Mamlaka za juu: Tamisemi, Mkuu wa mkoa tunaomba uangalizi haki sakata la Lihundi

zuberi Abraham

JF-Expert Member
Feb 13, 2016
480
389
Wana bodi

Katika taarifa ya habari ya saa 2:00 usiku wa tarehe 21/12/2016. Imeripotiwa habari ya kukamatwa kwa repota wa kujitegemea wa ITV na Redio one bwana Halfani Lihundi kwa kosa la uchochezi kwa kuripoti wananchi wa kata ya Leguruki kijiji cha Nkwasenga Arumeru kulalamika katika mkutano wao kuwa wanapata maji machafu baada ya mamlaka ya maji kufunga maji haya mara kwa mara.

Katika habari hiyo ya kukamatwa kwa Bw. Lihundi kwa maagizo ya mkuu wa wilaya ya Arumeru limeibua mjadala mzito. Ama tunaweza kusema hofu kubwa kwa public swali ni je habari aliyoitoa Mshitakiwa ni ya uchochezi kweli? Ama kuna nguvu kubwa nyuma ya pazia ya kutaka kuficha ukweli? wa malalamiko ya wananchi hao walipopaza sauti zao katika kikao hicho. Habari hiyo anayoshitakiwa Bw. Lihundi kua ni ya kichochezi ITV pia waliiripoti na public imejionea malalamiko hayo ya wananchi wa kata ya Leguruki. Sasa swali linalotuumiza kichwa sisi watazamaji na watanzania wazalendo ni je kusema ukweli ni kosa la kichochezi? Je mwandishi kuripoti habari ya mkutano na malalamiko ya wananchi ni uchochezi?

Tungependa kuona hatua stahiki zikichukuliwa kwa sakata hili pia kama si kosa la mwandishi huyu hodari basi tunahitaji kuona viongozi wa hili swala wakiwajibishwa kwa maana tunaona taratibu za kazi kukiukwa. Vile vile Mamlaka kama ni kweli wanafunga maji mara kwa mara basi tujue sababu na DC inabidi aangaliwe kwa jicho la karibu hatutaki kuamini anahusika na hili maana serikali ya awamu ya tano inatenda kazi nzuri na mapungufu ni machache na yanafanyiwa marekebisho hapo hapo.

Nalilet kwenu kwa kuwaomba Moderator wanisaidie kuwa tag wahusika na jamii kiujumla
 
Acha kutetea ujinga sema kitu direct serikali hii imeshindwa inaendeshwa kama gari bovu. Usiogope hawatakumax
 
Nimeisikiliza kwa makini ile habari ili angalau nigundue wapi ripota alipochochea mpaka DC kuiita habari ile ni ya uchochezi sijagundua!. Ni mtu mjinga tu ndiye atakayeamini kwamba ile ni taarifa ya uchochezi. Labda kama kuna jingine zaidi ya hilo!
 
Hawa ma DC hawa kuna haja kubwa kabisa mkuu wetu wa nchi awaangalie upya wanafanya mambo ambayo yapandikiza chuki wananchi dhidi ya serikali wwngine wana maamuzi ya kitoto sana ,nadhani wengi wao bado wana vitabia vya mitaani hawajua kuwa wanadhaman kubwa sana ambayo mh. Rais amewatunuku kwa kuwaamin lakin wao wanamuangusha mzee wetu hawa,siungi mkono mambo mengi ya hawa wakuu wa wilaya bora hata wa mikoa naona kidogo wana uafadhali
 
Mbona haisemwi habari waliyoiunganisha ITV mara baada ya ile habari ya Lihundi? Waziri mkuu si ameonekana akisema kuwa ni aibu kwa mkuu wa wilaya raia wako kuandamana kwa mabango anapokuja mgeni?? That means mkuu wa wilaya ametumia pia kauli hiyo kuhalalisha alichokifanya, all in all uandishi wa habari, wanahabari na wadau wote wa habari hatuko salama awamu hiu!
 
Huyu DC ni kama yahaya jammeh anakubali matokeo baada ya wiki anabadilika, tukio la November 16 anamkamata leo, hapo DC hajui mchochezi, mchochezi ni huyo aliyemshauri amkamate lihundi mwezi moja baada ya tukio, inabidi nape awape semina hawa ma DC make ni kama hawajui maana ya neno uchochezi, wakiamka na hungover ya gongo wanakuja na vituko vya ajabuajabu.
 
Nimeisikiliza kwa makini ile habari ili angalau nigundue wapi ripota alipochochea mpaka DC kuiita habari ile ni ya uchochezi sijagundua!. Ni mtu mjinga tu ndiye atakayeamini kwamba ile ni taarifa ya uchochezi. Labda kama kuna jingine zaidi ya hilo!
Siwezi kusema lolote kwa sasa hivi kwa sababu zifuatazo:
a. Habari hiyo ni upande mmoja tu ni upande mtuhumiwa tu ndiyo uliyowasilisha tukio, kuna uwezekano kuna kipande cha taarifa kimefichwa ambacho ndicho kilichopelekea kukamatwa kwa mwandishi .
b. Siku hizi kuna upotoshaji mkubwa sana kuhusu utendaji wa serikali. Mfano swala la Lema ukilifuatilia jinsi linavyoripotiwa unaweza kudhani kuwa Lema anaonewa. Mana kuna watu wanaaminishwa kuwa Lema antuhumiwa kwa ndoto aliyoota. Ukweli ni kwamba Lema anashtakiwa kwa makosa ya kuchochea vurugu na kumtusi mkuu wa mkoa kwa kumtumia meseji ya kumtusi mambo ambayo waandishi na mashabiki wa Lema hawayaweki wazi.
 
asiyesikia la mkuu , nyie waandishi wa habari ndio mliochangia kwa kiasi kikubwa kuwapotosha wananchi mwaka jana, haya mnayo yapata ni mshahara wenu. Acha awashughurikie , nadhani 2020 labda mtakuwa na akili
 
Huyu DC anaweza kuwa na nguvu kubwa maana hata RC Gambo alishafika Leguruki na kumaliza huu mgogoro sasa sijui imekuaje tena haya yakatokea ila tangia mwanzo ni kama DC ndiye alichangia mgogoro huu kukua.
Anyway viongozi wanapaswa kuelewa cheo ni dhamana tu na inaweza kuondolewa anytime
 
Haya ndio matokeo ya kuchagua makada kuwa ma DC hawajui lolote mtu hajawahi hata kuwa monita wa darasa anateuliwa kuwa DC.
Taarifa ya Lihundi nilitegemea iwe chanzo cha yeye kufanya kazi na kutatua tatizo la maji yeye anamuweka ndani huyo DC kilaza sijui aliokotwa wapi.
 
Back
Top Bottom