Mambo ya FDLR na Rwanda

Mambo ya FDLR na Rwanda

jMali

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Posts
8,412
Reaction score
5,013
Kunaonekana kusitasita kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua baada ya deadline ya kuweka silaha chini kupita, badala ya FDLR kupigwa kama walivyopigwa M23 na wengineo, SADC imeamua kukaa kikao kingine kujadili hatua itakayochukuliwa. Kwa nini FDLR haipigwi moja kwa moja kama M23 kwa kukaidi deadline?

Ni vizuri tukaangalia kwa kina FDLR ni nini (kwa maneno yao wenyewe sio maneno ya Rwanda) na nini kinawatofautisha na vikundi vingine vya waasi nchini DRC.

UASI WA FDLR:
Waasi by definition ni watu wanaoipinga serikali halali kwa silaha. M23 ni waasi kwa kuwa serikali ya kabila ni halali, na M23 ni kundi la askari wa kitutsi toka jeshi la wananchi wa DRC, FARDC, waliojitenga ili kupambana na serikali.

Lakini FDRL ni masalia ya wanajeshi halali wa serikali halali ya Rwanda chini ya juvenal Habyarimana, iliyoangushwa na waasi wa RPA/RPF wakiongozwa na Paul kagame. Wanajeshi hawa walikimbilia DRC baada ya kuzidiwa mapambano. Askari hawa kama wanajeshi wa nchi yoyote duniani walikula kiapo cha kuilinda nchi yao na raia wao (all hutus, tutsis, twa) dhidi ya chochote especially maadui kama waasi RPA/RPF wa Paul Kagame.

Sijui kwa nini baadhi ya watu wanaona kama vile FDLR ni wahuni fulani hivi.

Hebu tufikirie mfano: Tanzania tuvamiwe na waasi, serikali ipinduliwe, jeshi letu lipigwe na kukimbilia msumbiji, hivi jenerali mwamunyange akikusanya kikundi cha wanajeshi wake masalia ya JWTZ huko msumbiji, ili kulinda wakimbizi walioko huko dhidi ya mashambulizi ya hawa waasi walioteka nchi, na kufanya jitihada ya kukomboa Tanzania toka kwa wale waasi, ataonekana wa ajabu? si ndivyo kiapo chake kinavyomtaka afanye au ninakosea?

Mwaka 2005 baada ya kuona ukweli kuwa kutokana na hila/pressure za marekani kwa jumuiya ya kimataifa kama vile misaada ya kifedha, silaha na ufundi, paul kagame amekubalika machoni mwa dunia kuwa kiongozi "halali" wa Rwanda, FDLR iliamua kuachana na mapigano ya silaha, kuweka silaha chini na kukazania upande wa kisiasa.

Waliona kuwa haiwezekani kupigana na Rwanda kijeshi tena, sio tu watashindwa bali hata jumuiya ya kimataifa itawakuwa dhidi yao (kama ambavyo hata humu JF wengi walio dhidi ya FDLR hawajui FDLR ni nini, ila kwa vile wanaitwa "waasi" basi ndio hivyo tena....). So FDLR wakaweka silaha chini na kukazania upande wa siasa ili warudi Rwanda.

Paul kagame kwa kujua uhalali wa madai ya FDLR kisiasa, ndipo akamfadhili Laurent Nkunda kupitia vikundi mbali mbali vya "waasi wa kitutsi" toka jeshi la DRC. Hawa kina Nkunda kazi yao kubwa ilikuwa kuwapiga FDLR ambao walishasema hawataki vita! na kinachoshangaza zaidi, FDLR tatizo lao ni Rwanda sio DRC, hawana matatizo na DRC, sasa iweje 'wacongomani' waasi serikali yao halafu wawapige wao FDLR ambao sio adui?

