Mamlaka ya hali ya hewa WHY? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mamlaka ya hali ya hewa WHY?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kurzweil, Jul 19, 2012.

 1. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,902
  Likes Received: 4,759
  Trophy Points: 280
  Mara kwa mara nimekua nikiona makala maalum kuhusiana na Tsunami ya Japan tena ufafanuzi ukitolewa na mkurugenzi mkuu mwenyewe Dr Agness Kijazi, kupitia kituo cha TBCCM. Lakini mamlaka hii imekua ikishindwa kutoa utabiri sahihi kuhusu hali ya hewa hapa nchini sasa kwanini wanatumia nguvu nyingi kwa Tsunami ya Japan kuliko kujiimarisha wenyewe? Naomba muongozo kama hili swala tulijadiri au liko mahakamani. . . . .
   
 2. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Hili suala bado halijapelekwa mahakamani hivyo tunaweza kulijadili lakini Serikali na LUKUVI wakiona mnawagusa katika masilahi wataamua kulipeleka mahakamani ili kufunga watu midomo.

  Mimi binafsi nilikuwa najiuliza jana baada ya zile taarifa kuhusu kuzama kkwa Meli "Hivi hali ya Hewa mamlaka wapo kutudanganya kwa yanayotokea Japan tu, mbona masuala ya Tanzania wanakuwa kimya na yakishatokea ndipo wanasema kulikuwa na Hali mbaya ya Hewa baharini!!!!!!"

  Jana siku nzima kulkuwa na pepo kali sana maeneo ya DSM hasa karibu na bahari lakini Bi. Agness Kijazi hakuuona ingawa ulikuwa unapiga hadi ofcn kwake. Ule uliotokea Japan aliuona mapema na kutoa tahadhari ya uongo kuwa utafika pwani ya Tanzania.

  Na hadi Home kwa mkuu wa kaya JK pale Magogoni bila shaka upepo mkali ulivuma na kurusha rusha majani na nguo walizoanika pale nje!!!!!!!!

  Je, kuna umuhimu gani wa kuwa na mamlaka ya hali ya hewa hapa Tanzania kama wanashindwa kufanya kazi ipasayo????


  Je, Bi. Agness Kijazi kweli ana uelewa na kazi wanayoifanya au wamepewa tu ofc pasipo kujua kusoma hali ya hewa???

  Je kwa hili kwa nini Bi. Agness Kijazi asijiuzulu kazi kwani ameshindwa kutimiza wajibu???

  Au ndio kulindana kunaendelea katika watendaji wa Serikali zetu.  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 3. D

  DCM Senior Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 165
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Huwa inasikisha sana kwani huwa taarifa zao nyingi huwa ni baada ya tukio kutokea!
   
Loading...