Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 52,197
- 162,728
Kuna mambo katika jamii yetu ya kitanzania huwa yananishangaza sana, baadhi ya mambo hayo ni haya:
1.Mtu anakwambia hafuatilii siasa, ila ukifika wakati wa uchaguzi, anaenda kupiga kura!
2.Miaka 60 ya uhuru bado tunakimbiza mwenge!
3.Mtu(mimi mwenyewe nikiwemo), ana bachelor, masters, PhD au ni Professor, lakini akiandika, hajui wapi pa kuweka nukta, comma, semicolon, hyphen, n.k(Lissu ni msomi na mwanasiasa pekee ambae maandiko yake yanaonyesha yuko vizuri kwenye punctuation).
4.Graduate akiambiwa afanye presentation, basi anaweza kuugua,na kama ni kazini, anaweza asifike siku hiyo!
5.Mtu ni darasa la saba au form iv, lakini anaendesha biashara kwa mafanikio kuliko graduate aliesomea mambo ya biashara!
6. Watu wamekaa kundi/kikundi kwenye meza, mkeka, n.k, halafu mmoja anapigya chafya na hakuna anaeshituka(kuziba pua, mdomo au uso) kama hakuna kilichotokea (kabla na hata baada ya ujio wa covid)!
7. Watu wako mezani wanakula au wanapatwa vinywaji, wanaongea huku wanarusha mate na hakuna anaeshituka!
8. Miaka 60 ya uhuru kila siku unalalamika(mfano wazee) huku kila mwaka wa uchaguzi, kuanzia mgombea uraisi mpaka udiwani, unachagua kutoka chama kile kile!
9.Unatoa sadaka kubwabwa kwenye nyumba ya Ibada na hata kusaidia yatima, lakini ndugu zako na pengine hata wazazi wako umewatupa!
10.Kuna watu mpaka leo wanaamini nchi yetu ina amani kumbe ina utulivu tu.
11.Mtu anatoka chooni analipta bomba la maji kama halioni.
12. Mtu anaingia bafuni na mswaki na ndoo ya maji ya kuogea, huku maji hayo ya kwenye ndoo, ndio hayo hayo ya kupigia mswaki!
13.Mtu mzima(hasa wadada-tena warembo) wanalala na ndoo au vidumu vya kukojolea usiku huku nyumba anayoishi ni salama na ina uzio!
Wabongo wamenishinda!