Mambo ya Sabodo ni haya

Suzie

JF-Expert Member
May 7, 2010
1,259
409
Mustafa Sabodo ametoa msaada wa kujenga visima 10 vyenye thamani ya Sh75 milioni kwenye Jimbo la Ulanga Mashariki mkoani Morogoro.

Visima* hivyo ambavyo tayari vimeshakamilika vimejengwa katika Kata ya Mwaya vitatu vipo kwenye* Shule ya Msingi Libenanga, Sekondari ya Celina Kombani na Kijiji cha Nkongo.

Kata ya Mbuga kisima kipo katika Sekondari ya Mbuga, Kata ya Ilonga katika Sekondari ya Ilonga, Kata ya Chirombola katika sekondari ya Chirombola, Kata ya Vigoi katika Sekondari ya Mahenge mjini na Kijiji cha Safari Rodi, Kata ya Msogezi katika Shule ya Msingi Nalukoo* na Kata ya Euga katika Kijiji cha Ebuyu.

Akikabidhi visima hivyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti na Utumishi wa Umma, Celina Kombani amesema kuwa pamoja na misaada hiyo pia Sabodo ameahidi kuendelea kulisaidia jimbo hilo katika sekta mbalimbali.

Kombani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la* Ulanga Mashariki amesema kuwa Serikali haiwezi kutatua changamoto zote hivyo ni muhimu kushirikisha wafadhili binafsi ambao wamekuwa wakijitolea kusaidia maendeleo hapa nchini.

Naye Mhandisi wa Maji Wilaya ya Ulanga, Patrice Jarome amesema miradi hiyo ya visima 10 imetokana na jitihada mbalimbali za mbunge huyo kutafuta wafadhili kwa ajili ya kutatua tatizo la maji kwa baadhi ya vijiji vya Jimbo la Ulanga Mashariki.
 
nadhani misaada ya bwana Sabodo ni endelevu zaidi ya yule mzee wetu ambae huandaa chakula ndizi nyama na soda kisha kuonyesha kwenye tv na radio zake kwamba anasaidia kulisha.....
 
Nawezaje kuwasiliana na huyu Mzee anisaidiie tatizo la maji hapa kijijini kwangu!!!!!! Kata ya Nanyamba huku mtwara
 
nadhani misaada ya bwana Sabodo ni endelevu zaidi ya yule mzee wetu ambae huandaa chakula ndizi nyama na soda kisha kuonyesha kwenye tv na radio zake kwamba anasaidia kulisha.....
wehoodie umeongea point ya maana sana..... Yule mzee anavyofanya mimi naona kama anawadhalilisha walemavu...hana nia ya dhati ya kuwasaidia
 
Last edited by a moderator:
nadhani misaada ya bwana Sabodo ni endelevu zaidi ya yule mzee wetu ambae huandaa chakula ndizi nyama na soda kisha kuonyesha kwenye tv na radio zake kwamba anasaidia kulisha.....

Ni kama CCM wanawalisha pilau nyama wananchi kwa siku moja,siku zinazofuatazo mtajiju na njaa zenu;SABODO ni mzarendo sana MUNGU amjaalie maisha marefu.
 
Tungekua na Ma-Sabodo wa 3 hapa Tz, basi hata uchungu wa mafisadi kama yeye tusingeusikia
 
Back
Top Bottom