Man City na Teknolojia ya Hali ya Juu

Man City na Teknolojia ya Hali ya Juu

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Kikosi cha Man City[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Miaka kadhaa iliyolipa umaarufu wa timu hii ulikuwa “noisy neighbours” kwa maana ya kwamba wana kelele dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester United lakini hawana uwezo wa kushinda makombe, hiyo ni Manchester City ya zamani. Man City ya leo ikimilikiwa na tajiri wa petroli Sheikh Mansour Bin Zayed Al Nahyan wa ukoo wa ufalme wa Abu Dhabi ni moja kati ya klabu tajiri Ulimwenguni. Fedha za Man City zinaonekana katika seahemu mbali mbali, ampabo klabu hii ni moja kati ya klabu zinazolipa mishahara mikubwa na kununua wachezaji ghali mno. Pia klabu hiyo hivi karibuni imepitisha mpango wa kuupanua uwanja wa Etihad kufikia kuwa na uwezo wa kuchukua washabiki 62,000 kwa msimu wa 2015-16, hii itaufanya Man City kuupiku uwanja wa Emirates na kuchukua nafasi ya pili kwa ukubwa nyuma ya wapinzani wao Man United.

[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Chumba cha wachezaji[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Kwa upande wa teknolojia Man City sasa hivi ni klabu inayoongoza ulimwenguni, tutayataja baadhi ya mambo yanayoifanya klabu hiyo kuwa na nafasi hii. Jambo la kwanza ni WiFi. Mwaka jana Man City wamefuata nyayo uwanja wa Anfield wa Liverpool, Bernabéu wa Real Madrid na Nou Camp wa Barcelona za kuweka WiFi ya kasi uwanjani, kasi ya WiFi ya Etihad imevunja rekodi kwa kuwa na uwezo wa mpaka 72Mpbs, tofauti na za Liverpool, na viwanja vingine ambazo zimeripotiwa kuwa na matatizo watumiaji wengi wanapotumia sambamba. WiFI hii inawaruhusu wale wenye app zinazoonyesha kandanda moja kwa moja kama vile SkySports App iliyoko kwenye gajeti za iOS na Android kuweza kuona marudio ya sehemu muhimu za mchezo kama vile magoli, penalti, kadi nyekundu moja kwa moja.

​
Etihad pia imewekewa teknolojia ya ghali zaidi ya mstari wa goli, teknolojia hiyo ni Hawk Eye Spy Cam hugharimu £250,000.00 (Tsh. 686,500,170.00) na huweza kumuarifu refa mpira unavuka mstari wa chaki ya goli, hivyo kuondoa utata iwapo refa na wasaidizi wake hawana uhakika wa hili. Goli la 100 la msimu huu lililofungwa na mshambuliaji Edin Dzeko lilitolewa kwa taarifa ya Hawk Eye Spy Cam kwa vile refa na wasaidizi wake hawakuona kama mpira ulivuja chaki. Hawk Eye Spy Cam inatumika na klabu zote za ligi kuu ya Uingereza kwa sasa. Mbali na teknolojia hii Meneja wa Man City Manuel Pellegriny anatumia software ya hali ya juu aina ya Prozone Analysis tool kufanya uchambuzi wa utendaji (performance) wa wachezaji wake mazoezini na kwenye mechi za Etihad, si ajabu wanapokuwa Etihad Man City huwa hawashikiki.

Vile vile Man City imewekeza pound milioni mia moja (Shilingi trilioni mbili nukta saba nne) kujenga akademi ya kisasa ya mazoezi ambayo itakuwa na jumla y a viwanja 16, akademi hiyo inatarajiwa kuwa tayari mwanzoni mwa msimu ujao. Man City pia wataanza kuvaa fulana maalum mazoezini ambazo zitakuwa zinatoa taarifa za msukumo wa damu, mapigo ya moyo, maji anayopotezwa mwilini na kiwango cha CO2 anachotoa mchezaji. Sambamba na fulana hizo Viatu vya wachezaji wa Man City vitakuwa vinatoa taarifa kama vile mshindo wa mpira (impact) mchezaji anapoupiga, idadi ya hatua anazokimbia mchezaji kwa kila mechi au mazoezi na taaarifa zote za kipedometa, kocha ataweza kung’amua kwa urahisi ni nani ana juhudi ziada au anategea.

Teknolojia nyingine ambayo tayari iko njiani ni Sisco System StadiumVision ambayo inatumiwa na timu ya mpira wa kikabu ya Brooklyn Nets ya Marekani. Hii itaruhusu watazamaji kuona marudio muhimu sehemu za mechi katika pembe mbali mbali kwa kutumia gajeti zenye WiFi, hivyo kuona video ya mechi hakutategemea tena kulipia app ya Sky Sports na app nyingine kama hizo.Hudumua hii itakuwa ni ya kulipia.

​
Kwa upande wa apps City haiko nyuma, app ya Manchester City Connect tayari inaruhusu washabiki kucheza (game) mechi inayokaribia kuanza uwanjani kwa kujumuika kwa vikundi, mbali na kutoa taarifa na video za kawaida zinazotegemewa kupatikana katika app ya timu. App nyingine muhimu kwa wadau wa timu hii City App ambayo ina habari nyingi mbali mbali za klabu hiyo pia na City TV. App hizi tayari zinanufaika na mkataba kati ya Man City na kampuni ya iON ulitiwa saini Februari mwaka huu ambapo iON hutumia kamera za kisasa pamoja na software ya Air Pro 3. teknolojia hii sio tu itakuwa inachukua video pia itaruhusu wadau mbali mbali wa Man city kupakia video zao wakiwemo wachezaji na washabiki watimu hiyo.

