Ajira ni darasa jipya katika mfumo wa vitendo, kuwa na tabia njema, jitahidi kadri uwezavyo kutunza sana muda, kuwa na malengo, fata sheria, taratibu na miongozo, heshimu wakubwa kwa wadogo, nafasi uliyonayo ilikuwa na watu, wamepita, kumbuka kuwa hata wewe ipo siku hautakuwepo hapo, acha alama na kumbukumbu njema kuhusu wewe, wape watu furaha nawe hakikisha unafurahi kwa kuwa hapo kazini, ipende kazi yako na uifanye kwa ufanisi.
La kuzingatia zaidi, ajira ni utumwa na hautokaa utimize malengo yako kwa kupitia ajira, jitahidi kadri uwezavyo utengeneze vyanzo vya ziada vya kipato.
Ukiweza fanya ajira yako kuwa ni sadaka kwa kuwafanya wanaokuzunguka kama wazazi, ndugu na jamaa wafurahi kwa kuwa kwako na ajira.
Akili za kuambiwa, changanya na za kwako