Mandela Road: Barabara iliojengwa kwa viwango stahiki

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,826
9,533
Hii barabara pichani kwa jina MANDELA Road, ndio barabara yangu yenye ubora kabisa.

Kwanza, imedumu bila kubonyea bonyea, kuweka mabigijii kama ilivyo baadhi ya barabara zenye heavy traffic

Pili, imezingatia haki za watumiaji wote. Inayo sehemu ya mapitio ya dharura, waenda kwa miguu na magari pande mbili.

Ina mifereji mipana saafii inayopitisha maji vizuri.

My take:
Mkandarasi aliejenga hii apewe tena kazi ya barabara muhimu kv Moro Kibaha Express Lane nk. Heko alempa kazi na standards za kuzingatiwa.

Huu ni mfano bora.

UZI TAYARI

17050495785422006792535499259023.jpg
20240112_114633.jpg
 
Hahahahaha😀😀😀
Jielimishe kwanza. Hiyo sio Mandela Rd, ni Sam Nujoma Rd.
Hiyo barabara ina mazingira mazuri tu inavutia kuendesha, lakini haina ubora. Lau magari yanayopita Mandela Rd yanayobeba macontainer na heavy traffics yangekuwa yanapita hapo usingeisifia hiyo barabara.

Aliyejenga Mandela Rd yenyewe kuanzia Ubungo hadi Kurasini naomba tumsifu, kajitahidi sana. Mabigijii yapo, hasa sehemu ambazo kuna traffic lights kwa sababu magari mazito yanasimama kwa muda kama pale Serengeti na Tabata. Ila angalau amethubutu.
 
Hii barabara pichani kwa jina MANDELA Road, ndio barabara yangu yenye ubora kabisa.

Kwanza, imedumu bila kubonyea bonyea, kuweka mabigijii kama ilivyo baadhi ya barabara zenye heavy traffic

Pili, imezingatia haki za watumiaji wote. Inayo sehemu ya mapitio ya dharura, waenda kwa miguu na magari pande mbili.

Ina mifereji mipana saafii inayopitisha maji vizuri.

My take:
Mkandarasi aliejenga hii apewe tena kazi ya barabara muhimu kv Moro Kibaha Express Lane nk. Heko alempa kazi na standards za kuzingatiwa.

Huu ni mfano bora.

UZI TAYARI
Hii ni barabara ya sam nujoma road ila barabara zote 2 pamoja na ya mandera road zilichokwa kwa msaada wa pesa ya watu wa ulaya( European union) kwa hiyo hiyo ujengaji umeendana na viwango vyao walivyojiwekea kwa kumpa tenda mkandarasi wanaomjua wao.
 
Ilijengwa/ilikarabatiwa tena kipindi Cha Jakaya Kikwere na makandarasi MALTAURO-SPENKON kuanzia mwaka 2008- 2011 toka bandarini mpaka Ubungo mataa. Ile ya Mowlem ilibomolewa
Wameweka taa siku hizi?
 
Hongera kwa kutoa kongole. Nakumbuka kuna siku niliamua nitoe uchovu wa mwili nikaamua kukanyaga kwa mguu kutoka Ubungo mpaka Mwenge, yaan nilitembea bila bughudha eneo la watembea kwa miguu. Aliyeijenga kuanzia mtoa tenda na mpokeaji wapewe pongezi walizingatia mambo ya muhimu.

Ila mkuu samahani hiyo camera yako inaumwa mafua?
 
Back
Top Bottom