Mamilioni yatumika kuwalipia mawaziri mahotelini................. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mamilioni yatumika kuwalipia mawaziri mahotelini.................

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 2, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Nipashe la leo linatutaaarifu ya kuwa mamilioni ya fedha yanaendelea kuteketezwa kuwalipia mawaziri ambao wapo mahotelini...................................

  Hili siyo jipya kwa JK kwani alipoingia madarakani mwaka 2005 kashfa hii ndiyo ilikuwa ya kwanza kuighubika serikali yake mbali ya ukweli aliunda serikali kubwa ambayo ni mzigo mkubwa kwa walipa kodi...........................

  JK na serikali yake ilijibu ya kuwa walikuwa wanajenga nyumba kwa kila waziri nyumba ambazo zilikadiriwa kuligharimu Taifa Tshs 85 Milioni kwa kila nyumba..................Kisichoeleweka ni kwa sababu zipi mawaziri hao hawahamii kwenye nyumba hizo za serikali au ukubwa wa baraza la mawaziri una sababisha ziwe nyumba haba?
   
 2. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,576
  Likes Received: 1,664
  Trophy Points: 280
  Kwani akbla ya kuwa MAWAZIRI walikuwa wanakaa wapi? Wengi wao si waliuziwa zile nyumba zetu za Masaki na Oysterbay?
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  huu wimbo 2meuchoka,namna hii hayo matumiz ya serikali yataisha?mmoja najua analala newafrika
   
 4. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Ulimbukeni tu kuwa waziri ndo ulale nu africa yaani viongozi wa Bongo kazi kweli! Lakini sishangai siku 1 nikiwa dodoma wazri 1 asb aliitisha soseji 12 kwa ulimbuke matokeo yake aliishia kula 4 tu so nane zote zikawa ni waste!! ULIMBUKENI TU NDO UNAZINGUA!
   
 5. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna haja ya kufanya hesabu ya fedha yote ambayo serikali imekwishalipa kama gharama ya kuwaweka watumishi wake hotelini, tangu ichukuliwe hii hatua ya wendawazimu na bill hiyo apelekewe Mkapa. Naambiwa katika kipindi chote cha uspika wake Sitta alikuwa anaishi kwenye nyumba ya kupanga ambayo ilikuwa inalipiwa na serikali dola 7,ooo kwa mwezt. Sijui kama huyu aliopo bado anaendeleza mtindo ule ule?
   
 6. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye nyekundu ni kwamba Nyumaba aliokua anakaa ilikua inalipiwa dola 10,000 (elfu kumi) kwa mwezi...!

  Pia wanaoishi mahotelini sio mawaziri tu, kuna majaji pia...! Majaji wengi kwa sasa wanaishi mahotelini kwa sababu serikali haijawapa nyumba...! Nenda pale court yard utakutana nao wengi tu...!
   
 7. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,465
  Likes Received: 1,413
  Trophy Points: 280
  JK hana mapenzi mema na hii nchi, nashangaa hata wale waliorudi kwenye serikali yake nao wapo haotelini
   
Loading...