Kingine ambacho hata chizi alikiona ni kuwa viongozi wote wa hawa "waasi wa kitutsi toka jeshi la DRC", WOTE WALIKUWA WANAJESHI WA RPA ILE ILE ILIYOPINDUA SERIKALI HALALI YA RWANDA AMBAYO FDLR WALIKUWA NDIO WANAJESHI! kwa maana nyingine ni kuwa vita ile ile ya 1994 ilikuwa inaendela DRC kwa majina mengine, FAR ya Rwanda sasa ilikuwa FDLR, na waasi wa RPA kina Nkunda ndio hao CNDP, RCD, M23 etc.

Kutokana na hayo, FDLR ikashindwa kuweka silaha chini, kwani kila wakihadaiwa kuweka silaha chini, Rwanda anafanya hila zake wanajikuta ndio kwanza wanapigwa. Mashitaka yaliyopo sasa dhidi ya viongozi wa FDLR yanatokana na wao kuwachapa UN, Rwanda na DRC waliopigana nao miaka ya 2008-2009, pamoja na kwamba wao hawana mpango wa kupigana na yoyote yule.

MADAI YA FDLR:
FDLR kwa jinsi ninavyojua kwanza walikuwa wanapinga uhalali wa kagame kuwa kiongozi wa Rwanda, uhalali wa RPA n.k, kwa sababu kagame alikuwa muasi aliyepindua nchi, hakuchaguliwa kidemokrasia, ingawa baada ya kuingia kibabe akabadili mifumo inayomuwezesha kuwa sasa awe "anachaguliwa kidemokrasia". Kimsingi wanataka yaliyoamuliwa kwenye mazungumzo ya Arusha yatekelezwe.

Baada ya kupindua nchi, kagame alifuta yale maazimio na kufanya anavyotaka yeye akitumia kisingizio cha kuzuia "genocide against tutsis". Nchi zisizo na unafiki kama Tanzania tunajua kuwa kulikuwa na vita vya miaka minne toka 1990 mpaka 1994 tulipoamua kuweka mazungumzo ili kuvimaliza, lakini kagame anataka genocide ya siku 100 iwe ndio tukio pekee linalomtambulisha yeye nchini rwanda na sio uasi wake.

MADAI YA RWANDA DHIDI YA FDLR:
Rwanda inadai kuwa FDLR ni wauaji wa kimbari. Cha kushangaza haina mashitaka yoyote dhidi ya hao wauaji wa kimbari ambao ni wanachama wa FDLR. FDLR imeundwa mwaka 2000, miaka sita baada ya mauaji ya kimbari ya 1994. kwa nini toka siku zote hizo hawakuwa na orodha ya hao wauaji? Ilitakiwa waseme "fulani na fulani" tulikuwa tunawatafuta toka 1994 sasa wako FDLR. Lakini hawana hilo.

Rwanda vile vile haina tatizo lolote la wanachama wa FDLR kurudi Rwanda endapo tu wataacha kuwa wanachama wa FDLR. In fact Rwanda imeweka programu maalum kwa ajili ya wanachama wa FDLR wanaotaka kuasi chama chao na kurudi Rwanda, watakaporudi watapewa viwanja, nyumba, mafunzo ya ujasiriamali, fedha za kuanzia maisha etc, yote hayo mwananachama atayapata akiachana na FDLR na kukubali propaganda zote za serikali ya kagame. Kwa viongozi wakubwa wa FDLR ndio neema zaidi.

Mwanzilishi wa FDLR, na askari wa zamani wa jeshi la Habyarimana, Paul rwakarabije baada ya kusaliti FDLR na kurudi Rwanda, leo hii ni mkuu wa magereza wa Rwanda! Hivi FDLR inawezaje kuwa kundi la interahamwe na wauaji wa kimbari halafu muanzilishi wake akawa sio tu hana hatia bali anafaa kupewa cheo serikalini?

