Manchester city bingwa mpya wa uefa champions league 2019/2020

Aen Urner

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
358
351
Habari zenu wanasports,

Kwa kuweka kando ushabiki nimechunguza na kufanya analysis Kwa timu zilizobaki mpka Jana kwenye michuano ya kombe la ulaya ngazi ya vilabu (UEFA CHAMPIONS LEAGUE).
Nimegundua city hawana cha kupoteza msimu huu.

Kiu ya kubeba UCL imemkaba Pep, nahisi asingekuwepo Etihad mpaka sasa kama angekuwa ameshatwaa kombe hili, Hana alichobakisha Kwa CITY zaidi ya Uefa, ni wakati maridhawa kabisa Kwa CITY kunyanyua ndoo katika kipindi ambacho vidume wa ulaya LIVERPOOL washalamba mchanga, BARCELONA na Wenzao wa Bernabeu Tia maji, Tia maji, changamoto pekee Kwa city inabaki kuwa Bayern Munich ambayo Kwa mbinu na uzoefu alonao Pep guardiola sioni Bayern wakiwazuia City kutwaa ubingwa msimu huu.
Mwisho,

CITY BINGWA MSIMU HUU,
UNA MAONI AU MTAZAMO TOFAUTI NA HUU, KARIBU!!!
 
Mkuu mapema mno don't count eggs before they hatch!
Naona kwenye hesabu zako umewatoa kabisa Atletico Madrid, PSG, Juve, Bayern, Barcelona na wengine.
Mpira haupo hivyo mkuu, jana Liverpool walipiga Shots 34 langoni kwa Atletico yakaingia mawili (2) tu, huku Atletico alipiga 10 yakaingia matatu (3).
 
Mkuu analivyoperform altletico Kwa Liverpool, sivyo anavyoweza kuperform Kwa CITY, liver wamechoka kiaina, ilikuwa lazima wapumzike, city ndo timu pekee ya kuichanganya altletico na kuitoa. Trust!!!
 
Mkuu analivyoperform altletico Kwa Liverpool, sivyo anavyoweza kuperform Kwa CITY, liver wamechoka kiaina
Uliangalia mechi yao bila ushabiki wa kuipenda ua kuichukia timu flani kati ya hizo mbili?
Liverpool walitakiwa wamalize mechi dakika 90 tu, walipiga mashuti mengi mno golini.
It was a save after save encounter.
Msifie Jan Oblak na umuombee mabaya ikitokea timu yake inakutana na Man City huko mbele ya safari.
 
Mkuu nkujuze Tu, kwamba hakuna kocha yoyote duniani anayefurahia kipa wake kuwa MAN OF THE MATCH., Sawa atampongeza lakini kichwani atakuwa anaumizwa na hicho kitu, akitafuta namna sio ya kukiendeleza Ila kukiondoa kabsa.
Kwhyo ukiona oblak anafanya saves nyingi, ujue upande wa pili(strikers) either hawana accuracy au ubunifu, next time ukikutana na striker Wengine wenye ubunifu na accuracy wanaweka kamba.
 
Sawa mwamba.
Bado nasisitiza usitukane mamba kabla haujavuka mto.
Real Madrid bado anayo nafasi kuitoa City achana na hao akina Atletico.

Walichofanya akina Sala, Mane na Firmino kimefanywa sana na akina Raheem Sterling, Aguero na Jesus msimu huu.
Wamekuwa wakipiga mashuti mengi sana na kufunga goli chache kulinganisha na mashuti waliyopiga kuelekea golini kwa mpinzani.
 
Back
Top Bottom