MANARA: Nimeumbwa na moyo mgumu, ninatamani kufanya kitu ila dhamira inaniambia nimsamehe

Haji Manara hajawahi kuwa na hoja yenye mashiko kwa soka letu zaidi ya blah blah kama walivyo viongozi wengine wa Simba Koko, lakini heshima yake kama binadamu mwingine yeyote yule inapaswa kulindwa. Huyo aliyepost upuuzi huo anapaswa kuwajibishwa kwa matendo yake.
 
Huyu kijana pamoja na kusamehewa ila anatakiwa achapwe makofi hadharani bila kumuonea huruma.
Vijana wengi ni wajinga wa kupindukia na ukitaka kujua pitia kwenye hii mitandao ndio utajua idadi ya mazezeta katika nchi hii, wakiachwa hivi hivi litakuwa Taifa la vichaa, ni kumtia adabu tu wala si vinginevyo
Sijawahi kumuelewa Manara ila kwenye maumbile yake haikubaliki popote kumdhihaki, na kwenye hili hata sisi Yanga sugu tupo pamoja na Manara.
 
Yule aliyemtukana Manara sio mwanamichezo kabisa.

Sisi mashabiki wa Yanga tunalaani kitendo kile cha kumtukana Manara.

Soka ni furaha na utani, Yanga na Simba ndugu moja.
 
Baad ya kusoma hiyo post yake Leo mchana, nimemlaum Baba yake.. Mama yake.. majirani zake.. na Hata marafiki zake..

Natumaini Huyu sio Sura ya mtanzania aliyeiacha mwalimu Julius
 
16cd53e66e78beb535ab1c5020a76da4.jpg
"Nimeumbwa na moyo mgumu, ninatamani kufanya kitu, ila dhamira inaniambia nimsamehe, na Mola wangu Inshaallah atamsamehe, tujiepushe na ushahidi wa matusi, tambua Mungu ni wetu sote". Ameandika Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara kwenye mtandao wa Instagram.

My take: Jamani huu ni ushabiki wa kijinga namna hii tuache. Na tuwe mstari wa mbele kulaani unyama huu, tuondoe tofauti zetu kwa kukemea mambo kama haya. Akili gani hii ya kumtusi mtu pamoja na kejeli kwasababu ya ushabiki wa mpira kwa maumbile ya binadamu mwenzako. Hakika si jambo jema hata kidogo, tuwe na hofu na Mungu. Na tukumbuke kuwa Kabla hujafa hujaumbika.
Umenena vyema mkuu
 
Hii ndio simba na yanga.

Inafikia hatua mtu anaombea hata basi la timu nyingine lipinduke tu liue timu nzima.
 
Si sawa kabisa nalaani kwa nguvu zote mpumbavu huyo. Kama asemavyo Gwajima akome na asiludie tena.
 
huyo ni mshenzi mmoja ambae hana akili na hajielewi.ila mungu si wa kudhihakiwa kiasi hiki atapata malipo ya dharau zake na matusi yake hapa hapa duniani
 
Nimegundua huyo dogo sio mwanasoka kabisa..ni mtu wa visingeli .. Mungu amsamehe
 
Back
Top Bottom