Ikimura
Member
- Apr 1, 2011
- 22
- 2
Kwa ukweli mimi kama Raia wa kawaida sijui hasa ni zipi kazi za mamlaka hii hasa linapo kuja swala la television, tulitangaziwa kwamba Tanzania kama nchi nyingine duniani kote, inaondoka kwenye mfumo wa analogia na kujiunga na mfumo wa digitali...sawa si vibaya...Ila sasa mbona hamtuambii chochote kuhusu baadhi ya Tv stations kupunguza signal zao na mbona huwa taarifa hazitolewi kwa watumiaji??? Nikiongelea kupunguza signal na husisha wale watu wanaopata masafa ya tv kupitia mifumo ya satellite Dishes...Mnatuambia kuwa kufikia mwaka huu mwishoni vituo vyote vitakuwa vimesha hama kutoka kwenye analogia na kuingia kwenye digitali na hapo sasa kila mwananchi anatakiwa awe na kin'gamuzi..
Hivi ninyi mnaosema kuwa kila mtu anunue kin'gamuzi mmefanya uchambuzi yakinifu vizuri au ndio yale mambo ya 10% na kuanza kushabikia kila kitu hata kama kinawaumiza wengine...Najua wengi wenu mnao shabikia hili uwezo wakulipia Dstv mnao sasa ni vipi kwa wale ambao hata bill za umeme, maji na pango bado zinawashinda, tena unamletea bill ya tv ni kweli ataweza kulipia???
Na mbona kuna tv nyingi tuu ambazo ziko kwenye mfumo wa digital na bado zinaonekana kwenye madish bure na bila kulipia??? mfano Aljezeera, Kbc na nyinginezo???
Na mbona kama nilivyo ianisha hapo juu hamseme kupungua kwa signal kwa hizi tv za ndani, mfano ilianza tbc mwaka jana, afu ikawa stable baadae, ikaja channel ten hadi leo haijarudi, ikafuatiwa na Star tv ila imekwisha rudi, hivi sasa tv za mengi (IPP) hazionekani...Tuambiani tatizo ni nini???