Mambo ya kustaajabisha na Kujifunza toka kwa Steve Jobs!

emma115

Senior Member
Apr 28, 2012
135
167
Habari za leo rafiki?
Ni matumaini yangu kwamba upo vizuri na unaendelea kuweka juhudi kubwa kwenye kile ambacho umechagua kufanya kwenye maisha yako.karibu katika makala hii.


Steve Jobs alikuwa ni mtu tegemezi sana na daima atakumbukwa katika mchango wake kuhusiana na suala zima la teknolojia ndani na nje ya Apple (kampuni).

Bidhaa za Apple tangu kuanzishwa kwake zimekuwa zikipendwa na wengi jambo ambalo limeifanya Apple kama kampuni kupata faida kubwa kutokana na bidhaa zao na aliyekuwa mstari wa mbele kuanzisha utamaduni wa kuhakikisha Apple inatengeneza vitu vizuri alikuwa ni marehemu Steve Jobs.

Je, unajua kuna vitu alikuwa akifavifanya ambavyo vinaweza vikakuacha mdomo wazi?! Pata kuvijua vitu hivyo kama ifuatavyo:-

  • 1. Alikwa na ndugu aliyekuja kumfahamu ukubwani. Steve Jobs alikiwa na dada aitwaye Mona Simpon ambaye alikuja kumfahamu ukubwani katika miaka ya 90. Hii ilitokana na kwamba Steve Jobs alikuwa ni mtoto aliyeasiliwa (adopted) na wazazi wake hawakuwahi kumwambia kuwa alikuwa na dada. Mona Simpson ni mwandishi wa vitabu na katika kitabu chake ‘Anywhere but Here’ alizungumzia mahusiano yake (Mona) na wazazi wake. Jobs alikuja kujua ni dada yake baada ya kumfafuta.

2. Baba mzazi wa Steve Jobs aliitwa Abdulfattah Jandali. Wazazi wa Jobs walikuwa ni wahitimu katika chuo fulani ambao kwa upande fulani walikuwa hawataki mtoto kwa wakati huo ndio maana akaasiliwa. Sharti lao lilikuwa ni moja tu kwamba Jobs aasiliwe na wasomi wa chuo kikuu ambapo wazazi waliomuasili Jobs walidanganya kuwa ni wanakidhi kigezo hicho lakini wazazi halisi wa Jobs walikuja kugundua watu wale si wasomi wa ngazi ya chuo karibu wakatae kuruhusu mtoto wao aasiliwe na watu hao mpaka walihaidi kuwa wangehakikisha Jobs anafika chuo kikuu

3. Alitengeneza gemu iitwayo “Breakout”. Ndio, Steve Jobs alitengeneza gemu iliyojulikana kama Breakout. Ni gemu ambayo ilipokelewa vizuri na baadhi ya watu kuamini kuwa Steve Jobs ni moja ya watu 100 wenye akili nyingi sana.

4. Alimkataa mtoto wake wa kwanza. Jobs alimkataa mtoto wake wa kwanza kwa sababu ya kuwa alikuwa hana uwezo wa kumpa mtu mimba. Sababu ya ukweli alikwa nayo mwenyewe moyoni lakini inawezekana ilikuwa damuni kwani hata yeye aliasiliwa. Lakini hapo baadae Steve Jobs alikubali na hata kuiita kompyuta aina ya “Apple III” Lisa (jina la mtoto wake wa kwanza).

5.Pesa yake alikuwa haitumii kwa kutoa misaada (charity). Hii ilihirika pale alipokuwa CEO wa Apple kwani alziba mianya yote ambayo ilikuwa ikionyesha matumizi ya pesa kwa kutoa misaada na kusema mpka watakapopta faida ndio watakuwa wakitoa misaada. Jobs aliangalia sana katika utengenezaji wa vitu vya kitelnojia vya kuiingizia Apple faida kubwa.