Wanachama wengi wa FDLR hususani vijana ambao walizaliwa DRC baada ya 1994 wamerudi Rwanda na kufaidi hizo neema zote, lakini wengine waliobaki DRC wenye umri wa kukumbuka nadhani wameshindwa kusaliti nafsi zao. Watakubalije kupewa nyumba na shamba halafu sasa waseme kuwa wazazi na ndugu zao waliouawa na kagame na kuwafanya wakimbilie DRC in the first place walikuwa ni "interahamwe" tu wasiopaswa kukumbukwa (kama alivyowakumbuka victoire ingabire), wakati wao wenyewe wanakumbuka walivyokimbia risasi za kagame kwa neema ya mungu wakiwa na miaka 10? Ni vigumu kwa mwananchama wa FDLR kurudi Rwanda chini ya kagame wakati bado sababu iliyomfanya amkimbie huyo kagame iko pale pale.

Sasa iweje FDLR akirudi Rwanda kwa sharti la kuachana na FDLR apewe nyumba na shamba, lakini FDLR huyo huyo akiwa DRC, ameweka silaha chini anataka mazungumzo ya kisiasa, aambiwe yeye ni interahamwe, na apigwe kijeshi?

UGUMU WA KUIPIGA FDLR:
Ugumu unatokana na hili: FDLR hawapigani! Ni vigumu kwa jumuiya ya kimataifa kama SADC, kuwapiga watu ambao hawapigani. M23 na vikundi vingine vilikuwa vinapigana na serikali na mamlaka zozote ambazo zingewapinga hivyo deadlines ziwepo au zisiwepo wao walikuwa wanafanya mashambulizi hivyo walitakiwa kupigwa.

Kwa upande wa FDLR, wao hawapigani na yoyote yule, hizo silaha zao zilikuwa ni kwa ajili ya kujilinda na mashambulizi ya Rwanda na baadae kwa kiasi fulani DRC ambao walishirikana na Rwanda kuwapiga, na sio vinginevyo. FDLR sio aggressive force toka mwaka 2005. Nimemsikia msemaji wa FDLR akizungumza na ITV wiki iliyopita akisema "kama wanataka kuja kutuua waje tu".

Leo hii majeshi yakienda kule vijijini yatasema yanapigana na nani?
Pili, mataifa yasiyo na unafiki kama Tanzania yanajua kuwa FDLR wana uhalali katika madai yao, hivyo morally hawawezi kukubali FDLR warudishwe kinguvu Rwanda kana kwamba all is now well. Kulikuwa na sababu ya wahutu kukimbia majeshi ya kagame then, na sababu hizo hazijatatuliwa kwa sasa. Ndio maana wenye akili wakasema silaha zikae chini watu waongee. Lakini wasio na akili ndio kwanza wakatishia kumpiga hata aliyetoa wazo hilo!

Ingawa nategemea kuna watu watanipinga katika hili :yell:, lakini FDLR kwa kiasi fulani ni kama ANC ya afrika kusini enzi zile za kupigana na makaburu. ANC yenye silaha na wanajeshi ilikuwa nje ya afrika kusini ikiongozwa na watu kama Nelson Mandela, kina Mbeki n.k ambao walikuwa na kambi zao mpaka huku Tanzania, lakini kimsingi watu wote weusi ndani ya afrika kusini walikuwa wanaunga mkono ANC.

Lakini kutokana na hali ilivyokuwa hawakuweza kujipambanua kuwa na wao ni ANC wakiwa ndani ya afrika kusini, kwa sababu makaburu wangewapiga. "jumuiya ya kimataifa" kama kawaida ikiongozwa na marekani iliweka ANC chini ya definition ya "kikundi cha magaidi", Nelson Mandela aliondolewa kwenye orodha ya magaidi nchini marekani mwaka 2008!, mpaka 2013 bado mpigania uhuru mashuhuri wa ANC, komredi Tokyo sexwale alikamatwa Airport kwa vile jina lake bado lilikuwamo kwenye "orodha ya magaidi wa ANC"!

