stahiki

HIyo ni Sam Nujoma road sio Mandela road
 
Ilijengwa/ilikarabatiwa tena kipindi Cha Jakaya Kikwere na makandarasi MALTAURO-SPENKON kuanzia mwaka 2008- 2011 toka bandarini mpaka Ubungo mataa. Ile ya Mowlem ilibomolewa
huyo kachanganya hiyo ni Sam Nujoma road sio Mandela expressway unayoiongelea
 
Sasa mbona naona picha za sam nujoma road??
 
Mandela Road inaanzia Bandarini mpaka Ubungo Mataa.

Sam Nujoma Road inaanzia Ubungo Mata hadi Mwenge.

Picha ulizozipiga ni za Sam Nujoma Road na siyo Mandela Road
 
Kweli Kabisa mkúu huyo mkandarasi apewe Maua Yake.

Na aliyejenga kipande cha Shinyanga hadi Mabuki hao watu walikuwa watu kwerikweri
 
Kutoka Chalinze kwenda Morogoro barabara hii naikubali sana

Moja ya kipande kizuri sana cha lami zilizopo Tanzania...mahali pabaya ni ninapokumbuka ni maeneo ya Bwawani na Mikese...
 
Kipande kingine bora na pengine kilichodumu muda mrefu kwa barabara za Dar ni barabara ya Ali Hassan Mwinyi kipande cha kuanzia Maktaba hadi Morocco (Morocco kwenda Mwenge kimejengwa upya)...

Hii barabara kwa kumbukumbu zangu nadhani ilijengwa 1993/94 hapo, sijui kama iliwahi bomolewa na kujengwa tena...
 

Mandela road yenyewe imejengwa miaka ya 1970s.. na mpaka leo haijawai kurekebishwa rekebishwa kama zingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…