Wakati kuna fununu kwamba Barcelona huenda ikamuuza Lionel Messi mwisho wa msimu huu, Manchester City haitakuwa tu klabu ya kiteknolojia tu, kwani City ni moja kati ya klabu ambazo zinatajwa kujitayarisha ku-bid zaidi ya poundi milioni 100 kwa ajili ya kumnunua mchazaji huyo aliyeshinda FIFA Ballon D’or mara tatu mfululizo. Ballon D’or imeanzishwa miaka minne iliyopita ambapo Messi pia meshika nafasi ya pili mara ya mwisho. Je Messi atahamia klabu ya teknolojia mwakani? City App huenda ikawa ya kwanza kujibu swali hili.
Chanzo:gajetek habari
​

​
 
-kwa financial fair play city hawawez nunua mchezaj wa bei ghali wamevunja rekodi ya hasara umesahau kuitaja hii toka mmiliki ainunue wao wanavunja tu rekodi ya hasara na huenda mwisho wa msimu wakalazimika kuuza watu ili wanunue

-tech ya goli si ya mancity bali ni ya ligi ya uingereza. haiwezekani club ikahusika kwenye suala la maaamuzi mpira kuingia golini au kutoingia ni maamuzi ya marefa na chama cha fa. hivyo hawk eye ni ya epl na sio mancity.
 
Unahabari kuwa hawa jamaa walikuwa wanamtaka Messi kwa dau lolote lakini uongozi wa Nou Camp wakasema Messi hauzwi, na je waijua gharama halisi ya Messi iliyotolewa na wachambuzi wa fifa!?
 
Nashukuru kwa kumuokoa kijana kutoka kwenye biaseness
 
Unahabari kuwa hawa jamaa walikuwa wanamtaka Messi kwa dau lolote lakini uongozi wa Nou Camp wakasema Messi hauzwi, na je waijua gharama halisi ya Messi iliyotolewa na wachambuzi wa fifa!?
kaka kama financial fair play itatake place dirisha hili la manunuzi basi ili city wamnunue messi inabidi wauze sanaa tu.

kwa uingereza man u peke yake ndo amepata faida ya pound 140m ndio timu pekee inayoruhusiwa kufanya usajili wa kufuru. timu kama psg, man city,arsenal na chelsea zipo kwenye hatari kama zitafanya usajili mkubwa.

financial fair play (ffp) inasema hivi
Under this monitoring period, total losses of £37m (€45m) are permitted as long as clubs have owners who can cover such amounts.
For 2014-15, the monitoring period will be extended to cover the previous three seasons, but losses will still be limited to £37m (€45m).
For 2015-16, the monitoring period will again cover the previous three seasons, but the limit will drop to (£25m) €30m.
The pattern is repeated in 2016-17 and 2017-18.

so ukiangalia hapo utaona loss mwisho pound 37m

tuje kwa man city miaka hii miwili kala hasara pound 149m. kavunja rekodi ya hasara kupata kutokea epl, hivyo hata asponunua mchezaj yupo kwenye danger akimnunua mess ndo kabisaa hashirik uefa.

soma zaid hapa
BBC Sport - Manchester City await fate as Uefa's financial rules kick in
 
To Keep the facts right huu uwanja sio wa Manchester City bali ni wa Manchester City Council..

To ensure the long-term future of the stadium after the Commonwealth Games, it was agreed in 1998 that Manchester City F.C. would lease the stadium from Manchester City Council as a replacement for Maine Road. The conversion from a track and field arena to a football stadium cost the city council £22 million and Manchester City £20 million[SUP][/SUP] The club moved into its new home during the summer of 2003.
City of Manchester Stadium - Wikipedia, the free encyclopedia
 
kaka kama financial fair play itatake place dirisha hili la manunuzi basi ili city wamnunue messi inabidi wauze sanaa tu.

kwa uingereza man u peke yake ndo amepata faida ya pound 140m ndio timu pekee inayoruhusiwa kufanya usajili wa kufuru. timu kama psg, man city,arsenal na chelsea zipo kwenye hatari kama zitafanya usajili mkubwa.

financial fair play (ffp) inasema hivi

so ukiangalia hapo utaona loss mwisho pound 37m

tuje kwa man city miaka hii miwili kala hasara pound 149m. kavunja rekodi ya hasara kupata kutokea epl, hivyo hata asponunua mchezaj yupo kwenye danger akimnunua mess ndo kabisaa hashirik uefa.

soma zaid hapa
BBC Sport - Manchester City await fate as Uefa's financial rules kick in

Umejikita zaidi kwenye uchumi wa timu, kumbuka Messi alipotakiwa etihad mmiliki ndo alikuwa anatoa hela yake mfukoni na sio ya club, unaambiwa ikiwa man city ingekuwa inategemea mapato yake kununua wachezaji ingekuwa imeshafilisika, na hata kesho barca wakisema tunamuweka Messi sokoni watu wa kwanza kumwaga dau watakuwa man city na psg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom