Mambo ya kabla ya uwepo wa binadamu yalijulikanaje?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,348
Reaction score
26,145
Vitabu vitakatifu vya dini pamoja na maandiko mengineyo yanajaribu kusimulia jinsi Mungu alivyoumba malaika, binaadamu na viumbe vinginevyo.

Vitabu hivyo vinaanzia masimulizi hata kabla ya uwepo wa binadamu katika dunia hii tunayoishi. Sina tatizo juu ya mambo yaliyotokea kuanzia kuwepo kwa binadamu hapa duniani kwakuwa mambo hayo yalirithishwa kwa masimulizi na kadhalika.

Je, mambo yaliyotokea kabla ya uwepo wa binadamu hapa duniani yalijulikanaje?
 
Safi sana ni swali zuri na pia tuangalie na hili langu...je kabla ya hizi dini mbili watu walikua na imani ipi maana hizi dini si asili yake Africa na iweje maandiko yote yahusu uarabuni na ulaya pekee jee Africa kulikua hakuna imani au watu wanaotaka kujua hayo maandiko mpaka yahusu hao waarabu na wazungu???
 
hizi dini zililetwa africa kwa lengo la kuchukua rasilimali zetu....waarabu walikuja na uislam wakafanikiwa kufanya slave trade...ukristu uliletwa africa na wazungu kwa ajili ya colonialism.....kabla ya hizi dini tulikuwa tunaabudu chini ya mlima na kwenye miti.....na tunapata baraka..mfano babu zetu waliomba mvua na ikanyesha....ila saa hv mwee............na ambao bado wanaamini ktk mizimu mambo yao kiuchumi yako vizuri .....hebu jiulize kwann wachagga kila mwenzi wa12 huja kufanya hijja ....
 
Kabla ya utambulisho wa dini hizi mbili kubwa Afrika, mababu zetu walikuwa wakiamini katika mizimu. Mzimu ni yule mtu aliyekufa kitambo na katika uhai wake alifanya mambo makubwa au exceptional things katika jamii yake kwahiyo anapofariki ile jamii au ukoo inakuwa inaendelea kumtambua na kumuomba mambo mbali mbali wakiamini anawasaidi
 
hizi dini zililetwa africa kwa lengo la kuchukua rasilimali zetu....waarabu walikuja na uislam wakafanikiwa kufanya slave trade...ukristu uliletwa africa na wazungu kwa ajili ya colonialism.....kabla ya hizi dini tulikuwa tunaabudu chini ya mlima na kwenye miti.....na tunapata baraka..mfano babu zetu waliomba mvua na ikanyesha....ila saa hv mwee............na ambao bado wanaamini ktk mizimu mambo yao kiuchumi yako vizuri .....hebu jiulize kwann wachagga kila mwenzi wa12 huja kufanya hijja ....

Dyyuuu labda ni kweli
 
Mbona hata sasa kuna watu wana dini halafu pia ni wachawi,labda uulize dini ni nini na uchawi ni nini.
 
Safi sana ni swali zuri na pia tuangalie na hili langu...je kabla ya hizi dini mbili watu walikua na imani ipi maana hizi dini si asili yake Africa na iweje maandiko yote yahusu uarabuni na ulaya pekee jee Africa kulikua hakuna imani au watu wanaotaka kujua hayo maandiko mpaka yahusu hao waarabu na wazungu???

Sijawahi kusikia dini hata moja yenye asili ya afrika,mi mwenyewe nahitaji kusikia kuhusu hizo dini za africa maana mie najua kulikuwa na Imani tu mbalimbali.
 
We mpuuzi kweli we! Imani ni nini na Dini ni nini?
 
Ngoja nichangie kidogo.

Kama utakuwa ni mfwatiliaji wa mambo..vitabu vya dini viliandikwa kwa kupitia mitume..ambao kiimani walikuwa wanaongea na Mungu..sasa hilo swali ulilouliza hata wao pia wanaweza kuwa waliliuliza na majibu yake ndio hayo uliyoyaona kwenye vitabu.

2.Kama vitabu ingekuwa ni uzushi mtupu..basi mpaka leo hii watu wangeweza ku critisize facts zilizopo kwenye kitabu.

3. Wanasayansi na ubishi wao huwa wanafika mahali wanasema kuna nguvu iliyo kubwa somewhere ambayo ina control universe..na wanaogopa kusema kuna Mungu kwa kuwa sayansi inataka Proof.

4. Endelea kudadisi na kujiuliza maswali mengi mwishoni utafikia kipengele utajua kuna nguvu kubwa mahali..na hiyo Nguvu ni Mungu..majina ni mengi..hata hiyo mnayoita mizimu ilikuwa ni namna ya kutambua kuna Mungu.

Nawasilisha kwa mjadala zaidi
 
Afrika kulikuwa hamna dini. Wazee waliamini mizimu, waliamini miti, waliamini milima, waliamini wazee wao waliotangulia wanawalinda. Kuna wengine waliamini jua na hata moto.

