MANARA: Nimeumbwa na moyo mgumu, ninatamani kufanya kitu ila dhamira inaniambia nimsamehe

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
16cd53e66e78beb535ab1c5020a76da4.jpg
"Nimeumbwa na moyo mgumu, ninatamani kufanya kitu, ila dhamira inaniambia nimsamehe, na Mola wangu Inshaallah atamsamehe, tujiepushe na ushabiki wa matusi, tambua Mungu ni wetu sote". Ameandika Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara kwenye mtandao wa Instagram.

My take: Jamani huu ni ushabiki wa kijinga namna hii tuache. Na tuwe mstari wa mbele kulaani unyama huu, tuondoe tofauti zetu kwa kukemea mambo kama haya. Akili gani hii ya kumtusi mtu pamoja na kejeli kwasababu ya ushabiki wa mpira kwa maumbile ya binadamu mwenzako.! Hakika si jambo jema hata kidogo, tuwe na hofu na Mungu. Na tukumbuke kuwa Kabla hujafa hujaumbika.
 
Kwenye kumtusi kulingana na asili ya uumbaji wake nina laani kwa nguvu zote, sio sawa na uungwana,

Ila kwenye kufungiwa mwaka mzima na 9M , naona poa tu na ndo maana namkumbusha Haji kuwa Siku zote muosha huoshwa....akumbuke alivyomchongea Jerry Muro mpaka akapigwa korokoroni na Tifu-Tifu.
Na yeye akaungane nae benchi wangojee sub .
 
Personification sio nzuri ila kumfingia kwa manara na soka ni poa tu maana ameleta hoja ambazo sio za kisoka.
ni sawa,lkn hayo ya kuingilia kazi ya Mungu sio sahihi.mimi young african sport club, lakini siwezi kuandika ujinga huo
 
Kumbeza mlemavu yoyote ni upumbavu na kukosa usataarabu uliopitiliza.
Aliewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya uingereza GLENN HODLE,aliwahi kushinikizwa ajiuzulu na akajiuzulu baada ya kumbeza mlemavu
 
Siku zote muosha huoshwa....akumbuke alivyomchongea Jerry Muro mpaka akapigwa korokoroni na Tifu-Tifu
Tutaniane kwenye mambo ya soka lakini tusivuke mpaka katika kukejeli uumbaji wa mungu.. Haina maana..!
 
Kumbeza mlemavu yoyote ni upumbavu na kukosa usataarabu uliopitiliza.
Aliewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya uingereza GLENN HODLE,aliwahi kushinikizwa ajiuzulu na akajiuzulu baada ya kumbeza mlemavu
Mkuu.. Watu wengine ni hatari katika jamii.Hivi kweli unakosa cha kuandika katika mpira hadi unakashfu mtu kwa maumbile ambayo hakuyataraji, aisee wanadamu tunaleta machukizo mno kwa watu..!
 
Huyo jamaa hana elimu ya kutosha darasani,pia nyumbani kwao alipata malezi ya hovyo kabisa.
Utotoni ilikuwa ukimcheka mlemavu unabebewa msobe msobe hadi kwenu,hicho kipondo utakachopata hutarudia mpaka unaingia kaburini.Na waliofunzwa dini tokea utotoni (wakristo na waislamu)wamefundishwa kutobeza walemavu
 
Na hao sport Extra hawajifuta hiyo post, na kufutilia mbali huyo member wao!? Halafu na wewe mleta mada...sivizuri kuleta post hiyo kama ilivyo(ungetumia tafsida); kwa staili hiyo nawe unashiriki kuneza mawazo ya mkosaji, twaweza kukutafsiri kuwa nawe ni mshirika wake.
 
Tutaniane kwenye mambo ya soka lakini tusivuke mpaka katika kukejeli uumbaji wa mungu.. Haina maana..!
Hapo ni sawa, mambo ya uumbaji yasihisishwe kabisa ila tujadili soka na Kupiga teke bakuri kwa manara

ni sawa,lkn hayo ya kuingilia kazi ya Mungu sio sahihi.mimi young african sport club, lakini siwezi kuandika ujinga huo

Kweli kabisa
 
ni sawa,lkn hayo ya kuingilia kazi ya Mungu sio sahihi.mimi young african sport club, lakini siwezi kuandika ujinga huo
Huyo jamaa ni zaidi ya Shetani. Mambo ya maumbile ya mtu na ushabiki mbona havina uhusiano wowote.Mpuuz sana huyu jamaa
 
Na hao sport Extra hawajifuta hiyo post, na kufutilia mbali huyo member wao!? Halafu na wewe mleta mada...sivizuri kuleta post hiyo kama ilivyo(ungetumia tafsida); kwa staili hiyo nawe unashiriki kuneza mawazo ya mkosaji, twaweza kukutafsiri kuwa nawe ni mshirika wake.
... Hakuna kitu kama hicho sote tuinue sauti zetu kwa kulaani huu udhalilishaji

Mkuu yeye mwenyewe ndo kuweka wazi kwenye mtandao.
 
Back
Top Bottom