Sinabudi kumshukuru mungu kwa kumpatia dawa babu yetu wa Loliondo kwahajili
ya kutibu magonjwa KATILI bin SUGU yaliyokosa dawa zake hapa duniani kwahajili
ya kutibu ukimwi,kansa,kisukari nk. Nasema ahsante mungu,ahsante babu wa loliondo. Lakini kunakitu nimegundua kuhusiana na watu wanaotuletea habari hizi
kupitia mablog,magazeti,radioni na hata kwenye luninga toka habari hizi ziwe hot
cake takribani wiki tatu hivi. -Swali langu ni -Hivi kwanini hakuna mtu yeyote aliyeji
tokeza hapa jamvini live au kwenye media zingine na kukili kuwa mimi ni mmoja kati ya watu waliotoka au waliopo loliondo kwa babu kwa kusumbuliwa na ukimwi au kansa au kisukari na sasa nimepona baada ya kutumia dawa za babu huyo wa
loliondo? Badala yake utakuta watu au mtu anakuja hapa jamvini au kwenye media
zingine na kusema ooooh....huyo babu si mchezo anatibu kila kitu! au utamsikia
mtu anasema mimi nilimpeleka rafiki yangu kwa babu na sasa amepona. Au utasi
mimi nilidrive na familia yangu kwa safari ya shida sana hadi loliondo,lakini baada ya mateso ya kadha wa kadha hatimae familia yangu ilipata dawa na sasa wote wamepona (yeye kajitoa hapo) na sasa tumerudi. Mwingine oooooh.... nilimpeleka
shangazi au mjomba kwenye machela,lakini baada ya kunywa dawa ya babu'ghafla
alisimama na sasa amepona kabisa. Swali langu la pili ni -hivi kwanini mtu usiseme
kuwa wewe ndiye muhusika? ulikuwa unaumwa ukimwi au kansa au kisukari na sa
sa umepona kupitia babu? kwanini kila mtu anatuletea habari ya loliondo kupitia
ushuhuda wa mtu mwingine? kwani ukiwa muwazi na kukiri wewe ndiye muhusika
mwenyewe itaaribika nini?
Mie nafikiri tufike sehemu tuwe wawazi hasa kwenye mambo tata kama haya ili iwe
faida kwa jamii mzima. - Nawasilisha waungwana
Mungu ibariki Tanzania,Mungu mbariki babu wa Loliondo
a. Dawa ya Mungu hainaga masharti, hata ukipewa sio masharti kama ya Loliondo eti hakuna mtu mwingine kukupa dawa hiyo ukanywa zaidi ya yeye peke yake View attachment 24640
Hebu ngoja tuone, hivi kumbe Mfalme Naamani yeye hakupewa masharti? Sijui bana haya mambo mie, kikubwa matendo yangu tu, the rest are details
IS this a breaking news?
KWAMBA NI KUTOKA KWA MUNGU AU KWA SHETANI SIJUI, NINACHOJUA MIMI NI KWAMBA NILIKUWA MGONJWA NA SASA NIMEPONA
Habari Za wandugu wa JF,
Nimeamini kuwa kilichosemwa na BIBLIA hakitabadilika hata kama ni kwanini.
1.WATU HAWA WANAMACHO LAKINI HAWAONI, WANAMASIKIO LAKINI HAWASIKII.
2. WENGI WATAKUJA KWA JINA LA MUNGU.
Tusibabaishwe na mganga wa Loliondo ukweli hakuna Mungu wa namna hiyo yeye angetumia tu jina la Mganga wa kienyeji sio Mungu unajua ni kwanini?
a. Dawa ya Mungu hainaga masharti, hata ukipewa sio masharti kama ya Loliondo eti hakuna mtu mwingine kukupa dawa hiyo ukanywa zaidi ya yeye peke yake swali: Watumishi wa Mungu Loliondo ni yeye peke yake? kama wengine wapo kwanini wasisaidiane? si kumpa tu mtu maji anakunywa??
b. Kwanini mti huo kama umefunuliwa na Mungu ukitumiwa na wengine usiponye?? Maana yake Mungu ameanza lini kutufundisha ubinafsi na uchoyo?
Nikomee hapa nitarudi! View attachment 24640