Mambo ya kuyaepuka kwenye gear box ya Automatic

Mambo ya kuyaepuka kwenye gear box ya Automatic

Neutral huwa ni kichocheo kikubwa cha kuharibu brake pads.Since nimeanza driving sijawahi kutumia N just kuokoa mafuta kama wengi wanavyofanya, sababu huwa haijawahi kuniingia akilini kuokoa kiasi kidogo cha mafuta kwa ku risk break pads ambazo ni one ya mechanism za muhimu za kuokoa maisha yangu,ya wengine na gari pia kwa ujumla.
 
Neutral huwa ni kichocheo kikubwa cha kuharibu brake pads.Since nimeanza driving sijawahi kutumia N just kuokoa mafuta kama wengi wanavyofanya,sababu huwa haijawahi kuniingia akilini kuokoa kiasi kidogo cha mafuta kwa ku risk break pads ambazo ni one ya mechanism za muhimu za kuokoa maisha yangu na gari pia kwa ujumla.

Halafu gari nyingi ukishakuwa mteremkoni ilimradi hujakanyaga brake basi mafuta kidogo sana yatakuja kwenye engine...
 
Neutral huwa ni kichocheo kikubwa cha kuharibu brake pads.Since nimeanza driving sijawahi kutumia N just kuokoa mafuta kama wengi wanavyofanya,sababu huwa haijawahi kuniingia akilini kuokoa kiasi kidogo cha mafuta kwa ku risk break pads ambazo ni one ya mechanism za muhimu za kuokoa maisha yangu,ya wengine na gari pia kwa ujumla.
Huwa natumia N kwenye foleni kali au kwenye mataa.

Kukanyaga break muda wote inachosha.
 
Na ndio maana hakuna sehemu nimetaja forward gear yoyote maana hizo ndio huwa zinabadilika automatic.

Mfano wa gear ambazo hazibadiliki automatic ni kutoka D kuja R, D kuja 2, D kuja L n.k. Hapa ndio hasa napaongelea.

Sasa hizi gear ulizotaja ndio ambazo mtu hapaswi kubadili wakati gari ikiwa kwenye mwendo (motion)?
 
And I have been doing it for number of times without problems and its advisable! L or L2 Ina speed range yake.ex.L2 Ina speed range up to 40km/hr in some cars-therefore ukiwa kwenye speed range ya up to 40km/hr unaweza shift from D to L2

Hebu nifahamishe kidogo mkuu, when do switch from D to L or to L2 or D4 ..!
 
Hebu nifahamishe kidogo mkuu, when do switch from D to L or to L2 or D4 ..!
D ina optional gear nyingi from 1st,2nd,....6th nk. na speed range yake ni 0km-180km/hr,range ya speed inaweza kuwa more or less kwendana na limiter ya gari husika.

L ni gear kubwa equivalent to 1st gear kwenye manual transmission assuming range yake ni 0km/hr-20km/hr
L2 inategemea kwendana na gari husika,ina speed range yake let's say equivalent ya 2nd gear kwenye manual car assuming kwamba range yake ni 0km/hr to 40km/hr.

Ni wakati gari utumie range ipi inategemea na mazingira na uamuzi wa mtu binafsi

Mf.
*Kwenye vibao vya barabarani ambavyo speed limit ni 40km/hr-50km/hr wengine wana opt L2 ili kuweza kuendana na speed limit ya eneo husika na kuepuka kujisahau, kwenye hili wengine huwa makini kwenye acceleration na hutumia D tu ku control acceleration kwa kuongozwa na dashbord na mengineyo na kuondokana na karaha ya shifting.

*Kwenye eneo lenye utelezi na mteremko mkali naweza opt L ambayo itapunguza speed ya gari na kuzipunguzia brake pads stress kutokana na kusaidiwa na engine ambayo itakuwa inatoa some form of engine braking.

ECU haitaliruhusu gari ku roll zaid ya 20km/hr ikiwa kwenye L assuming limit yake ni up to 20km/hr.Lakini gari likiwa ni AWD or 4WD hutakuwa na sababu ya kuopt L ili kufanya matairi yasi sleep kwenye utelezi.

All ni all inategemea na mtu na mtu.
 
Ili automatic gear box iwe imara zaidi.zingatia saana kubadili Oil ya gear box(Transmission Oil) ZINGATIA SAANA KTK UBADILISHAJI WA
OIL SIO ILIMRADI HYDRAULIC OIL TU.NDIO UWEKE HAPO UTAUWA GEAR BOX YAKO.

HAKIKISHA KABLA YA KUMWAGA OIL YA KWENYE GEAR BOX CHOMOA OIL STICK YA GEAR BOX KISHA IPANGUSE HALAF TAZAMA KUNA NAMBA ZIMEANDIKWA KTK OIL STICK HIO..HIZO HIZO.NDIO NAMBA ZA OIL YA GEAR BOX YAKO AMVAYO UNAPASWA UKAINUNUE
 
Huwa natumia N kwenye foleni kali au kwenye mataa.

Kukanyaga break muda wote inachosha.

Nimeshafungua gearboxes kadhaa za automatic.

