Man U kuraruana na Arsenal | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Man U kuraruana na Arsenal

Discussion in 'Sports' started by Bikra, May 16, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  May 16, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Manchester United wanatazamia kutangazwa mabingwa wa ligi msimu wa 2008-09, ikiwa wataepuka kushindwa na Arsenal Jumamosi hii.
  Man U itakuwa ni klabu ya kwanza kupata 'hat-trick' mara mbili, yaani ushindi katika misimu mitatu mfululizo.

  Man U kwa mara ya kwanza iliweza kutimiza ushindi wa aina hiyo katika miaka ya 1999, 2000 na 2001.

  Kama itafanikiwa kutangazwa bingwa msimu huu, basi itapata 'hat-trick' kutokana na ushindi wa mwaka 2007, 2008 na 2009.

  Huu itakuwa ni ufanisi muhimu pia kwa meneja Sir Alex Ferguson, kwani atakuwa anaandikisha ushindi wa ligi kuu ya England kwa mara ya 11.

  Sir Ferguson, kutoka Uskochi, na mwenye umri wa miaka 67, ndiye meneja mwenye sifa zaidi hapa Uingereza, kwa kunyakua vikombe 31, pasipo kuhesabu ubingwa wa dunia wa Kombe la Vilabu.

  Atakuwa ameandikisha rekodi mpya, ambayo awali ilishikiliwa na Bill Struth wa klabu ya Rangers ya Uskochi, ya vikombe 30, katika miaka ya 1920 hadi 1954, na Willie Maley, akiongoza Celtic, pia ya Uskochi, miaka ya 1897 hadi 1940.

  Hii itakuwa ni mara ya 40 kwa Sir Ferguson na Arsene Wenger, meneja wa Arsenal, kukutana.

  Meneja hawa wawili ndio waliohudumu kwa muda wa miaka mingi zaidi katika ligi kuu ya Premier.

  Man U na Arsenal walipokutana, United imefanikiwa kushinda mara 15, na Arsenal mara 14, chini ya uongozi wa Wenger.

  Mechi zao nane, kati ya kumi, walitoka sare, na mbili ziliamuliwa kwa mashuti ya penalti.

  United ilinyakua ushindi katika fainali ya Community Shield mwaka 2003, nayo Arsenal ikalichukua Kombe la FA mwaka 2005 kupitia penalti.
   
 2. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Sitegemei kuona mechi yenye msisimko leo. Hii mechi ni muhimu kwa Utd tu. Haina umuhimu sana kwa Arsenal (kujituma kwao itakuwa 50% - 50%).
   
 3. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,262
  Likes Received: 4,236
  Trophy Points: 280
  Fegie mpange TEVEZ aendelee kugawa dozi
   
 4. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mechi muhimu sana kwa Arsenal asikudanganye mtu; unafikiri wenye gunners wanafurahia kuwa kichwa cha mwendawazimu? Patience inapungua na Wenger aweza kupoteza kibarua hivi hivi, hivyo Arsenal watacheza kwa nguvu zote.
  Si hilo tu; Arsenal watataka kulipa kisasi, na watafurahi sana kuwaharibia Man United kutangazwa mabingwa kwao, tegemea mechi kali.

  Ila binafsi sina wasiwasi na Man United, najua Gunners wakijitahidi sana, wataishia draw.

  Hapa nishaandaa $50 ya kwenda kusherehekea ushindi! Karibu tushiriki.
   
 5. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #5
  May 16, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Weweeeeee??
   
Loading...