Mamia ya wanachama wa CUF Mtwara wahamia NCCR

Hawa nao! Wanatoka CCM B na kuhamia CCM C, bado wako mmo kwa mmo!!!.
 
tuliambiwa hawa ni mizigo kwa chama uwepo wao wao unasababisha chama kishindwe kusonga mbele

huu mwaka tutaona na kusikia mengi hadi uishe ,,,,,,,,,,,,sijui
 
Yesu alisema acha wafu wazikane. Nccr na cuf wote ni wafu tuuu. Nccr ilikuwa mkoa mmoja tu wa kigoma sasa tangu katibu mkuu ruhuza ashushwe jukwaani akihutubia kasulu mjini jimbo la mh machali mpaka leo mbatia hataki kwenda. Anaogopa yasimkute yaliyomfika katibu mkuu wake. Sasa huko mtwara kuna nccr ya mbatia kweli? Au masalia ya mrema? Kazi kwelikweli.
 
Bila shaka hao ma100 wanafikiri Lyatonga bado ni mwenyekiti wa nccr, wakikumbuka enzi za kufuma kwake.
Coz cuf iko icu, lakini nccr mageuzi, ina dalili tayari za mafua za hapa na pale na homa ya kila week so, kifo chake hakiko mbali pia. Wangetafakari vizuri baada ya kutoka cuf, waendee chama gani makini chenye dhamira ya kuleta ukombozi kwa mtanzania.
 
Yesu alisema acha wafu wazikane. Nccr na cuf wote ni wafu tuuu. Nccr ilikuwa mkoa mmoja tu wa kigoma sasa tangu katibu mkuu ruhuza ashushwe jukwaani akihutubia kasulu mjini jimbo la mh machali mpaka leo mbatia hataki kwenda. Anaogopa yasimkute yaliyomfika katibu mkuu wake. Sasa huko mtwara kuna nccr ya mbatia kweli? Au masalia ya mrema? Kazi kwelikweli.
Pole sana kwa kutumia jina la Yesu kuwaita wenzio wafu, angalau ungelinganisha avatar yako na kauli zako.
 
Warid huo ndio ukweli kuwa cuf inakufa lakini nccr ilikufa. Kama wanapigwa na kuzomewa na kushushwa jukwwani kwenye jimbo la mh machali wanapataje mamia huku mtwara ambako hawaongozi hata kitongoji? Mmekuja kufanya manunuzi kuliko hata sisiemu. Kweli hii nccr manunuzi. Sasa hao mliowanunua leo hawana mpango na chama chenu mmemdanganya nani? Wanaotaka kuhama cuf sereous wanasubiri ziara za cdm. Wajiunge na chama cha wanaume. Sio hizo nyumba ndogo za ccm.
 
Cuf hayo ndo madhara ya kushirikiana na wezi wa tz ccm ambao wakishawatumia wanawatupa kama toilet pepa poleni sana kwa kuwahi kufa kabla ya ccm ambayo mnaiacha inatapatapa basi wahini mkawashikie nafasi huko ahera
 
Warid huo ndio ukweli kuwa cuf inakufa lakini nccr ilikufa. Kama wanapigwa na kuzomewa na kushushwa jukwwani kwenye jimbo la mh machali wanapataje mamia huku mtwara ambako hawaongozi hata kitongoji? Mmekuja kufanya manunuzi kuliko hata sisiemu. Kweli hii nccr manunuzi. Sasa hao mliowanunua leo hawana mpango na chama chenu mmemdanganya nani? Wanaotaka kuhama cuf sereous wanasubiri ziara za cdm. Wajiunge na chama cha wanaume. Sio hizo nyumba ndogo za ccm.
Kuondoka (kuondolewa) kwako NCCR ndio kunakufanya udai kwamba chama kimekufa, huna jingine
 
Kutoka gazeti la Mtanzania


MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amekibomoa Chama cha Wananchi (CUF) Mjini Mtwara, baada ya kuzoa wafuasi zaidi ya 463 wa chama hicho.
Miongoni mwa walioihama CUF, ni aliyekuwa mgombea ubunge wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, Abdallah Uledi na Kiongozi wa Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Mtwara, Mussa Abdallah.

Kutokana na wingi wa wafuasi hao, Mbatia, ambaye alikuwa na jukumu la kupokea kadi za CUF na kuwagawia wanachama wapya kadi za NCCR- Mageuzi, alizidiwa uwezo na badala yake kukaimisha jukumu hilo kwa wasaidizi wake, wakiwamo Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali na Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar, Mussa Kombo Mussa.

Hata hivyo, zoezi la kugawa kadi hizo halikumalizika kutokana na wingi wa wananchi na pia Mbatia alikuwa akiwahi kwenda kufungua tawi jipya eneo la Majengo, Ilala, mjini Mtwara kabla giza halijaingia.

Tukio hilo, lilitokea jana wakati Mbatia alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Vigaeni, vilivyoko eneo la Chikongola, Mjini Mtwara.

Mbatia, mshauri wake mkuu, Danda Juju, Machali, Kombo, pamoja na viongozi wengine wa ngazi za juu wa chama hicho, wako katika ziara ya kukijenga chama mkoani Mtwara.

