Ligi Kuu Bara: Toto Africa vs Yanga Africans

Danny greeny

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
3,856
1,648
Dk 90, Kimanzi anapiga shuti lakini mpira unapita juu kidogo ya lango

Dk 89, Yanga wanatumia akili zaidi, wanacheza taratibu huku wakizuia mpira kwenda kwenye lango lao

SUB DK 88, Evarist Benard anaingia kuchukua nafasi ya Waziri Junior kwa upande wa Toto

Dk 87, Anthony anapiga shuti kali akiwa umbali wa takribani mita 27 hivi, linatoka nje kidogo ya lango la Yanga

Dk 86 krosi safi kabisa ya Kimanzi lakini inapita juu ya lango la Yanga

Dk 83 hadi 85, Yanga wanaonekana kumiliki mpira kupoteza muda, lakini Toto hawana presha kubwa kuwapokonya

Dk 82, Ngoma anaangushwa na taratibu anaibuka na Juma Abdul anauchonga mpira ule kwa shuti kimo cha paka lakini Toto wanaokoa

SUB Dk 79 Yanga inafanya mabadiliko kwa kuwatoa Kaseke, Tambwe, Niyonzima na kuwaingiza Matheo, Kamusoko na Busungu. Kocha Hans van der Pluijm ameamua kufanya sub ya watu watatu kwa mpigo

GOOOOOOO Dk 77 Juma Abdul anaifungia Yanga bao safi kwa shuti kali, ilikuwa ni baada ya kipa kuokoa mpira wa kurushwa wa Oscar Joshua, mabeki wakaokoa shuti la Msuva na Juma Abdul akatandika shuti kali kabisa

Dk 74, Matheo Anthony, Thabani Kamusoko na Malimi Busungu wanaonekana wakipasha misuri pale nje

Dk 72, Khatibu anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa krosi wa Juma Abdul inakuwa kona, inachongwa na Kaseke lakini ni rahisi kabisa kwa kipa

Dk 65 hadi 69, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja, hakuna mashambulizi makali

Dk 63, Kimanzi anamtoka Bossou hapa na yeye anamvuta na kumwangusha kwenye eneo la hatari lakini mwamuzi anasema ni kona inachongwa na kuokolewa kwa mkono na Dida

Dk 62, al manusura Ngoma afunge bao la pili la ,mpira wake unapita juu kidogo ya lango la Toto

KADI Dk 62 Carlos Protas anaonyeshwa kadi ya njano kutokana na kulalamika. Awali alilalamika na Tambwe akasawazisha

Dk 58 hadi 61, inaonekana mpira unachezwa katikati zaidi ingawa wachezaji wa Toto wanaonekana kuwa na hasira

Dk 57, kipa anatoka na kuokoa kwosi safi ya Joshua na Ngoma tayari alisharuka juu

DK 56 mwamuzi anawaita Tambwe na Mlipili na kuwaambia waache maneno na kucheza soka

Dk 55 sasa, timu zote bado zinacheza zikionekana kusaka mabao....lakini Toto African wanaonekana kutokuwa makini sasa katika safu ya ulinzi

GOOOOOO Dk 50, Tambwe anafunga bao safi kabisa kwa kichwa akiunganisha krosi nzuri ya Ngoma

Dk 47, Toto wanapoteza nafasi nzuri kabisa lakini Yondani anafanya kazi ya ziada kuokoa

Dk 46, Mpira unaanza, Yanga wakionekana kidogo kuanza kwa kasi lakini Toto pia wako makini kutibua kila mipango

MAPUMZIKO

-Kipa Mussa Mohammed anadaka mpira kwenye miguu ya Msuva aliyekuwa anajaribu kuuwahi
-Kidogo Yanga wanaonekana kuwa na papara na hofu kidogo

DAKIKA 2+ ZA NYONGEZA
Dk 42 hadi 44, Toto wanaonekana kuwa wajanja wakipoteza muda, huenda wanataka kwenda mapumziko wakiwa na bao hilo moja

Dk 40, kipa wa Toto yuko chini akidai ameumia, mwamuzi anaita waguzi

GOOOOOO Dk 39, William Kimanzi anakwenda kuandika bao la kwanza kwa Toto baada ya kuunganisha mpira wa kona uliochongwa na Kimanzi na kuandika bao kwa kichwa safi kabisa

Dk 37 kipa Dida wa Yanga anachochanya akiwa mwenyewe, anautoa mpira nje na kuwa kona

Dk 33, kipa Mussa Mohammed wa Toto anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa kichwa wa Tambwe. kaumia, yuko chini anatibiwa

Dk 30, Ngoma anamtoka beki mmoja wa Toto, anashangiliwa, anampa Niyonzima anapiga shuti kuuubwaaa, goal kick

Dk 29, Toto wanafanya mashala, nusura Ngoma aunase mpira lakini wanaokoa na kuwa kona, inachongwa na Msuva, ni kona dhaifu

Dk 27, kipa Toto shujaa tena, anaokoa mkwaju mkali wa krosi ya Msuva, Tambwe anaanguka baada ya kuukosa

Dk 23 hadi 25, Yanga ndiyo wanamiliki mpira zaidi, lakini bado mashambulizi ni mojamoja

Dk 22, Yanga wanapata kona nyingine, lakini kama zile za mwanzo, wanapiga na haina madhara hata kidogo kwa Toto...

