Huo ndio ukweli , Kama unaangalia mpira kwa jicho la 3 , tatizo la Man u sio Maguire Ni structure mbovu
Tena Man u bila Maguire ina record mbaya
1 win in 11 without Maguire
Without Maguire this season:
7 draws
2 losses
0 wins
Just the 1 clean sheet (0-0 against watford) in those 9 games.
mkuu huu mpira tunaocheza sasa tumeanza kucheza takribani mwezi mmoja uliopita chini ya ralf rangnick baada ya kuona wachezaji hawataki kubadilika na kufuata matakwa yake, mechi ya kwanza ya crystal palace tulianza kuimplement gengenressing na wengi wetu tulifurahia performance ile japokuwa tulicheza kwa higher energy kwa dakika 30 lakini kwa kuwa ilikuwa mechi ya kwanza kocha aliridhika, kupitia mechi ile tuliweka rekodi ya kupokonya mara 14 kama nitakuwa sahihi, tokea aondoke ferguson rekodi kubwa ya kupokonya mpira dhidi ya adui ilikuwa dhidi ya arsenal na tuliwapokonya mara 9 hadi 12 (nimeshasahau zile takwimu) . Balaa lilianzia mechi ya pili tuliocheza dhidi ya norwich city na 4-2-2-2 yetu, licha ya kupata ushindi wa goli 1 lakini performance yetu haikuwa nzuri. Baada ya kumalizika kwa mechi hiyo ralf alitanabahisha matatizo makuu mawili alioyaona nayo ni udhaifu wa wachezaji katika kugombania mpira dhidi ya adui na kushinda 1v1 kwa kutumia mwili (physicality) na kukosekana muamko (intensity) wa kupambana muda wote wa mchezo dhidi ya timu inayokimbia vizuri, inayojilinda vizuri na inayomiliki mpira vizuri kama walivyofanya norwich city siku hiyo. Ina maana ilimchukua ralf rangnick wiki moja tu kuyaona matatizo makuu ya timu ilioachwa na OLE, ila tatizo hili la intensity na physicality lilianza chini ya mourinho (rejea interview yake baada ya kufungwa na liverpool naye aliyalalamikia mambo hayo huku akiwasifia sadio mane na salah kwa kuongoza kikosi kazi cha liverpool maeneo hayo, kwa sasa natumia kimeo hivyo sitoweza kuweka link ya youtube), bila ya shaka matatizo hayo mawili(phyisicality and intensity) yametokanwa na poor recruitment yetu tulioifanya kwa hii miaka 9 kwa sababu haiwezekani makocha wote watatu wayagusie matatizo hayo kwa nyakati tofauti,nje ya fred na mctominay hawa kina martial, lingard, lindelof, rashford, greenwood, bruno, telles, dalot na mata wote wana ugonjwa huo na sioni wakibadilika kiurahisi. Kuhusu mpira tunaocheza wa kuacha space kubwa ndani ya uwanja mbona ndani ya thread hii huko nyuma tumeshayazungumza na shahidi atakuwa ni
fuentte na
PTER . Tatizo hii limeletwa na OLE na si ralf rangnick baada ya kuona wachezaji alionao hawawezi kumpa anachokihitaji, tukumbuke OLE alijinasibihisha ya kwamba yeye ni muumini mkubwa sana wa mpira anaofundisha klopp na atataka wachezaji wake wawe fiti kama liverpool na bahati nzuri hayo yalifanyika vizuri sana mechi 10 za mwanzo chini yake na tukaingiwa na matumaini makubwa sana kumbe ilikuwa ni honeymoon. Baada ya kufungwa na everton kwa magoli manne ole alisema wachezaji wengi waliocheza leo hawatakuwepo msimu ujao kwa sababu hawaendani na falsafa zangu cha ajabu mpake leo wameondoka wawili tu ambao ni smalling, na lukaku wengine mpaka leo tunao. Swali linakuja Kwa nini tulikuwa tunapata matokeo mazuri chini yake licha ya kucheza mpira huo wa kuacha nafasi kubwa, hatufanyi pressing (timu yetu haikuwa nzuri kitakwimu za pressing, natumai chief atanisaidia takwimu), hatulindi set piece ipasavyo, tunafanya comeback mara kwa mara dhidi hata zile dhaifu)?.......Jibu ni rahisi nyakati zile wachezaji walionyesha ari ya kupambana (attitude) pamoja na kusimama na mwalimu ila walipomchoka naye wakamfukuzisha.. Tukirudi mechi ya 3 kwa ralf rangnick tulicheza dhidi ya newcastle na tukatoka draw, kwa mara nyengine ralf akagusia tena matatizo mawili ya phyisicality, intensity na pia akaongezea udhaifu wetu wa kushinda second ball dhidi ya adui na running au sprinting (hatukimbii kwa haraka a.k.a wavivu). Mechi ya 4 tunafungwa na wolves hatimaye akaachana na 4-2-2-2 ya kutumia namba 10 wawili na akaimplement 4-3-3 baada ya kurudi kwa paul pogba mechi