Mambo ya unyumba usiingilie

Chibidu

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
387
49
Wana jamii mimi leo nimeona niwapatie zawadi ya wikiendi wale walio katika unyumba.Japo zawadi yenyewe kiduchu lakini nafikiri itawafaa.
kuna tatizo katika jamii za wana ndoa au hata wale walio nje ya ndoa mara kwa mara watu kujaribu kufuatilia mambo ya ndani ya familia nyingine jirani wakati hayawahusu. Kwa mfano mtu anaweza kusikia mke na mume wanagombana nyumba ya pili, mtu huyo bila kuombwa utakuta tayari ameshasogelea ili apate habari ya kusimulia kwa wengine huku akijifanya anataka kusaidia kuleta mapatano kati ya wagombanao bila hata kuombwa. Tabia hiyo kwa kweli haipendezi katika jamii. Kitendo cha huyo mtu kuingilia ugomvi au mambo yasiyomuhusu, badala ya kuleta suruhisho mara nyingi huchochea matatizo.

Kwa mfano wiki hii kwenye mtaa mmoja kuna mama mmoja alisikia jirani zake (mke na mume) wanagombana ndani (tabia hii inaweza kuwa hata kwa mwanaume pia), akajifanya kwenda kuwaamulia. Akawa anawauliza "kwani vipi jamani, mbona hivyo?" Toba!! kusikia hivyo, yule mama aliyekuwa anagombana na mumewe akamgeuzia kibao huyu mama aliyejifanya kuja kusuruhisha. Akamwambia "tena wewe ndiye unayemtia jeuri mume wangu, unajifanya wewe mzuri sana. Unadhani mimi sijui kama unakula sahani moja na mume wangu.Leo umekuja kuthibitisha mwenyewe, utanitambua". Jamani mambo ya unyumba tusiingilie. Dunia haitaki papara. Mtakuja umbuka bure kwa mambo yasiyo wahusu.

Na zawadi yenu hii hapa kutoka kwa Maquiz original enzi hiiiiiiizoooooooo.[ame="http://www.youtube.com/watch?v=LI6hnf_PTMI&feature=quicklist"]bofya[/ame]. Sikiliza hawa jamaa walivyokuwa wanajua kufikisha ujumbe, sauti taaaaaaaaaaamu, gitaa la Nguza viking ndio usiseme, we acha tu. Wikiendi njema waungwana
 
Last edited:
Back
Top Bottom