Katika hali hiyo hiyo, FDLR yenye silaha na inayojulikana ndio iko nje ya Rwanda, DRC, ulaya n.k na kama kawaida imepachikwa nembo ya "negative force", na baadhi ya viongozi wake wana mashitaka mbalimbali. Lakini kama ilivyokuwa kwa ANC, ndani ya Rwanda majority ya watu ni FDLR ingawa ni "mabubu" kama ambavyo ANC ndani ya afrika kusini walikuwa mabubu. FDLR ni kubwa zaidi ndani ya Rwanda kuliko ilivyo DRC. Ndio maana hata watutsi wanaokwenda kinyume na kagame wanashitakiwa kwa kujiunga na FDLR, FDLR ile ile ambayo supposedly ndio iliyowaua wao kwenye mauaji ya kimbari!

UNAFIKI:
Kwa unafiki marekani na wenzie walishinikiza DRC iongee na M23 kule Uganda (of all places!), wakijua fika kuwa M23 hawakuwa na uhalali wowote ule wa kuishinikiza DRC, lengo la M23 lilikuwa ku-destabilize DRC kwa manufaa ya Rwanda. Cha ajabu marekani hao hao, uingereza hao hao walisimamisha misaada Rwanda wakishinikiza Rwanda iachane na M23, lakini hao hao mbona hawashinikizi mazungumzo kati ya FDRL na Rwanda kama walivyofanya kwa M23?, badala yake wanataka FDLR wapigwe tena ikibidi hata kwa makomandoo toka marekani! Kabla M23 hajapigwa aliitwa kampala, akaleta hoja zake mezani zikawa zinajadiliwa kifungu mpaka kifungu, lakini shida yake ikawa wakati mazungumzo yanaendelea na yeye huku anaendelea na vita anasogea sogea ndani ya DRC, ndipo DRC ikaona huu ujinga tukawachapa. Lakini kwa upande wa FDLR na Rwanda hilo halijatokea badala yake wanatakiwa kupigwa tu, why?

Tuzingatie yafuatayo:

  • Mahakama ya ICTR ilishurutishwa na marekani kusitisha mashtaka dhidi ya kagame na kundi lake la RPA. Carla del ponte muendesha mashtaka, alifukuzwa kazi mara moja pale alipotaka kumshitaki kagame, na muendesha mashtaka aliyefuatia alikalia faili hili mpaka leo hii ICTR imefungwa!
  • kagame anashitakiwa katika mahakama za ufaransa, spain na hata marekani kwenyewe kesi ilizuiwa kwa sababu ya sheria inayozuia marais kushitakiwa marekani, vinginevyo kagame anayo kesi mpaka marekani! kwa kesi hizi hizi za mauaji ya 1994.
  • Ripoti za UN zimeweka wazi kuwa kagame na serikali yake wamefanya "genocide against hutus" huko DRC. ripoti hiyo "UN mapping report" imekaliwa na "jumuiya ya kimataifa" (marekani). Haya mauaji ambayo UN wenyewe wanasema ni "genocide against hutus" ndio yanayotengeneza FDLR! Sasa iweje FDLR warudishwe Rwanda bila mazungumzo yoyote yale?

Kwa upande wa pili:

  • ICTR haijawahi kumshitaki kiongozi yoyote yule wa FDLR kwa mauaji ya kimbari. Hawa FDLR wanaitwa "interahamwe" kwa vigezo vya mahakama gani? Na kama mwanzilishi wa FDLR yenyewe kapewa ukuu wa magereza Rwanda hawa kweli ni wauaji au wanasiasa wa upinzani?
  • Kule ICC nako mashtaka yote dhidi ya viongozi wa FDLR yalifeli wakaachiwa huru, na walivyoachiwa mahakama ya ICC ilisema hivi "no case to answer". Hivi sasa mashtaka yaliyoko dhidi ya viongozi wa FDLR ni kutokana na rufaa ambayo kagame alilazimisha ICC waifungue, ili in exchange awape Bosco Ntaganda. Na bado kagame anamhifadhi Laurent Nkunda ambaye anatakiwa ICC.