Huwa inakuwa na clutch pack kadhaa ndani ambapo ndani ya kila clutch pack kunakuwa na clutch kadhaa. Pia ukiangalia michoro ya umeme ya gearbox huwa kunakuwa na uhusiano kati ya gearbox na brake system.

Sasa katika clutch pack zote huwa inakuwepo moja ambayo huwa inadisengage unapokanyaga brake na kuengage unapoachia brake.

Hivyo kukanyaga tu brake siyo vibaya
 
Sasa hizi gear ulizotaja ndio ambazo mtu hapaswi kubadili wakati gari ikiwa kwenye mwendo (motion)?

D kwenda R pamoja na kinyume chake ni lazima usimame na ukanyage brake....

Kutoka D kwenda zilizobakia... kuna mazingira lazima ukanyage brake kwa sababu mfano kama L, 2, 3, B n.k. zote ni low gears... Hivyo kama upo speed kubwa basi kukanyaga brake is a must.
 
Nichangie na mimi Pointi namba 3.... Nimewahi kuona spear tire imeandikwa kuwa isitumike zaidi ya umbali wa 60km, aina ya gari ilikuwa ni hizi minicars zenye 660cc.
Kale kaspea tairi majanga sana. .
Kwenye gari yangu huwa nikikafunga mbele , taa ya ABS na Parking brake zinawaka ila gari linatembea kawaida...Nikikatoa tu nikaweka tairi husika, taa zinazima...hiki kitu kimenitokea mara mbili
 
D ina optional gear nyingi from 1st,2nd,....6th nk. na speed range yake ni 0km-180km/hr,range ya speed inaweza kuwa more or less kwendana na limiter ya gari husika...

Kwa gari za kisasa hata ukitembelea L au L2 kwa muda mrefu itajibadilisha na kwenda kwenye higher gears ili kuepusha kuistress engine kwa muda mrefu hasa kama umekanyaga sana accelerator pedal.
 
Kale kaspea tairi majanga sana. .
Kwenye gari yangu huwa nikikafunga mbele , taa ya ABS na Parking brake zinawaka ila gari linatembea kawaida...Nikikatoa tu nikaweka tairi husika, taa zinazima...hiki kitu kimenitokea mara mbili

Hahah Dah. Sijui shida itakuwa nini.
 
2. Usizidishe mzigo kwenye gari lako
Kama unataka kuvuta tela au kubeba mzigo mkubwa ni vizuri ukarejejea kwenye owners manual ya gari lako.
magari ya mizigo yakiingizwa nchini yanapelekwa Arusha kufanyiwa modification ya chasis, axle na body ili ibebe lumbesa. Engine na Gearbox huwa haziguswi.

Na gari inapiga mzigo fresh.

Inakuaje?
 
magari ya mizigo yakiingizwa nchini yanapelekwa Arusha kufanyiwa modification ya chasis, axle na body ili ibebe lumbesa. Engine na Gearbox huwa haziguswi.

Na gari inapiga mzigo fresh.

Inakuaje?

Kwanza hapa nazungumzia gearbox za automatic ingawa pia natambua kwamba kuna malori yana gearbox za automatic.

Yote kwa yote kama mzigo wanaoubeba uko within range inayotakiwa wala hakuna shida. Ila kama wanazidisha na wana gearbox za automatic basi wanapunguza maisha ya gearbox kwa haraka sana.
 
Nimeshafungua gearboxes kadhaa za automatic.

Huwa inakuwa na clutch pack kadhaa ndani ambapo ndani ya kila clutch pack kunakuwa na clutch kadhaa. Pia ukiangalia michoro ya umeme ya gearbox huwa kunakuwa na uhusiano kati ya gearbox na brake system...
Namanisha nachoka kukanya brake all the time. Naweka N halafu nachomoa mguu.

Maana kuitoa D kwenda P na kuirudisha all the time haina tofauti na kuendesha manual.
 
Namanisha nachoka kukanya brake all the time. Naweka N halafu nachomoa mguu.

Maana kuitoa D kwenda P na kuirudisha all the time haina tofauti na kuendesha manual.

Okay nilijua unafanya hivo ili kuisave gearbox yako na kuisha haraka.

Japo hata hapo ni kama tu unaendesha manual. Maana kila ukisimama lazima uhamishe gear lever.
 
kwani gearbox za manual zenyewe hazipati moto zikizidisha mzigo kama za automatic?

Gearbox ya manual kama kuna joto linazaliswa ni kidogo sana na ndio maana ni ngumu kukuta gearbox ya manual inakufa kizembe unless kama mtumiaji alikuwa anashift gear vibaya.

Utofauti wa gearbox ya automatic na manual upo kwenye clutches. Gearbox ya manual ina clutch moja tu na system yake ya clutch inajitegemea(independent). Hivyo hata ikizingua wala huhangaiki na gearbox.

Sasa njoo kwenye automatic. Picha linaanza kuna viclutch zaidi ya 20 humo ndani na kila kimoja kinazalisha joto kwa wakati wake. Na ukibeba mzigo ndio kabisaaaa joto linakuwa juu.

Hivyo athari ya joto ni kubwa sana kwenye automatic gearbox kuliko kwenye manual.
 
Back
Top Bottom