Ukimaliza kuuguza machungu,urudi hapa...ueleze nini ulikuwa udhaifu wa MU katika hii mechi ya leo?
Mimi niliona baada ya bao walilopata,walianza kucheza kujihami, badala ya kuongeza mashambulizi ili kuongeza mabao. Walinzi wa MU badala ya kumvamia na kumpokonya mpira, wao walikuwa wanamsindikiza Modric kwenda kufunga bao.
Hata baada ya wavu kutinga walibakia wamepigwa na butwaa...maruerue hayajaisha wanaona wavu unatinga tena. MU ganzi iliwatoka baada ya bao la pili, lakini ilikuwa too late.
Watu yenu walijitahidi lakini the special one alikuwa mjanja zaidi katika kupoteza wakati...hata hivyo leo RM hawakufanya sana ile janja ya kujiangusha chini ovyo ovyo.