Mamlaka ya mkuu wa mkoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mamlaka ya mkuu wa mkoa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanantala, Apr 2, 2012.

 1. M

  Mwanantala Senior Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Heshima kwenu wakuu! Nipo Bukoba. Kero yangu ni juu ya mamlaka ya mkuu wa mkoa wa Kagera ndugu Fabian Masawe kulazimisha wananchi kupaka rangi kuta na paa za nyumba zao kwa amri bila kujali uwezo wao. Mbaya zaidi ameagiza bwana afya wa mkoa kukata migomba yetu na imetekelezwa. Naomba mwongozo wenu wa kisheria ili niondoe udhalilishaji huu.
   
 2. JAPUONY

  JAPUONY JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Najua wadau wasiojua taratibu za kiserikali watakurupuka hapa kwa matusi. Lakini, chamsingi Mkuu wa Mkoa ni msimamizi wa shughuli zote za Serikali ndani ya Mkoa na Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa Raia ndani ya Mkoa. Kwahiyo kama migomba iliyokatwa ilikuwa ina something to do with Afya ya raia wengine au wewe mwenyewe yeye kama msimamizi wa usalama wako anaouwezo wa kufanya hivyo kuhakikisha aidha wewe au wengine wanakuwa salama.Pili, kuhusu kupaka nyumba rangi sijaelewa vizuri manake hujaeleza sababu za kusisitiza upakaji wa rangi ulikuwa ni nini hasa.Eleza sababu zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa halafu tukupe majibu hapa hapa.

  Thanks.
   
 3. M

  Mwanantala Senior Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asante kwa ufafanuzi. Migomba haikuwa na athari yoyote kwa jamii. Yeye hataki kuona migomba mjini. Kuhusu rangi anadai nyumba za mjini lazima zipakwe rangi nyeupe au anazopendekeza yeye. Bati ipigwe rangi nyekundu. Uwezo wa kutimiza hayo yote sina. Je, amri hii ni halali kwa mujibu wa sheria za nchi?
   
Loading...