Tueke siasa pembeni kidogo hapa.The lying about COVID19 situation in Tanzania is now costing the country big time and I am not sure it’ll be for how long.
Sasa si tunajua jinsi Covid19 inavosumbua mataifa ya wenzetu au sio? wanakufa hadi watu 4000 kwa siku au sio? Tunakuta wenzetu wana karantini, wanatumia kila mbinu kujikinga lakini bado wanakufa kwa mafungu ya nyanyakama vyombo vyao vinavosema au si kweli?
Hebu turudi hapa kwetu Tanzania tuone uhalisia wa mambo.
Si unaona pale kariakoo watu wanavyosongamana? si unaona hakuna tahadhari yoyote inayochukuliwa? si unaona kwenye usafiri wa umma mambo yalivyo? yaani in short, si unaona kuwa watanzania hatuchukui tahadhari na tunaishi kama hamna corona vile? Kweli sisi wakukosa vifo 4000 na kuendelea kwa siku? na kama ni ivo kweli, kweli tunaweza kuficha vifo vyote ivo namna hio? Okay labda Tanzania bara ni nchi kubwa na watu wengi na maeneo ya kuzika yanaweza kuwa mengi na mengine mtu usijue yako wapi.
Tuje nyumbani kwetu Zanzibar, visiwa vyenye watu milioni 1 na nusu labda tuseme. Kwenye suala la tahadhari hakuna tofauti na bara kabisa.
Kweli kutokee vifoo vingi vya corona Wazanzibari tusijue? Jinsi ilivokuwa hatuna tahadhari, si ajabu sote wazanzibari tukawa na corona.
Turudi kwenye Siasa kidogo,
Leo hii wagombea upinzani hao hao ambao wanasema Serikali inaficha data, wanakwenda kwenye mikutano wakiwa hawana barakoa, na watu wamekusanyika hamna tahadhari yoyote..
What is happening sasa?
Kifo lazima kikuumbuwe tu.