khaliciouz
JF-Expert Member
- Nov 12, 2013
- 579
- 212
Mambo ya Meseji za Kwenye Simu:
Hapa Mtaani kwetu, kuna Kijana mmoja alikuwa akimpenda sana msichana wa nyumba ya jirani. Lakini masikini huyu kijana hakuwa na ujasili wa kumweleza yule msichana kuwa anampenda.
Siku moja akaamua kuondoa woga, akasubiri mida ya saa tano usiku, akatuma meseji kwa sms, akaandika kwa Kiingereza.
"I love you, I wanna date you. Plz reply & tell me how u feel."
Baada ya sekunde mbili tu, akasikia simu yake ikihalika kuwa kuna ujumbe umeingia. Kijana wa watu akapata woga akaogopa hata kushika simu. Akaamua kusubiri mpaka asubuhi.
Usiku kucha hakupata usingizi, ilipofika alfajiri, akaamua kwa mara ya kwanza kusali swala ya alfajiri akiomba meseji ile iwe na majibu yatakayomletea faraja.
Akaoga vizuri na kupiga mswaki, akavaa nguo zake nzuri, kisha akanywa chai, alipomaliza akapanda kitandani, na kuchukuwa simu yake ili asome ujumbe ulioko kwenye simu.
Alipofungua simu yake na kusoma ujumbe, ulikuwa unasema hivi:
"Dear Customer You Have Insufficient Balance To Send This Message.
Please Recharge Your Account & Try Again Later".