Wakati wa kuwapokea wanachama hao, Uledi alionekana kuwa kivutio kikubwa kwa kuwa wakati alipokuwa akieleza sababu za kuhamia NCCR-Mageuzi, mamia ya wananchi waliokuwa katika mkutano huo, walikuwa wakilipuka kwa shangwe na vigelegele wakionyesha kuungana naye. Uledi ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnain Murji (CCM), wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

Akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano huo, Mbatia alisema Watanzania, wakiwamo wakazi wa Mtwara, wanaishi maisha magumu kutokana na tabia yao ya kutotaka mageuzi ya kisiasa.

"Mtwara mna utajiri wa kutosha, nyie mna gesi lakini gesi haiwanufaishi, badala yake sasa inapelekwa Dar es Salaam, nyie mnalima korosho na mna utajiri mwingi tu, lakini kwa sababu hamtaki mageuzi ya kisiasa mmekuwa mkiwachagua CCM kila uchaguzi unapofika. "Badilikeni kama kule Kigoma, walikuwa nyuma sana kimaendeleo, Kigoma hawakuwa na barabara na pia Mkoa wa Kigoma ulikuwa ni moja ya mikoa iliyokuwa nyuma kimaendeleo kwani hawakuwa hata na umeme.

"Lakini Kigoma walipokubali mageuzi, walipokubali kuwachagua wapinzani, sasa Kigoma wana barabara nzuri za lami na hivi sasa wanapelekewa umeme wa uhakika tofauti na nyinyi."

Mbatia alizungumzia zao la korosho na kusema anashangaa kuona korosho ya Tanzania inauzwa bei kubwa katika maduka ya kisasa jijini Dar es Salaam, wakati bei ya zao hilo kwa wakulima iko chini.

Kwa mujibu wa Mbatia, bei ya nusu kilo ya korosho katika baadhi ya maduka jijini Dar es Salaam ni Sh 10,500 na kwamba bei ya zao hilo nchini Uholanzi ni Sh 24,000 kwa kilo.

Kutokana na hali hiyo, alisema Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho, Anna Abdallah na Makamu wake, Mudhihiri Mudhihiri, hawawasaidii wakulima wa zao hilo, badala yake wanashika nafasi hizo kwa masilahi yao binafsi.
 
Kazi inaendelea Mtwara

Mtwara kuwa ngome ya NCCR-Mageuzi


na Mwandishi wetu


amka2.gif
CHAMA cha NCCR-Mageuzi, kinatarajia kuufanya Mkoa wa Mtwara kuwa ngome yao kisiasa.
Uamuzi huo ulielezwa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia, alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho katika mkutano wa ndani mjini hapa.
"CCM wamechoka, hawana sera mbadala, kwa hiyo, mikakati yetu tuliyonayo ni kuufanya Mkoa wa Mtwara kuwa ngome yetu kisiasa.
Alisema hili la kuufanya mkoa huu kuwa ngome yao halitakuwa la kwanza kwa sababu walifanya Kigoma na kufanikiwa kwani katika majimbo manane ya mkoa huo, wamenyakua manne, CHADEMA wanalo moja na CCM wanayo mawili.
Mbatia aliongeza kuwa hilo wakilidhamiria watafanikiwa kwa sababu CCM wamechoka, hivyo watapambana nao kwa sera, kila wakifanya hivi wanawajibu na mwisho watafanikiwa kama walivyoweza Kigoma.
"Kwa maana hiyo, nataka niseme tu kwamba, nguvu na mbinu tulizozitumia kule Kigoma ndizo hizo hizo tutakazozitumia kuuchukua mkoa huu," alisema Mbatia.
Katika mazungumzo yake, Mbatia aligusia umuhimu wa wanachama wa chama hicho katika kukijenga na kuwataka wawe mstari wa mbele wakati wote.
Kwa mujibu wa Mbatia, wanachama wa NCCR-Mageuzi wanatakiwa kuwa waaminifu, wawajibikaji, kuheshimiana na kuwa makini katika kujali muda.
"Chama hakijengwi hivi hivi, lazima haya niliyoyasema muyajali na kuyafuata, pia mthaminiane na kuheshimiana wakati wote kwa sababu bila kuheshimiana na kuthaminiana hakuna kitakachofanyika.
Katika hatua nyingine, Mbatia alisema chama hicho kimejipanga kujiimarisha na kuwa na nguvu kama siku za mwanzo za kuanzishwa kwake na kwamba chini ya mikakati hiyo, kimeanza kununua ofisi na viwanja vya kujenga ofisi za kudumu katika maeneo mbalimbali nchini.


Chanzo: Tanzania Daima
 
Ukiangalia hii siasa ya tanzania inavyokenda haitabiriki huwezi kujua pamoja na kwamba nccr ni hakina wabunge wengi lakini ukiangalia katiba yao ipo vizuri sana na pia ukongwe unawasaidia sana huko mbele huenda kikawa chama pinzani kwa chadema tusubiri uchaguzi ujao ndipo tutajua siasa ya hapa bongo.
 
Back
Top Bottom