Mazungumzo yalifanikiwa kuleta amani South Africa na leo wanaishi kama watu wamoja, sioni kwa nini hilo lisiwezekane Rwanda. Naunga mkono msimamo wa Tanzania wa mazungumzo badala ya vita kwenye suala la FDLR vs Rwanda.

Kuna challenge nyingi sana kwenye National Building. Both external and internal especially kwenye nchi ya Rwanda RPF waliwaondoa hao the so called freedom fighters according Jmali and Company.

Kuna madhara ukimnyang'anya MTU ugali mdomoni. Ukaenda kumuacha msituni ambapo hana tena support aliyokuwa kaizoea. Lazima atafute njia ya kutoka tena apate ile support yake ya zamani.

Na FDLR inatumiwa kwa maslahi ya mda mchache na serikali ya Tanzania baada ya hapo akija President mwingine ambaye sio Membe ofkoz. Nyimbo za kuwaonea FDLR huruma hutozisikia tena. Na wakina Jmali and co ndo mwisho wao tena.

Wale interahamwe waliokuwa wana relax Kenya na kula bata sasa ivi kwisha habari yao. Hata hapa this is the year whereby all genocide symphathisers who are hiding in magomeni and several other hideouts, time is clocking down and its getting dark.

Tunajenga nchi ya uchumi Wa kati(middle income economy). That's the goal and we shall achieve that no matter the setback.

There is nothing we are facing which is so new.

We have been there done that.

WE CALL THEM CHALLENGES OF NATIONAL BUILDING.
 
jMali
1:M23 ni kundi la askari wa kitutsi toka jeshi la wananchi wa DRC, FARDC, waliojitenga ili kupambana na serikali.😛oa😛oa
2:FDRL ni masalia ya wanajeshi halali wa serikali halali ya Rwanda chini ya juvenal Habyarimana;
(uhalali as per your description does not apply to Habyarimana kumbuka nayeye aliipindua serikali halali ya Kayibanda, kwanini iwe halali kwake ila yeye akipinduliwa isiwe halali?? hahah
3.Rwanda vile vile haina tatizo lolote la wanachama wa FDLR kurudi Rwanda endapo tu wataacha kuwa wanachama wa FDLR. In fact Rwanda imeweka programu maalum kwa ajili ya wanachama wa FDLR wanaotaka kuasi chama chao na kurudi Rwanda, watakaporudi watapewa viwanja, nyumba, mafunzo ya ujasiriamali, fedha za kuanzia maisha etc,😛oa😛oa
4.FDLR kwa kiasi fulani ni kama ANC; duu! kwa hiyo Bagosora anastahili kupewa heshima kama Desmond Tutu hivi hahah!

Apart from your Ideology ambayo inajulikana, lakini nakubaliana nawewe on some point, kweli kuipiga FDRL sio kazi rahisi as it was for M23.
FDRL wako mapolini, wengi wanaishi na familia zao they are not organized, Waziri wa mambo ya nje Rwanda, juzijuzi alikiri kwamba FDRL does not pose military threat to Rwanda; ila tatizo ni Genocide propaganda wanazoeneza kwenye maeneo haya wakitumia njia mbali mbali ikiwemo mitandao ya kijamii kama jamiiforums;We know this is one of their strategy and they been recruiting people to work for them;
It is the duty of Rwandan government to make sure that innocent civilians ambao wameshikiliwa matekwa na FDRL wanapata nafasi ya kurudi kwao.
Kumbuka kuna watoto wadogo wasiojuwa lolote kuhusu siasa, unadhani nimaisha gani yanayowasubiri hapo mbele bila elimu, bila matibabu n.k
Ingekuwa bora kama kweli FDRL wanampango wakuwa kikundi cha siasa, warudi Rwanda then siasa waifanyie nchini mwao.
Kama kweli wana program nzuri dhidi ya nchi then wananchi watawachagua:
Kumbuka hapa tunaongelea kundi la watu wasiozidi 4000, ambao hawafiki hata 1% of Rwandese population so it is hard kufuata masharti yao, uache yale ya 12 millions zilizo kuchagua.
Lastly, jamani DRC haiwataki,juzijuzi wale waliohamishiwa Kisangani, Polisi ilibidi iingile kati wananchi waliingia barabarani kuonyesha hasira zao, hawapendwi, jamaa wanaroho mbaya na wamefanya maovu mengi tu.
 
