Wakati mwingine malori yanaachiwa kutoka bandarini kwa wakati mmoja basi yatajipanga kuanzia Ubungo hadi Uwanja wa Taifa, hiyo njia imetuponza wengi has ukiwa unawhi airport anza safari masaa 3 kabla!
Jana Nape alienda UDOM kusimamia kuziba nyufa, nina imani amesikia kilio cha foleni na atakuja na solution ya kumaliza tatizo la traffic jam hapa mjini. Nape, baada ya kuziba nyufa Udom, pse njoo utuokoe na hili janga la traffic jams mjini
Kipande cha kati ya Buguruni-Chama na TAZARA, kuna Reli inayokatisha barabara pale, imeng'olewa na upande mmoja wa barabara umefungwa. Kuna foleni ya kimtindo hivi, so mnaoweza kuepuka kwa kutumia barabara nyingine inabidi muangalie uwezekano huo, kwani kama hali iko hivi saa hizi, nadhani jioni hapatapitika!
Hivi hiyo barabara ya Mandela ujenzi wake UMEKAMILIKA; UMESITISHWA; UMETELEKEZWA au ni nini hasa kinaendelea pale???Ukienda Buguruni kwenye makutano utaona vitu vya ajabu...Huku kati maeneo ya relini nako ni vituko!! Jamani nisaidieni wenzangu; nini kinaendelea kuhusu mustakablai wa barabara hiii!!! Siku hizi nikiwa natoka Mwenge kwenda au kutokea Ukonga na Uwanja wa ndege SITAKI KUSIKIA WAZO la kupita barabara hiyo kwani mara ya mwisho nilipopita nilitumia muda ambao mtu aliyekuwa anasafiri kwa bus toka Ubungo kwenda Tanga alifika mie nikiwa bado nashangaa kwenye junction ya kwenda Chuo Kikuu cha Dar es Salaam!!!! GOD HELP Tz
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.