6. Alimdanganya Steve Wozniak. Steve Wozniak ambaye pia ni mwanzilishi mwenza wa Apple alishirikiana na Jobs kutengeneza gemu ya Breakout ambapo mchongo mzima wa kutengeneza gemu hiyo Jobs alilipwa $5,000 lakini akamwambia kuwa amelipwa $700 tu.

7. Hakwenda chuo. Mark Zuckerberg na Bill Gates ni watu wanaojulikana kwa kutohitimu masomo yao chuo. Hivyo hivyo kwa Jobs nae hakuhitimu masomo yake baada ya kujiunga na chuo cha Reed na kuacha baada ya muhula wa kwanza kumalizika.


  • 8. Alikula mboga aina ya samaki tu. Jobs alikuwa aakila samaki tu katika jamii ya mboga na kuwa tofauti na vegetarian kwani wao wanakula maziwa na mayai. Watu wenye kula samaki tu wana 34% pungufu ya kutokufa kutokana na matatizo ya moyo ukilinganisha na watu wanaokula nyama mara kwa mara. Huku wanaokula mboga za majani tu wana 20% pungufu ya kutokufa kutokana na matatizo ya moyo ukilinganisha na watu wanaokula nyama mara kwa mara.

    Mambo ya Kujifunza Toka Kwa Steve Jobs

    1.Kuongoza kwa Vitendo

    Jobs alikuwa mzuri sana katika kubuni teknologia na ku zitangaza lakini alikuwa mtendaji wa mojakwa moja katika kubuni na kutengeneza bidhaa katika kila hatua. Alikuwa kiongozi wa kiufundi na alishiriki katika kila hatua za uzalishaji katika Apples.

    Mojawapo wa mradi mkubwa aliousimamia ni Komputa ya Macintosh. Yeye mwenyewe alishiriki katika kubuni na utengenezaji wake ikiwemo kuitangaza.

    Jobs hakuwa anasubiria ripoti mwisho wa siku au wiki,alikuwa akienda katika kila benchi la mfanyakazi na kujua kinachoendelea pamoja na kujua changamoto na kushiriki kwa kutoa ushauri wake au maelekezo.


    2. Mwanamasoko na Mtangazaji wa Bidhaa-Mtazamo wa Mtumiaji


    Jobs alikuwa ni mwanamasoko mzuri wa bidhaa za kampuni yake,alikuwa mtu maalumu ambaye anatumiwa kufungua bidhaa mpya ikitoka kabla ya kwenda kwa watumiaji. Mikutano yake ya ufunguzi wa bidhaa mpya imekuwa ikihudhuriwa na mamia ya watu. Unaweza ukaona baadhi ya mikutano hii katika mtandao wa youtube.

    i. Ufunguzi wa iPhone 2007



    ii. Ufunguzi wa iPad 2010


    iii. Ufunguzi wa iPod Touch 2010



    Alikuwa anatumia yeye mwenyewe kwanza kuona kama ataipenda ndipo iende sokoni. Vinginevyo inarudishwa kiwandani kwa maboresho zaidi. Alisema “Ukitaka kuuza wazo,bidhaa au huduma,jiweke mwenyewe katika nafasi ya mtumiaji”

    Alikuwa mtu anayependa vitu vizuri na vyemye ubora na kwa tabia hii bidhaa za Apple zimekuwa bora sana katika soko hadi leo hii ukilinganisha na washindani wake ambao wengi wanaiga toka kwao.

    3. Uongozi Bora wa Timu: Ajiri na Kufukuza Kazi – “Ajiri Waliobora Tu “

    Steve Jobs alikuwa anaamini kuwa anauwezo mkubwa yeye mwenyewe na alikuwa anaamini mambo makubwa yatafanywa na watu wenye mtazamo wa mbali wenye kupenda wanachokifanya na wenye vipaji.

