Mambo ya msingi kuyafanya kabla ya kuoa/kuolewa

Mambo ya msingi kuyafanya kabla ya kuoa/kuolewa

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2016
Posts
1,288
Reaction score
1,262
Ndoa nyingi zinaingia kwenye migogoro kwa sababu ya mambo ya kukurupuka na kufanya haraka bila wahusika kufahamiana vizuri, hebu tuzingatie yafuatayo ili tusiseme 'NINGEJUA NISINGEOA/NISINGEOLEWA'

1. Chanzo cha uhusiano wenu kiwe ni upendo wa dhati

2. Chunguza kwa mwenzio juu ya tabia:nidhamu, adabu, hasira, ulevi na umalaya.

3. Mpeane muda wa kutosha kufahamiana.

4. Mtembee pamoja maeneo tofautitofauti kama michezoni, bar na out mbalimbali ili muone interest za kila mmoja.

5. Muwe wa imani moja, ila kama mmeshibana sana na mwaweza kuvumiliana hata wa imani tofauti ni sawa.

6. Wajue ndugu wa mwenzio ili kupata habari zao zitakazokufahamisha mwenzao pia yukoje.

7. Pimeni afya zenu bila aibu,kuna maradhi mengi kama HIV/AIDS na mengine.

8. Kama ni Mkristo au Muislam funga ndoa Kanisani au Msikitini na siyo Bomani.

9. Kwa Wakristo ndoa haina talaka huu ni mpango wa Mungu kuachana na kuoa mwingine ni dhambi.

N.B: Kama mwenzio ana tabia usiyoipenda, usifunge ndoa naye ukitegemea atabadilika,abadilike wakati mkiwa wachumba na siyo kwenye ndoa, labda kama umeshamkubali kama alivyo.
 
1464370468620.jpg
 
WATU wanakuwa pamoja hadi 5 yrs bila kuoana wakija kuoana ndani ya miezi 4 tu kitu kina buna, zamani watu walikuwa wanakabidhiwa mme/mke bila hata ya kufahamiana ila walidumu hadi kufa kwao , wakiwa pamoja.

Cha mhimu ni Kuomba Mungu basi, hakuna cha Pythogrus wala Logarithm kwenye Mapenzi.
 
Hahahaaa eti wanakaa miaka mitano wakioana tu hata miezi minne haifiki
WATU wanakuwa pamoja hadi 5 yrs bila kuoana wakija kuoana ndani ya miezi 4 tu kitu kina buna, zamani watu walikuwa wanakabidhiwa mme/mke bila hata ya kufahamiana ila walidumu hadi kufa kwao , wakiwa pamoja.

Cha mhimu ni Kuomba Mungu basi, hakuna cha Pythogrus wala Logarithm kwenye Mapenzi.
 
UKIMWI janga yaan unaweza achwa iv iv kisa umeomba mkapime.
 
ndoa nyingi zinaingia kwenye migogoro kwa sababu ya mambo ya kukurupuka na kufanya haraka bila wahusika kufahamiana vizuri, hebu tuzingatie yafuatayo ili tusiseme 'NINGEJUA NISINGEOA/NISINGEOLEWA'
1. chanzo cha uhusiano wenu kiwe ni upendo wa dhati
2. chunguza kwa mwenzio juu ya tabia:nidhamu, adabu, hasira, ulevi na umalaya
3. mpeane muda wa kutosha kufahamiana
4. mtembee pamoja maeneo tofautitofauti kama michezoni, bar na out mbalimbali ili muone interest za kila mmoja
5. muwe wa imani moja. ila kama mmeshibana sana na mwaweza kuvumiliana hata wa imani tofauti ni sawa.
6. wajue ndugu wa mwenzio ili kupata habari zao zitakazokufahamisha mwenzao pia yukoje
7. pimeni afya zenu bila aibu. kuna maradhi mengi kama HIV/AIDS na mengine.
8. kama ni Mkristo au Muislam funga ndoa Kanisani au Msikitini na siyo Bomani.
9.Kwa Wakristo ndoa haina talaka. huu ni mpango wa Mungu. kuachana na kuoa mwingine ni dhambi.
N.B: kama mwenzio ana tabia usiyoipenda, usifunge ndoa naye ukitegemea atabadilika.abadilike wakati mkiwa wachumba na siyo kwenye ndoa, labda kama umeshamkubali kama alivyo
Thank u
 
WATU wanakuwa pamoja hadi 5 yrs bila kuoana wakija kuoana ndani ya miezi 4 tu kitu kina buna, zamani watu walikuwa wanakabidhiwa mme/mke bila hata ya kufahamiana ila walidumu hadi kufa kwao , wakiwa pamoja.

Cha mhimu ni Kuomba Mungu basi, hakuna cha Pythogrus wala Logarithm kwenye Mapenzi.
hitilafu ktk ndoa zipo za kutosha na wakati mwingine ni bahati mbaya. ktk hali kama hii inahitaji sana busara na kumwomba sana Mungu na uvumilivu. ila hoja yangu ni kwamba wengi wakijiaandaa vema bila kykurupuka watadumu. tena hakuna kitu kibaya kwa karne hii kama kuchaguliwa mke. watu wapendane wenyewe.
 
UKIMWI janga yaan unaweza achwa iv iv kisa umeomba mkapime.
ni heri kujua afya yako kabla ya kuoa/kuolewa. mwenzio akiwa nao umwache ila mpe faraja na matumaini na usimtenge. na ww ukiwa mgonjwa basi mwache mwenzio usimwambukize na usikate tamaa.
 
Back
Top Bottom