Akalee wajukuu tu maana atakuwa amechoka hataweza mikikimikiki ya mbeleni katika Uongozi. Miaka ijayo Wazee wengi wa sasa hawakuwepo, vijana ndio watakuwa wengi hawatavumilia mawazo ya kizamani katika Uongozi. Hivyo kuendelea na huu usanii wa kisiasa wa sasa itakuwa ngumu sana Mtu wa aina hiyo kuwaongoza vijana mbeleni. CCM hawawezi kufanya kosa hilo, watamshauri tu Mama Samia apumzike.Angela Merkel alistaafu na miaka mingapi? Halafu huu ni ubaguzi wa kijinsia usio wa kisayansi, yaani sisi wanaume tuna nini wenginec kina Paul Biya hata kumbukumbu zinacheza na bado wako Ikulu ila mwanamke miaka 70 tuone shida? Mungu akimjalia uhai 2025 ni Mhe. Rais Samia tena. 🙏🙏🙏