Last edited by a moderator:
Huyu jmall anaonekana ni FDRL, kwanini asiwashauri hao jamaa zake warudi RWANDA wapatiwe ulinzi na umoja wa mataifa?kama kuna genociders waombe kuwepo na tume ya maridhiano kama ile ya south africa chini ya Desmond tutu, wakiri makosa na kuomba msamaha ili maisha yaendelee.tatizo ni kwamba wanaoteseka porini ni watoto ambao hawajui madhambi yaliyofanywa na baba zao
 
Usishangae hutapewa like na kina Pro PK...hapo kwenye bold ndio wasipopataka...
 
jMali

mimi sina haja yakusoma huu utumbo kwani umevuruga hapo mwanzoni,eti FDLR ni masalia ya jeshi halali la rwanda!kama ni hivyo kati ya jeshi lililo jiengua kutoka jeshi halali la congo kama M23 na FDLR iliyofukuzwa kutoka rwanda kutokana na mauaji waliyofanyia watusi nilipi halali hapo???
 
What if, you stay within your borders and build your so-called middle economy without trying to anhiliate anyone who tries to go against anything you believe in?

In Kenya, Tanzania and even Uganda , there are opposition groups cursing, asking all kinds of questions and revealing all the dirty tricks of their governments without facing persecution. RENAMO had no legitimate reasons to go to war, especially soon after achieving independence. They committed all kinds of crimes which were reciprocated by FRELIMO honestly. Taliban and Pakistan/US, FARC/Colombia etc ...They all sat down and talk. Why not Rwanda??

FDLR is just an excuse, because if anything, Rwandese in diaspora are way too vocal against Kagame. Contrary to your belief, time seems to be your worst enemy.

FDLR will be disarmed, and the international community will soon scream "Checkmate!" .... What are you gonna do?
 
Huyu jmall anaonekana ni FDRL, kwanini asiwashauri hao jamaa zake warudi RWANDA wapatiwe ulinzi na umoja wa mataifa?kama kuna genociders waombe kuwepo na tume ya maridhiano kama ile ya south africa chini ya Desmond tutu, wakiri makosa na kuomba msamaha ili maisha yaendelee.tatizo ni kwamba wanaoteseka porini ni watoto ambao hawajui madhambi yaliyofanywa na baba zao
Hiyo waulize kina PK .... FDLR would love that.
 
Huyu jmall anaonekana ni FDRL, kwanini asiwashauri hao jamaa zake warudi RWANDA wapatiwe ulinzi na umoja wa mataifa?kama kuna genociders waombe kuwepo na tume ya maridhiano kama ile ya south africa chini ya Desmond tutu, wakiri makosa na kuomba msamaha ili maisha yaendelee.tatizo ni kwamba wanaoteseka porini ni watoto ambao hawajui madhambi yaliyofanywa na baba zao