Dk 20, Oscar Joshua anaachia shuti kali sana, lakini kipa Toto anaonyesha ubora na kupangua vizuri

Dk 19, Carlos Protus anafanya kazi ya ziada kuuwahi mpira ambao alipenyezewa Ngoma, anaotoa na kuwa kona. Inachongwa lakini haina madhara kwa Toto

Dk 14 hadi 18, mpira kidogo unachezwa zaidi katikati na hamu ya mashambulizi inapungua
inaonekana Dk 13, Ngoma na Msuva wanagongeana safi, Msuva anatoa pasi au krosi nzuri kabisa lakini Ngoma anaukosa mpira...

Dk 10, nafasi nzuri zaidi hadi sasa anaipata Waziri Junior akiwa peke yake, anaruka juu na kupiga mpira juuu ya lango la Toto

Dk 7, Msuva ainaingia na kupiga kona safi kabisa, lakini hakuna mtu, Toto wanaokoa, kona. Inachongwa vizuri lakini haina faida kwa Yanga

Dk 6, Niyonzima anapiga pasi nzuri kabisa katikati ya lango la Toto, mabeki Toto wanajichanganya wakidhani offside lakini hakuna mtu pale

Dk 3, Waziri Junior nusura autumbukize mpira wavuni lakini Yondani anaondosha

Dk 1 tu, Toto wanapata kona, anaichonga Seseme, inaokolewa na kuwa mpira wa kurushwa. Yanga wanaondoa sehemu ya lango lao

Mechi imeanza hapa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Toto African wakiwa wenyeji dhidi ya Yanga wanaowania ubingwa.

*****************************
FULL TIME: Toto Africa 1 - 2 Yanga
 
Full Time : Toto Africa 1 - 2 Yanga Africa

William Kimanzi 39' Mins (Toto Africa)
Amisi Tambwe 50' Mins ( Yanga Africa)
Juma Abdul 77' Mins (Yanga Africa)
 
Hatimaye tumelitekenya Toto Letu. Tunasubiri kesho tuone mashost mtu na dada yake wakikatiana shanga taifa.
 
Huhuuuuuuu
Hiyo ndio Yanga bwana.....
Rrraaaaaaaah tu.
Ila atakayesema Toto katulegezea atakuwa mnafiki aliyetukuka...jamaa wamekaza kinoma.
Nilikuwa sina amani dakika zote 90!
 
Huhuuuuuuu
Hiyo ndio Yanga bwana.....
Rrraaaaaaaah tu.
Ila atakayesema Toto katulegezea atakuwa mnafiki aliyetukuka...jamaa wamekaza kinoma.
Nilikuwa sina amani dakika zote 90!
Lengo ni kubeba vikombe vikombe vyote
 
Huhuuuuuuu
Hiyo ndio Yanga bwana.....
Rrraaaaaaaah tu.
Ila atakayesema Toto katulegezea atakuwa mnafiki aliyetukuka...jamaa wamekaza kinoma.
Nilikuwa sina amani dakika zote 90!
Mtani ndio mbinu za kisasa kiini macho. Staili moja kwa mechi zote, anafungwa moja kisha anasawazisha kisha anaongeza kuzuga watu.
 
Daaaaa mende alitaka kudondosha kabati, ikabidi ashughulikiwe kikamilifu
Kudadeki!
 
Huhuuuuuuu
Hiyo ndio Yanga bwana.....
Rrraaaaaaaah tu.
Ila atakayesema Toto katulegezea atakuwa mnafiki aliyetukuka...jamaa wamekaza kinoma.
Nilikuwa sina amani dakika zote 90!
Subiri watakuja kusema Yanga imebebwa. Wanasahau Yanga inajibeba yenyewe!
 
Coastal naye kapigwa na African Sports pungufu. Tunasubiri waseme refa kawaua!
 
Huhuuuuuuu
Hiyo ndio Yanga bwana.....
Rrraaaaaaaah tu.
Ila atakayesema Toto katulegezea atakuwa mnafiki aliyetukuka...jamaa wamekaza kinoma.
Nilikuwa sina amani dakika zote 90!

Siku hizi wala hampati shida wenyewe, mnajinunulia tu mechi na marefa mchezo umekwisha. Yanga bwana.

Ova
 
Back
Top Bottom