Mambo ya Mwenge kwa waosha miguu na wapata rangi.

Mambo ya Mwenge kwa waosha miguu na wapata rangi.

Retreat

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2010
Posts
229
Reaction score
72
Jamani wadau mnaliongeleaje hili suala la wale wakaka wa pale Mwenge? maana ndoa zinavunjika tu siku hizi. Cheki hii katuni.

Source: Global Publishers Mwenge.jpg
 
sasa ndoa wanavunjaje kama sio mademu wenyewe wanaotaka ni mtu akiwa na msimamo wake ndoa haivunjiki hata tone
 
kama maumivu ya kichwa yanaaanza pooole poole
vivyo hivyo na kwa wapaka rangi na kukata kucha!
 
wapo kazini bwana wanasaka kipato.wala hawana shida yeyote vipi wamekuchukulia nini?

Sawa lakini polepole basi, maana wengine kila jmosi tunaagwa kuwa anakwenda Mwenge kupaka rangi sijui na kuoshwa miguu, nimeshtuka sasa naanza kujifunza hii kazi, naipiga mwenyewe hakuna cha Mwenge wala nini.
 
sasa ndoa wanavunjaje kama sio mademu wenyewe wanaotaka ni mtu akiwa na msimamo wake ndoa haivunjiki hata tone

Big One we ongea tu kirahisi rahisi hivyohivyo, ukiisha ibiwa ndo utashtuka.
 
Hawajajua tu kushika soko la watu fulani hivi. Wanahuduma nzuri sana, waweza sinzia kabsaa. Tuwachangie wapate sehemu nzuri zaidi waweke na vitanda. Wadada mnaonaje hili? They are stress releasers.
 
mmeanza na wauza nguo sasa memrudi huku................haya tuendelee

Bora wauza nguo, hawa ni balaa zaidi. Kwani wanawatekenya sana wanapokuwa wanawaosha miguu. Wauza nguo access ya kugusana ni ndogo sana.
 
Hakuna ndoa inavyovunjika wala nini? inategemea umeenda pale kufanya nini kama hujieshimu ukaanza kuwachekea ndo ndoa zinavunjika usiwaharibie wenzako biashara bwama.
 
Hawajajua tu kushika soko la watu fulani hivi. Wanahuduma nzuri sana, waweza sinzia kabsaa. Tuwachangie wapate sehemu nzuri zaidi waweke na vitanda. Wadada mnaonaje hili? They are stress releasers.

Ati! Tuwachangie wapate sehemu nzuri zaidi waweke na vitanda? Weweweeee! Utaua watu kwa presha sasa. Hata kama ni stress releasers kwa wadada lakini sio kwa wakaka.
 
Mm nafikiri wao tu kujiangalia ni nini walichofuata pale,na wapakaji wazingatie kilichowaweka pale,
kuhusu suala la kuibiwa litakuwa limewekwa pembeni,
na mara zote kumbuka
aliwazalo mjinga ndio litakalo mtokea.
Au awazavyo mtu nafsini kwake ndivyo alivyo.
 
Back
Top Bottom