Soma kitabu cha Chinua Achebe, Things Fall Apart, ameeleza vizuri Maisha ya kijiji cha Kiafrika kabla na baada ya dini / Wakoloni kuja Afrika.

Baadhi ya Wamarekani weusi pia wanaamini " Kwanzaa" badala ya Krisimasi. Profesa wao alikuja Afrika na kuona wanakijiji wanatoa mazao kwa mizimu yao ili wabarikiwe tena msimu mwingine. Profesa akawaambia Wamarekani wenzake aliporudi kuwa washerehekee mila zao ( kama vile Afrika ni nchi moja) na leo wanaita Kwanzaa Day. Alitumia lugha ya Kiswahili kuwaambia wenzake washeherekee umoja na upendo wao, nia na imani kuendeleza utamaduni na jamii yao. Kwanzaa imetoka katika zao la "kwanza" la wanakijiji. Kwa kifupi amejitungia sikukuu na kuweka mazao katika mkeka ili mradi na wao wawe na sikukuu kama wazungu.

Dini za leo pia zinaambatana na utamaduni wa nchi. Ndio maana Mtu anaamini Mungu na uchawi, kwa kuwa uchawi ni utamaduni wake. Au anaamini Mungu na pia uwezo wa Binadamu mwenzake kuwa na super power za kutibu kitamaduni n.k.

Katika Dini za Kikristo utaona kule Ufilipino , Hispania au Mexico (wakatoliki) wanaamini Yesu na pia sanamu za watakatifu (saints), kitu ambacho hatuoni Afrika sana. Kuna saints wa kubariki biashara, wagonjwa, watoto, kijiji na kadhalika. Ni sherehe kubwa na sijawahi kuziona Katika jumuiya ya Kikristo Tanzania. Wananchi wanakimbiza masanamu ya watakatifu wao barabarani kwa sherehe kubwa.

Pia katika nchi za kitajiri za ulaya na marekani, utamaduni wao unawaruhusi watu wa jinsia Moja kuoana kanisani. Vitu hivi vinapingwa Afrika kwa kuwa utamaduni wetu ni tofauti. Sina uhakika kama kuna mapadri wa kike Tanzania kama ulaya.

Katika dini ya Kiislamu pia dini na utamaduni upo vile vile. Kuna mashehe wanajifanya wana uwezo wa kutibu kuliko daktari. Mimi binafsi nilimwona mmoja akisoma Quran tukufu huku akitema mate Katika glasi. Akamwambia mgonjwa anywe hayo mate yamsaidia kutibika. Mwengine atasema ni dawa, mimi nilifikiri itampa madhara zaidi mgonjwa kama sheikh ana TB au magonjwa mingine ya kuambukiza. Pia kuna wale wa dini zote wanawaua wazee au zeruzeru kwa sababu za kichawi.

Pia kuna tofauti ya kufuata dini kutokana na desturi ya wananchi. Kuna nchi kama Indonesia ambapo pia wana tabia ya kuomba kwa wazee wao na mizimu , mazao bora. Wananchi wao wengi ni waislamu lakini wanawake wengi hawavai baibui na wamesoma sana na wako huru kimawazo, kimaisha na kimapenzi. Haya Maisha katika nchi yenye waislamu wengi kuliko wote duniani ( milioni 250) ni tofauti na nchi za kiarabu kama Saudi Arabia ambapo mwanamke hana Haki sawa na mwanamme na haruhusiwi kuendesha gari wala kutoka bila baibui au kusafiri peke Yake. Hapo dini imeambatana na utamaduni wa kibedui.

Nawasilisha.
 
Ngoja nichangie kidogo.

Kama utakuwa ni mfwatiliaji wa mambo..vitabu vya dini viliandikwa kwa kupitia mitume..ambao kiimani walikuwa wanaongea na Mungu..sasa hilo swali ulilouliza hata wao pia wanaweza kuwa waliliuliza na majibu yake ndio hayo uliyoyaona kwenye vitabu.

2.Kama vitabu ingekuwa ni uzushi mtupu..basi mpaka leo hii watu wangeweza ku critisize facts zilizopo kwenye kitabu.

3. Wanasayansi na ubishi wao huwa wanafika mahali wanasema kuna nguvu iliyo kubwa somewhere ambayo ina control universe..na wanaogopa kusema kuna Mungu kwa kuwa sayansi inataka Proof.

4. Endelea kudadisi na kujiuliza maswali mengi mwishoni utafikia kipengele utajua kuna nguvu kubwa mahali..na hiyo Nguvu ni Mungu..majina ni mengi..hata hiyo mnayoita mizimu ilikuwa ni namna ya kutambua kuna Mungu.

Nawasilisha kwa mjadala zaidi

Nani kakwambia watu wameshindwa ku criticise vitabu hivi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom