Sema Tanzania
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 251
- 466
Fahamu jinsi ya kuwasiliana na mtoto mchanga - mtoto mchanga akiwa ameshiba, ataachia ziwa au kikombe cha maziwa, atafunga mdomo ishara kuonyesha hataki kuendelea kunyonya. Atageukia pembeni na hata anaweza kusinzia kabisa.
Jinsi ya kufahamu kuwa mwanao ana njaa - mtoto aliye na njaa atakuwa ananyonya vidole vyake au ngumi yake, atanyonya midomo na ulimi huku akitoa sauti ya kama anaenyonya, atageuka na kuelekea lilipo ziwa huku mdomo wake ukiwa wazi. Na kama ataona mama yake hamwelewi atalia.
Jinsi ya kujua kuwa mwanao amechoka. Mtoto aliyechoka atakuwa analialia, anafumba na kufumbua macho, anapiga miayo, anatupatupa miguu, akipewa kitu hataki anageukia upande mwingine, anapinda mgongo kama anaetaka kujitoa au kuwa kando.
^ #Malezi @SemaTanzania