Mamlaka ya mawasiliano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mamlaka ya mawasiliano

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ikimura, Jan 3, 2012.

 1. Ikimura

  Ikimura Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa ukweli mimi kama Raia wa kawaida sijui hasa ni zipi kazi za mamlaka hii hasa linapo kuja swala la television, tulitangaziwa kwamba Tanzania kama nchi nyingine duniani kote, inaondoka kwenye mfumo wa analogia na kujiunga na mfumo wa digitali...sawa si vibaya...Ila sasa mbona hamtuambii chochote kuhusu baadhi ya Tv stations kupunguza signal zao na mbona huwa taarifa hazitolewi kwa watumiaji??? Nikiongelea kupunguza signal na husisha wale watu wanaopata masafa ya tv kupitia mifumo ya satellite Dishes...Mnatuambia kuwa kufikia mwaka huu mwishoni vituo vyote vitakuwa vimesha hama kutoka kwenye analogia na kuingia kwenye digitali na hapo sasa kila mwananchi anatakiwa awe na kin'gamuzi..

  Hivi ninyi mnaosema kuwa kila mtu anunue kin'gamuzi mmefanya uchambuzi yakinifu vizuri au ndio yale mambo ya 10% na kuanza kushabikia kila kitu hata kama kinawaumiza wengine...Najua wengi wenu mnao shabikia hili uwezo wakulipia Dstv mnao sasa ni vipi kwa wale ambao hata bill za umeme, maji na pango bado zinawashinda, tena unamletea bill ya tv ni kweli ataweza kulipia???

  Na mbona kuna tv nyingi tuu ambazo ziko kwenye mfumo wa digital na bado zinaonekana kwenye madish bure na bila kulipia??? mfano Aljezeera, Kbc na nyinginezo???

  Na mbona kama nilivyo ianisha hapo juu hamseme kupungua kwa signal kwa hizi tv za ndani, mfano ilianza tbc mwaka jana, afu ikawa stable baadae, ikaja channel ten hadi leo haijarudi, ikafuatiwa na Star tv ila imekwisha rudi, hivi sasa tv za mengi (IPP) hazionekani...Tuambiani tatizo ni nini???
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  globalization na kukua kwa technology
   
 3. Ikimura

  Ikimura Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sijakuelewa Mkuu
   
 4. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Sebuleni pangu nina ving'amuzi vi 3 mpaka sasa,StarTimes,Ting,Dstv na sasa nasikia kuna Zuki oops Zuku ,pia nasubiria cha Mengi na Diallo kwa hili hii ni kero(inabidi niongeze stuli za kuwekea hivyo vinavyong'amua) ,hivi kwanini tusitumie tu Smart card kwa king'amuzi chochote kama vile tunavyofanya kwenye simu?embu watu wa Tekohama mtuambia kama hilo linawezekana au haliwezekani na ni kwanini inawezekana au haiwezekani
   
 5. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  hapo kuna ishu ya content provider na service provider
  itakuwa vema kama akitokea mwekezaji wa cable atakaeunganisha masafa yote ya tv stations ndani na nje yaani achanganye dstv,easy,startimes na wengineo lakini hapo itahusisha TCRA kama national regulator kuratibu hilo. tatizo sasa ni garama kuweka miundombinu ya cable kwani itahitaji copper wires,booster mafundi nk na mwekezaji huyo inambidi aunganishe service tatu kwa wakati mmoja ndio aweze kupata faida kama tv signals, internet na simu,je TCRA wako tayari kuruhusu hili? kwani lazima atumie mitambo ya TTCL na hivo kutakuwa na ushindani mmkubwa baina yake na makampuni mengine kama tigo,airtell kwani nao wanatoa huduma hza internet pia na simu.hili litawezekana kama sheria za mawasiliano zikabadilishwa.
  kwa nchi kama yetu bado tutaendelea kuteseka hivo hivo na service provider wengi huku huduma zao zikiwa mbovu
  kwa wenye madishi endeleeni kuyatumia kwani receiver zao ni nzuri kuliko content za service provider wa ndani labda dstv kidogo wanajitahidi kwa vile lazima utumie dish zao na sio antena. ndugu yangu kuliko kuwa na vingamuzi vingi nashani dstv ukiwa nao na labda chagua service provider mmoja mwenye channel za nyumbani kama easy sijui wengine.
  nimewapa darasa kidogo la electronic communication

   
 6. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2012
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu Lokisaa kwa tanzania yetu hii ni wangapi wataweza kumudu gharama hizo???
   
 7. S

  Samkyjr JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ving'amuzi vinasumbua sana, mbeya startimes inasumbua sana kupita kiasi na ni mjini sijui kwa watu wa vijijini tulishasahau mambo ya kupanda kwenye mabati kurekebisha antena sasa naona yanarudi tena.
   
 8. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  kaka ndio maana nkasema ni tabu kwa tanzania kwani ni garama na pia sheria bado kufanyiwa marekebisho,suala la gharama nimezungumzia kumbe hujaona hii sentensi tatizo sasa ni garama kuweka miundombinu ya cable kwani itahitaji copper wires,booster mafundi nk.... simu ninazozungumzia sio mobile ni landline kwa hivo TTCL wanatakiwa kutoa access ktk miundombinu yao ILI mwekezaji huyo mpya aweze kutoa huduma ktk mikoa yote nchini.je itawezekana??hakuna ajuae wapo mabilionea ndani na nje huenda akajitokeza mmoja.
  .
   
 9. b

  buswe Member

  #9
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mimi Tcra wananiudhi kwa kushindwa kudhibiti kampuni za simu zinazowaibia wananchi muda wa maongezi.
   
Loading...