zuberi Abraham
JF-Expert Member
- Feb 13, 2016
- 480
- 389
Wana bodi
Katika taarifa ya habari ya saa 2:00 usiku wa tarehe 21/12/2016. Imeripotiwa habari ya kukamatwa kwa repota wa kujitegemea wa ITV na Redio one bwana Halfani Lihundi kwa kosa la uchochezi kwa kuripoti wananchi wa kata ya Leguruki kijiji cha Nkwasenga Arumeru kulalamika katika mkutano wao kuwa wanapata maji machafu baada ya mamlaka ya maji kufunga maji haya mara kwa mara.
Katika habari hiyo ya kukamatwa kwa Bw. Lihundi kwa maagizo ya mkuu wa wilaya ya Arumeru limeibua mjadala mzito. Ama tunaweza kusema hofu kubwa kwa public swali ni je habari aliyoitoa Mshitakiwa ni ya uchochezi kweli? Ama kuna nguvu kubwa nyuma ya pazia ya kutaka kuficha ukweli? wa malalamiko ya wananchi hao walipopaza sauti zao katika kikao hicho. Habari hiyo anayoshitakiwa Bw. Lihundi kua ni ya kichochezi ITV pia waliiripoti na public imejionea malalamiko hayo ya wananchi wa kata ya Leguruki. Sasa swali linalotuumiza kichwa sisi watazamaji na watanzania wazalendo ni je kusema ukweli ni kosa la kichochezi? Je mwandishi kuripoti habari ya mkutano na malalamiko ya wananchi ni uchochezi?
Tungependa kuona hatua stahiki zikichukuliwa kwa sakata hili pia kama si kosa la mwandishi huyu hodari basi tunahitaji kuona viongozi wa hili swala wakiwajibishwa kwa maana tunaona taratibu za kazi kukiukwa. Vile vile Mamlaka kama ni kweli wanafunga maji mara kwa mara basi tujue sababu na DC inabidi aangaliwe kwa jicho la karibu hatutaki kuamini anahusika na hili maana serikali ya awamu ya tano inatenda kazi nzuri na mapungufu ni machache na yanafanyiwa marekebisho hapo hapo.
Nalilet kwenu kwa kuwaomba Moderator wanisaidie kuwa tag wahusika na jamii kiujumla