    Alikuwa mjengaji mzuri wa timu ya kazi. Aliamini ili kuendelea katika kampuni ni lazima na muhimu kuwa na timu thabiti. Alijiita Timu A na alikuwa na usemi unaoenda “Watu wa Timu A huajiri watu wa timu A,Watu wa timu B huajiri watu wa team C”. Kwa kuwa alijiona mwenyewe kama mtu wa timu A hivyo aliajiri watu wenye uwezo wa juu na kuwaweka katika timu yake. Alifukuza yeyote ambaye alionekana kutojiamini ,mvunjaji moyo kwa wenzake na asiyeenda sambamba na dira ya kampuni au idara anayofanyia kazi.

    Maendeleo mengi katika sehemu ya kazi yanarudishwa nyuma kwa ugumu wa viongozi kutowawajibisha watu wasio na sifa na wasio na uwezo wa kupeleka kampuni mbele,kwa mtazamo wa Steve hawa ni vikwazo na ni muhimu kuondolewa mara moja kwa mustakabali mzuri wa kampuni.


    4. Mwona Mbali na Mbunifu


Kama kiongozi mbunifu alikuwa mwona mbali,na anaonekana toka mwanzoni mwa kazi yake wakati akianzisha kampuni pamoja na rafiki yake Woziniak. Steve alikuwa akisema kuwa “tutengeneze bidhaa rahisi kutumia na bora ambayo itabadilisha ulimwengu” na alifanya kazi kila siku katika kuhakikisha hilo linatimia

Siri kubwa ya mafanikio ya Apples and Steve ipo katika ubunifu. Jobs ni alikuwa mzuri sana katika ubunifu. Jicho la mtumiaji ambalo alikuwa nalo lilisaidia sana katika kufanikisha kazi za ubunifu. Karibu kila mwaka Apples wamekuwa wakitoa bidhaa mpya na inayopendwa na watu.

Ukiangalia sana utaona kuwa hakuna mabadiliko makubwa sana bali nyongeza au maboresho machache yanayotokana na bidhaa ya nyuma na hili ndilo jambo linalotakiwa leo katika makampuni mengine yakiwemo yetu nchini mwetu.

Uboreshaji wa vitu ambavyo tayari tunavyo. Idara za Maboresho na Ubunifu zinahitajika sana katika makambuni uyetu na biashara tunazofanya-Vitu vidogo ambavyo vinaleta mabadiliko makubwa.

Angalia tabia za watumiaji,na angalia nini unaweza kubadilisha katika huduma au bidhaa unayozalisha na kuuza ambayo italeta mabadiliko katika soko-Hii ni siri ya mafanikio ya biashara

5. Fanya Unachokipenda Ili Kufanikiwa

Jobs alikuwa na mapenzi makubwa na teknolojia na hili lilimfanya mwenyewe kuwa mtumiaji wa kwanza. Kama hakuipenda bidhaa basi ilitakiwa kurekebishwa.

Hata katika usaili wa wafanyakazi na kuchagua timu ukiachia akili na ubunifu alikuwa anaangalia sana mapenzi yake katika bidhaa.

Kwasababu kunamsukumo mkubwa wa mafanikio zaidi wa kupata fedha unaokufanya uendelee kufanya unachokifanya kwa mapenzi ili kufikia mafanikio. Steve anasema “Kama unafanya kitu usichokipenda basi ukiache na endelea kutafuta unachokipenda mpaka ukipate”

KWA KIFUPI

Jobs alikuwa Kiongozi aliyefanikiwa sana,Mbunifu,Mzungumzaji mwenye kalama,mwenye mapenzi na kazi yake na aliyeamini katika kazi ya timu. Haya ni mambo ya kujifunza toka kwa Steve Jobs.

Steve Jobs alizalimwa mwezi Februari 24, mwaka 1955 huko California Marekani na kufariki tarehe 5 mwezi Oktoba mwaka 2011.
 
Back
Top Bottom