Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,498
- 37,792
Siku zote Kwa watu Wenye busara tatizo huzaa Somo.
Jana Mwamuzi Stuart Antwel akishirikiana na Waamuzi wa VAR kwenye Mechi ya Mahasimu wa Manchester ameanzisha mtifuano wa hoja dunia nzima. Amewapa watunga sheria na kanuni kazi ya kufanya.
Mpaka Sasa Kila upande Una lake, Hakuna anayekubali kushindwa.
Mwamuzi mstaafu wa England Dermont Gallagher yeye kasema suala lile maamuzi yoyote ya mwamuzi yalikuwa sahihi.
Maamuzi kama haya ndo sehemu sahihi Kwa Waamuzi wetu kuingia darasani na kutuletea maoni sahihi ya "Ni offside au siyo offside?" Rashford anapewa pasi akiwa eneo la kuotea na mpinzani wake Akanji akiwa Mita 4 toka kwenywe mpira na 2 toka Kwa Rashford.
Mfukuzano huo unakwenda umbali wa zaidi ya Mita 20 bila yeyote Kati Yao kugusa mpira wala Akanji kimkaribia Rashford. Wanapokaribia eneo la 18 ghafla anatokea Fernandes na Kupiga mpira ule golini na kufunga.
Unazuka utata ni goli halali au haramu? Antwel anawasiliana na VAR officials kujiridhisha kama mpira uliguswa na Rashford au la? Wao pamoja na Mashika kibendera No. 2 wanasema Rashford hakugusa mpira Kwa umbali wote wa zaidi ya Mita 20 alizofukuzana na mpira ule.
Baada ya maelekezo hayo anaruhusu bao Kwa Man Uta lakini anapingwa vikali na Man City.
Watu wanarudi kwenye kanuni lakini nazo zinazidisha mkanganyiko tu maana Kila mmoja anazituzitumia kuvutia upande wake.
Nani atatutalia Fumbo hili? Ni Peluig Collina au Ramadhani Kayoko? Ni Athumani Kazi au Scars wa JF? Tusubiri huku tukiendelea kutoa maoni Kwa kutumia vielelezo na hoja jadidi.