Mambo ya ttcl internet

Mambo ya ttcl internet

mshihiri

Senior Member
Joined
Jul 15, 2011
Posts
138
Reaction score
89
KAMPUNI ya simu Nchini (TTCL) leo imezindua huduma mpya ya Bando na TTCL itakayomuwezesha mteja kufaidika na meseji bila kikomo ,kuperuzi intaneti na muda wa maongezi kwenda mitandao yote kwa bei nafuu.

DAR ES SALAAM, Tanzania

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kaimu Ofisa Mkuu wa Mauzo Peter Ngota alisema huduma ya bando na TTCL itamuwezesha mteja pia kutuma meseji bila kikomo kwa bei ya hadi shilingi mia tano.
Alisema bando TTCL inawalenga zaidi watumiaji wa simu za kisasa za smart phones za kampuni hiyo ambazo zinapatikana katika vituo vyao vya simu kote nchini.

Alisema kampuni hiyo imeshusha kwa kiwango kikubwa bei ya vifurushi vyake vya mobile internet kwa kampeni ya Basti ikimaanisha peruzi internet zaidi kwa gharama nafuu.

“Hii ni punguzo la bei la aina yake , mathalani kifurushi cha mwezi cha 4GB kilichokuwa kinauzwa shilingi 90,000 sasa kinauzwa shilingi 25,000 hii ni nafasi sit u kwa wateja waliopo TTCL kuongeza matumizi kwa gharama nafuu bali hata kwa wateja wapya ikiwamo watumiaji wadogo kujiunga na mtandao wa TTCL,”alisema Ngota.

Alisema Bando na TTCL na kampeni ya Basti zina manufaa kkwa mteja ikiwa ni pamoja na huduma ya mobile internate kwa gharama nafuu,vifurushi vya siku ,wiki na mwezi kulingana na mahitaji ya mteja,mobile internate yenye ubora na kasi ya juu zaidi,kwa kununua modemu ya shilingi 29,900 utapata 2GB bure kuperuzi intaneti.

Aidha alisema kua huduma ya bando na TTCL inapatikana pia kwa simu za kisasa za smart phones na inatoa thamani bora kwa pesa huku akieleza kua kama kampuni kongwe na mhimili wa mawasiliano nchini inatambua kuwa na jukumu kubwa la kutoa huduma za mawasiliano kwa wateja kote nchini.
 
MH!! Hv Jaman Hawa Jamaa wanatumia CdMa Ukiweka Line Zao kwenye Modem Tulizo Chakachua HUwa Znasomeka Kwelii??? Sjawah KujaribuHii Kitu
 
4gb kwa elfu 25000? Ttcl wajipange upya hapo! Kuna YATOSHA AIRTEL 3gb kwa 5999
 
4GB kwa Tsh25,000 bado hawajafanya Mapinduzi yoyote. Sana sana wanawaibia wateja wao waziwazi.

Airtel yatosha Unapata 12GB kwa Mwezi kwa TSh24,000 tu. Big Up Airtel kwa kuwajal wateja wenu japo ni mm ni mteja wa Tigo sijui wameniloga ndio ndio Maana nashindwa hata kuwahama.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Wamechelewa sana hawa makupe
 
Hawana jipya wakajipange upya. Nina limodem lao yaani hamna kitu very slow yaani hata udownload huwezi maliza mb 500 kwa mwezi nahisi speed ni kb 0.001 per sec siwapendi.
Internet nzuri ni voda.airtel.tigo na zantel hawa ttcl sijui shida ni nini.
 
Au kwa vile wameona mkongo unaleta shida kiasi kwamba hata ununue hizo bundle hutazimaliza kutokana na speed mbovu
 
za joni wakuu mchango wangu ni huu siku hizi net ambayo siyo unlimited downloading mimi kwangu aina maana hizi habari za kuperuzi sku nzima wapelekewe dda zetu zta wafaa mpango nikkushusha tu
 
KAMPUNI ya simu Nchini (TTCL) leo imezindua huduma mpya ya Bando na TTCL itakayomuwezesha mteja kufaidika na meseji bila kikomo ,kuperuzi intaneti na muda wa maongezi kwenda mitandao yote kwa bei nafuu.

DAR ES SALAAM, Tanzania

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kaimu Ofisa Mkuu wa Mauzo Peter Ngota alisema huduma ya bando na TTCL itamuwezesha mteja pia kutuma meseji bila kikomo kwa bei ya hadi shilingi mia tano.
Alisema bando TTCL inawalenga zaidi watumiaji wa simu za kisasa za smart phones za kampuni hiyo ambazo zinapatikana katika vituo vyao vya simu kote nchini.

Alisema kampuni hiyo imeshusha kwa kiwango kikubwa bei ya vifurushi vyake vya mobile internet kwa kampeni ya Basti ikimaanisha peruzi internet zaidi kwa gharama nafuu.

"Hii ni punguzo la bei la aina yake , mathalani kifurushi cha mwezi cha 4GB kilichokuwa kinauzwa shilingi 90,000 sasa kinauzwa shilingi 25,000 hii ni nafasi sit u kwa wateja waliopo TTCL kuongeza matumizi kwa gharama nafuu bali hata kwa wateja wapya ikiwamo watumiaji wadogo kujiunga na mtandao wa TTCL,"alisema Ngota.

Alisema Bando na TTCL na kampeni ya Basti zina manufaa kkwa mteja ikiwa ni pamoja na huduma ya mobile internate kwa gharama nafuu,vifurushi vya siku ,wiki na mwezi kulingana na mahitaji ya mteja,mobile internate yenye ubora na kasi ya juu zaidi,kwa kununua modemu ya shilingi 29,900 utapata 2GB bure kuperuzi intaneti.

Aidha alisema kua huduma ya bando na TTCL inapatikana pia kwa simu za kisasa za smart phones na inatoa thamani bora kwa pesa huku akieleza kua kama kampuni kongwe na mhimili wa mawasiliano nchini inatambua kuwa na jukumu kubwa la kutoa huduma za mawasiliano kwa wateja kote nchini.

Kama na wee ni mfanyakazi wa TTCL waambie wamepotea njia, kwenye mobile waachane nako waimarike kwenye broadband, wataingia chaka!
 
Kitambo ngota mpaka leo bado upo tuu?nilizani amehama TTCL
Sasa Airtel juzi nimetoa 45000tshs wakanipa8GB sijui ni offer
 
Walipotea sana walipo leta simu zao za kipekee wakagalagazwa mbaya
 
Hivi hao hata hawaangilii wenzao na bei zao?

Hio wanayoita nafuu ni nafuu ya wapi ?, Tanzania au ?
 
4gb kwa elfu 25000? Ttcl wajipange upya hapo! Kuna yatosha airtel 3gb kwa 5999

mbaya zaidi, wao ndo network provider, which means wanawauzia makampuni ya simu airtime. Cjui kwa nini wao wawe na bei kubwa hivyo!!!!
 
Hawana jipya wakajipange upya. Nina limodem lao yaani hamna kitu very slow yaani hata udownload huwezi maliza mb 500 kwa mwezi nahisi speed ni kb 0.001 per sec siwapendi.
Internet nzuri ni voda.airtel.tigo na zantel hawa ttcl sijui shida ni nini.

Speed yao ni sawa na utendaji wa Chama Tawala!
 
Kitambo ngota mpaka leo bado upo tuu?nilizani amehama TTCL
Sasa Airtel juzi nimetoa 45000tshs wakanipa8GB sijui ni offer

...Kuna wakati aliondoka nafikiri. Karudi tena TTCL??
 
Back
Top Bottom