Hivi enzi za nyerere huyu mzee Mohd Said alikuwaga wapi? Imekuaje anaonekane vocal sana kipindi hiki kwenye mitandao inayopitiwa na vijana zaidi huku akiwaaminisha kwamba yeye ndo anayejua tulikotoka, tulipo, na tunapokwenda!! Kweli kama ana kipaji cha maono na akiwa ni mwanahistoria mzuri kama anavyojitanabaisha humu JF kwa data ambazo ninazidoubt ilikuwaje akaachwa nje ya uongozi wa mwalimu au hata mwinyi au hata mkapa!? asichaguliwe kuongoza wananchi wa japo eneo analoishi tu??
Humu mitandaoni ni vijana zaidi wamo... ni kwa nini asishiriki katika ligi za wazee wenzake kina warioba, Agustino Rama, Kingunge, Iddi Simba etc etc. ili tumuone ubavu wake akipambana na wazee wenzake kwenye jumuia za carriber yake? Humu amebaki kutema sumu na kupotosha vijana na kujenga chuki miongoni mwa wakristu na waislamu akijificha nyuma ya key-board bila kujali ni madhira gani yataipata nchi yetu usoni pindi mbegu anazopanda zitakapo komaa.
Hata huko nje anakoalikwa nna imani anatumika tu kama sample ya kufundishia wanafunzi waelewe ni jinsi gani binadamu anavyoweza badili historia ya kweli ikaonekana ni ubatili mtupu na akaingiza uongo unaompa advantage yeye na ukasupportiwa na vijidocument vya hapa na pale kisha akakomaa na huo uongo to the extent ya kupata wafuasi na waumini ambao ni wavivu wa kuthibitisha mambo na kufanya utafiti.
Huyu mzee hata sura yake hajulikani barabara tofauti na mch. Mtikila ambaye anajulikana live! kaandika hii makala kwa uoga wa hali ya juu kwa kumuogopa Rev. Mtikila, hata heading yake tu ni polite na humo ndani hajamshambulia Rev. vibaya kama anavyomshambuliaga Baba wa taifa Mwl J. K. Nyerere... Hivi ni kwamba anaogopa Mziki wa Mtikila!!?? Au anamheshimu Mtikila zaidi ya Nyerere? Au anasubiria Mtikila akivuta ndo aanze kumshambulia kama anavyomshambulia Kipenzi chetu baba wa taifa Mwl J. K Nyerere!!?
Kwa nini ameandika hii makala kwa kizungu? Unafikiri Rev. Mtikila hajui kizungu?