Mambo ya kuyaepuka kwenye gear box ya Automatic

Mambo ya kuyaepuka kwenye gear box ya Automatic

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
3,383
Reaction score
9,835
images (4).jpeg

Nimejaribu kuweka baadhi ya vitu vichache ambavyo huenda watu wanavifanya na vinaleta shida. Natambua kwamba vipo vingi ila nimeandika vichache tu. Kama kuna mtu anaweza kuongezea, karibu.

Okay sasa tuendelee,

1. Usiwashe gari na kuanza kupiga resi
Ukiwasha gari yako ni vizuri kuiacha ifikie joto lake kabla ya kuanza kuresi. Pia kama unaondoka ni vizuri ukakanyaga accelerator taratibu, Kama utakanyaga kwa nguvu unaweza kufanya clutch bands kwenye gearbox yako kuisha haraka na hivyo gearbox yako haitaishi maisha marefu.

2. Usizidishe mzigo kwenye gari lako
Mizigo mikubwa inaweza kupelekea gearbox kufanya kazi katika joto kubwa kuliko joto lake la kawaida. Hii inaweza kupelekea vitu kusagana harakaharaka ndani ya gearbox yako na hivyo kupunguza urefu wa maisha ya hiyo gearbox. Kama unataka kuvuta tela au kubeba mzigo mkubwa ni vizuri ukarejejea kwenye owners manual ya gari lako.

3. Usiendeshe gari muda mrefu huku ukiwa umefunga spea tairi(temporary spear tyre)
Kuna mtu unakuta amefunga kile kispea tairi kidogo, halafu ndio anaendesha hilo gari kila siku. Kutumia tairi dogo la spea kwa muda mrefu inaweza kuwa na athari kubwa mbili. Moja, inapelekea kubadilika kwa alignment kwenye mfumo wa suspension wa gari yako. Mbili, Unakuwa unaistress gearbox yako na hivyo kuipunguzia urefu wa maisha yake.

4. Usibadili gear gari inapokuwa inatembea
Gearbox za automatic huwa zinakuwa na bands za clutches. Kutegemeana na aina gearbox unaweza kukuta gearbox ina hata bands 8 za clutches. Kila band huwa inakuwa na lock pin. Hivyo kama unabadili gear huku gari inatembea inaweza kupelekea lock pin kuhama kwenye njia yake au hata kuvunjika. Hili likitokea inaweza kupelekea gearbox yako kukosa gear kabisa au kupata gear fulani kwa shida.
 
Maisha yangu yote, sijawahi kuendesha gari automatic, nijuavyo mimi ni kuwa automatic ukishaweka D ni unakajaga mafuta tu,

Naomba unifafanulie hapo uliposema kuwa "usibadili gia,gari inapokuwa inatembea umenichanganya kidogo mkuu"

Maelezo tafadhali.
 
Ndugu yangu haya mambo acha tu! Nina escudo old na ni automatic transmission nilimuazima mtu karudisha gear box kwisha nikapeleka Kwa fundi anabadilisha vifaa baadhi tu, sasa nikiingiza gia inakuwa inashtuka hivi, hasa reverse, je hii ina maana gani wakuu?

Possible kuna valve ina stuck. Nikizicheck valves zake tunaweza kupata solution.
 
Ndugu yangu haya mambo acha tu! Nina escudo old na ni automatic transmission nilimuazima mtu karudisha gear box kwisha nikapeleka Kwa fundi anabadilisha vifaa baadhi tu, sasa nikiingiza gia inakuwa inashtuka hivi, hasa reverse, je hii ina maana gani wakuu?

Nicheck 0621221606
 
Usibadili gear gari inapokuwa inatembea.


Fafanua kidogo hapa mkuu

Mfano shifting from D to R hapo umebadili gear. Sasa ukifanya hivo wakati gari inatembea unasaga vitu.
Maisha yangu yoote, sijawahi kuendesha gari automatic, nijuavyo mimi ni kuwa automatic ukishaweka d ni unakajaga mafuta tu,

Naomba unifafanulie hapo uliposema kuwa "usibadili gia,gari inapokuwa inatembea umenichanganya kidogo mkuu"

Maelezo tafadhali.
 
Hata ukitoka D kuja 2, 3 n.k. kama gari inatembea. ni majanga. Gearbox automatic ni kama mayai tu...

Japo ukiitunza inakaa
 
Mkuu kwenye gari ambayo ni semi-automatic (CVT) kama hiyo katika picha. Mtu mwingine hapendelei kuendesha kama automatic anachagua upande huo wa manual ambapo kuna alama + na - . Je, kuna madhara ya kufanya changedown au enginebrake kwa hizo gear box.
Hakuna. Na hata kubadili kutoka D kwenda kwenye hiyo S au M then unachange up and down unafanya gari ikiwa inatembea.
 
Mkuu hivi unaweza badili toka D kwenda R wakati gari inatembea na ikawa sawa tu,au mimi ndo nachanganyikiwa
Kutoka D kwenda R wakati gari linatembea ni balaa. Unaweza kuua gearbox. Na mifumo ya gari nyingi za kisasa haiwezekani kutoka D kwenda R ukiwa kwenye mwendo. Hata ukijaribu inagoma kabisa.
 
Mkuu kwenye gari ambayo ni semi-automatic (CVT) kama hiyo katika picha. Mtu mwingine hapendelei kuendesha kama automatic anachagua upande huo wa manual ambapo kuna alama + na - . Je, kuna madhara ya kufanya changedown au enginebrake kwa hizo gear box.

Mkuu kwa semi-Automatic gearboxes sifahamu chochote kwa kweli.
 
Boss unataka kuniambia natakiwa kusimama ili nibadili kutoka D kwenda 2 au L...huwa nikiwa milimani wakati wa kushuka nimekuwa nikifanya hivyo...

Kutoka D kuja kwenye hizo 2 na L maana yake ni unatoka gearkubwa kuja gear ndogo. Kama upo katika speed kubwa ukibadili kuja 2 au L ni majanga na utakuwa unasaga vitu. Kama upo kwenye speed ndogo haina shida.

Pia kuna watu wanatumia 2 na L kama engine brake. Hiyo ni very risk.
 
Back
Top Bottom