Mambo ya kuzingatia kwa kijana msaka ajira

Mambo ya kuzingatia kwa kijana msaka ajira

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
4,580
Reaction score
7,955
Ni furaha kwa kijana na mzazi au mlezi wake kuona kijana wake anajitegemea na kutegemewa pia.
Ili kijana aweze kujitegemea na kutegemewa lazima awe amejiajiri au ameajiriwa. Ila mara nyingi suala la kujiajiri ili lifanyike kwa ustawi ni vyema mtu awe amewezeshwa vya kutosha au awe mwajiriwa wa kipato angalau cha wastani.
Huu ni ushauri kwa wanaotaka kuajiriwa hasa serikalini kwa zama hizi zenye ushindani mkubwa;
1.Soma alama za nyakati,hapa lazima ujue sera kuu ya kiongozi/rais wako. Kasomee kitu ambacho Rais ndicho anakiongea kila leo na uache kusoma kwa sifa. Hapa kama umesoma kozi ambazo hazina soko cha msingi uangalie ni kozi gani isiyo na gharama na ni fupi na pia ni marketable.
2.Pitia matangazo mbalimbali ya ajira kila leo, hii itakusaidia kujua aina ya kazi ambazo hutangazwa mara kwa mara na sifa zake. Zoezi hili litakuwezesha kusoma kozi fulani zitakazokulipa.
3.Soma kozi ambazo karibu kila taasisi inauhitaji wa watu hao na ushindani wake ni mdogo. Mf. Udereva, ukatibu muhtasi(usekretari), uhasibu, manunuzi n.k.
4.Ingia mitandaoni mara kwa mara ili ujifunze maswali ya usaili kwa kada yako. Youtube na google kuna maswali na majibu mengi. Kumbuka siku hizi ajira za mafungu zinaelekea kuishia kabisa. Kanuni ya mwenye kisu kikali ndiye hula siku hizi inamata sana. Hata maH.R maswali hutoa mtandaoni sometimes.
5.Usicheze mbali na media kama magazeti, radio na intabent . Hii itakupa nguvu ya kupass kwenye written interviews. Maswali ya written ni ya jumla/random.
6.Jifunze kuandika wasifu nzuri(C.V) acha kwenda stationary na kumwambia binti wa stationary akutolee C.V iliyohaririwa. Jifunze pia kuandika barua nzuri kwa ufupi.
Mambo mengine nitayajazia.
Thanks
 
Safi na hongera kabisa.
Naamini, vijana watapata kitu hapo.

Sisi vijana wa zamani, ndiyo tunaouliza maswali kwa sasa hatuhitaji tena hizi techniques.
Haaaa haaaa haaaaaa haaaaaa haaaaaa haaaa.
 
Safi na hongera kabisa.
Naamini, vijana watapata kitu hapo.

Sisi vijana wa zamani, ndiyo tunaouliza maswali kwa sasa hatuhitaji tena hizi techniques.
Haaaa haaaa haaaaaa haaaaaa haaaaaa haaaa.
Tatizo vijana wa kileo kazi ya smartphone wanajua ni kwa whatsap tu mengine ni ziada.
Kijana kila siku anawaza kicreate group jipya tu.
Mungu atusaidie
 
Tatizo vijana wa kileo kazi ya smartphone wanajua ni kwa whatsap tu mengine ni ziada.
Kijana kila siku anawaza kicreate group jipya tu.
Mungu atusaidie


Mkuu, ni kweli na Instagram ongezea fb akili zote zinabakia "naomba anisaidie ku-share /ku-post" ni tatizo.
 
Back
Top Bottom