ya FA dhidi ya middlesbrough na hapo alianza kutumia namba 8 wawili lakini uwanja bado tulikuwa tunaubana (low space), hapa yakazaliwa matatizo mengine mawili nayo ni kuchoka haraka (tukaitwa timu ya dakika 30) pamoja na udhaifu wa kufunga magoli (tulitengeneza nafasi tukizidiwa na liverpool tu lakini kwenye kufunga magoli tukaachwa mbali sana) hatimaye tukatowa draw na aston villa, burnley, southampton na tukatolewa kwa penalty na middlesbrough. Mechi ya leicester city ndio ilizidi kumkera ralf rangnick, goli tulilofungwa na leicester city tulishuhudia ndani ya sekunde 3 hadi 10 wachezaji wa leicester walionyesha utayari wa kugombania mpira maeneo ya hatari kwa kuingiza mwili bila ya uoga (tielemans alimfanyia tackling fred na kuwin mpira, beki wa kushoto wa leicester naye akamfanyia tackling bruno aliyeogopa kuweka mguu wake hatimaye akawa anamtegemea refa ampe advantage ya foul, beki wa kushoto wa leicester akapiga krosi iliozaa goli la iheanacho), hata ya mechi atletico tukafungwa goli kama hilo baada ya elanga kushindwa nguvu na mchezaji wa atletico akaanguka chini na akasubiri advantage ya refa hatimaye ikapigwa counter attack na tukafungwa baada ya mpira wa krosi. baada ya kumalizika kwa mechi ile ya leicester ralf rangnick akaacha kabisa kuzungumzia ishu ya intensity na physicality baada ya kugundua wachezaji hawaonyeshi utayari. ndipo zikavuja taarifa za ralf kutowa mapendekezo 4 ya kufanywa na bodi kuanzia sasa ili kuweza kuirudisha timu ya ushindani dhidi ya liverpool na man city, miongoni mwa mambo aliyoyapendekeza (1) ujio wa kocha mwenye utambulisho wa mpira unaoeleweka, hapa nilivyotafsiri mimi alikuwa anampigia kampeni erik ten hag mbele ya pochettino asiyejulikana falsafa yake ni ipi mpaka leo. huko nyuma tulijadili sana humu ndani kuwa ole gunnar na lampard hawana filosofi inayoeleweka na hivyo watapitwa na arteta lakini wengi hawakunielewa,
fuentte atakuwa shahidi wangu (2) usajili wa wachezaji uendane na matakwa ya mwalimu husika, pia wasajiliwe wachezaji wanaojijenga na si wale walioridhika kimafanikio. (3) wasajiliwe wachezaji wenye uwezo wa kupambana kwenye mazingira yeyote ya mechi kinguvu, speed, intensity na skills. Kwa sasa naye rangnick karudisha 4-2-3-1 ya ole kuanzia mechi ya tottenham hotspurs, hatufanyi pressing ya nguvu kama anavyotaka, tunaacha gape kubwa kati ya mstari wa beki, kiungo na striker. Mechi ya liverpool aliwaambia wachezaji wasiwafanyie high pressing (tusikabe juu) liverpool kwa sababu wao ni mahodari wa kufanya counter pressing ila cha ajabu ndani ya dakika 3 tokea kuanza kwa mechi wachezaji wanakwenda kukabia juu na hatimaye dakika ya 4 tunafungwa baada ya liverpool kubypassing pressing yetu, je hapo tumlaumu mwalimu?.... Goli la pili elanga kwa mara nyengine tena anashindwa kuweka mwili kwenye vita yake na robertson hatimaye tunamtegemea refa (intensity and physicality), goli la 4 maguire anapiga pasi mbovu kwa hannibal, poor control pamoja na udhaifu wake wa kimwili (physicality) unamfanya apoteze mpira huku wachezaji wengine wakiwa nje ya mchezo. Kwa sasa ralph rangnick ameamua kuchukua mshahara wake kimya kimya, ameacha kuzungumzia kabisa hadithi za kujenga msingi wa gengen pressing. Nawapa assignment, nitafutieni clip 5 zinazomuonyesha bruno ambaye ni mchezaji tegemeo akishinda vita ya kugombania mpira na adui bila ya kumtegemea refa ampe fouls. Baada ya hapo katafuteni clip ya goli alilofunga mahrez dhidi brighton muone balaa la kelvin de bruyne anavyoburuta mpira mbele ya wachezaji watatu wa brighton kabla hajatoa assist. Pia nitafutieni mechi moja ya bruno aliocheza kwa kiwango cha juu dhidi ya timu kubwa nami nitawatafutia nyingi za salah, gundogan, kdb, mane, kante, kovacic, modric. Rafiki yangu
PTER aliwahi kusema bruno ni mark noble aliyejaaliwa ufundi. Sijafanya setting nzuri kwa sababu ya kutumia kitochi hapa nilipo hivyo vumilia porojo langu. ole alibebwa na attitude ya wachezaji, ralf ameangushwa na attitude ya wachezaji.