Mamlaka ya hali ya hewa kushirikiana na BAKITA kurahisisha taarifa za Hali ya Hewa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Dar es Salaam.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema imeanza mazungumzo na Baraza la Kiswahili Tanzania (Bakita) ili kutafuta tafsiri rahisi ya maneno ya kitaaluma yanayotumiwa kwenye utabiri wa hali ya hewa.

TMA imesema hilo litasaidia wananchi wengi kuelewa kwa haraka utabiri ambao mara kwa mara umehusisha maneno ya kisayansi yasiyo rahisi kuelewekewa na jamii yote.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi amesema hayo leo Agosti 30 wakati wa mjadala kuhusu utabiri wa mvua za msimu zinazotarajiwa kuanza Oktoba hadi Desemba.

Amesema TMA inaendelea kujizatiti kuwafikia wananchi wengi zaidi katika lugha nyepesi inayoeleweka kutokana na umuhimu wa taarifa hizo kwenye kuandaa mipango ya maendeleo na utekelezaji katika sekta mbalimbali zikiwemo za kilimo, ujenzi na miundombinu.

"Nafurahi kuwajulisha kwamba, tayari mamlaka imeshawasiliana na Bakita na wamekubali tuwasilishe maneno hayo ili yajadiliwe na kupatiwa tafsiri rahisi itakayoeleweka kwa watumiaji," amesema.

Amesema katika msimu wa mvua za masika Machi hadi Mei, maeneo mengi ya nchi yalipata mvua za chini ya wastani kama ilivyokuwa imeainishwa katika utabiri na hazikuwa na mtawanyiko mzuri.

Hata hivyo, amesema kwa maeneo ya ukanda wa Pwani, hasa Mkoa wa Tanga kulitokea vipindi vya mvua kubwa Aprili vilivyosababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi katika maeneo ya Lushoto, huku visiwa vya Unguja na Pemba vikipata mafuriko, vifo na uharibifu wa mali.



mwananchi
 
mpaka sasa tu misamiati mingi ya kiswahili hatutumii.
Kiswahili tunachotumia ni cha mazoea sasa wanataka kuongeza tena misamiati
 
Back
Top Bottom