1. Hivi huwezi kujadili kitu bila kupachika watu unyarwanda? huu mwaka mpya jamani badilikeni tujadiliane kwa hoja. SADC nzima nayo ni FDLR?
2. kwa kiasi kikubwa hicho ulichosema ndio exactly FDLR wanataka. wanataka international community iweke vigezo vya wao kurudi nyumbani kama chama cha siasa wakiwa guaranteed usalama wao. sio kama wale wakimbizi ambao warudishwa Rwanda kinguvu chini ya UN halafu baada ya hapo eti "wakapotea"!
kwa upande wa pili hapo kwenye tume ya maridhiano, again, tuko pamoja, ila tatizo ni hapo unaposema kuwa "wakiri makosa na kuomba msamaha". Mbona tayari umeshawahukumu kabla hata ya tume? Una uhakika gani kuwa hawa wakimbizi ndio waliokuwa na matatizo na sio kagame na serikali yake?
Kumbuka FDLR haina hata mtu mmoja aliyeshitakiwa kwenye mahakama ya mauaji ya kimbari ya ICTR, wakati kagame na jeshi lake RPA wana indictments zilizokaliwa! Hivyo hata bila ya tume, kwa mtu yoyote asiye mtutsi mwenye msimamo mkali, watakaotakiwa kuomba msamaha haraka sana ni kagame na RPA bila shaka yoyote, halafu ndio hao FDLR nao wachunguzwe.
 
jMali
1:M23 ni kundi la askari wa kitutsi toka jeshi la wananchi wa DRC, FARDC, waliojitenga ili kupambana na serikali.😛oa😛oa
2:FDRL ni masalia ya wanajeshi halali wa serikali halali ya Rwanda chini ya juvenal Habyarimana;
(uhalali as per your description does not apply to Habyarimana kumbuka nayeye aliipindua serikali halali ya Kayibanda, kwanini iwe halali kwake ila yeye akipinduliwa isiwe halali?? hahah
3.Rwanda vile vile haina tatizo lolote la wanachama wa FDLR kurudi Rwanda endapo tu wataacha kuwa wanachama wa FDLR. In fact Rwanda imeweka programu maalum kwa ajili ya wanachama wa FDLR wanaotaka kuasi chama chao na kurudi Rwanda, watakaporudi watapewa viwanja, nyumba, mafunzo ya ujasiriamali, fedha za kuanzia maisha etc,😛oa😛oa
4.FDLR kwa kiasi fulani ni kama ANC; duu! kwa hiyo Bagosora anastahili kupewa heshima kama Desmond Tutu hivi hahah!

Apart from your Ideology ambayo inajulikana, lakini nakubaliana nawewe on some point, kweli kuipiga FDRL sio kazi rahisi as it was for M23.
FDRL wako mapolini, wengi wanaishi na familia zao they are not organized, Waziri wa mambo ya nje Rwanda, juzijuzi alikiri kwamba FDRL does not pose military threat to Rwanda; ila tatizo ni Genocide propaganda wanazoeneza kwenye maeneo haya wakitumia njia mbali mbali ikiwemo mitandao ya kijamii kama jamiiforums;We know this is one of their strategy and they been recruiting people to work for them;
It is the duty of Rwandan government to make sure that innocent civilians ambao wameshikiliwa matekwa na FDRL wanapata nafasi ya kurudi kwao.
Kumbuka kuna watoto wadogo wasiojuwa lolote kuhusu siasa, unadhani nimaisha gani yanayowasubiri hapo mbele bila elimu, bila matibabu n.k
Ingekuwa bora kama kweli FDRL wanampango wakuwa kikundi cha siasa, warudi Rwanda then siasa waifanyie nchini mwao.
Kama kweli wana program nzuri dhidi ya nchi then wananchi watawachagua:
Kumbuka hapa tunaongelea kundi la watu wasiozidi 4000, ambao hawafiki hata 1% of Rwandese population so it is hard kufuata masharti yao, uache yale ya 12 millions zilizo kuchagua.
Lastly, jamani DRC haiwataki,juzijuzi wale waliohamishiwa Kisangani, Polisi ilibidi iingile kati wananchi waliingia barabarani kuonyesha hasira zao, hawapendwi, jamaa wanaroho mbaya na wamefanya maovu mengi tu.

1. dah leo umenipa like, halafu sehemu nyingine umekubaliana....ama kweli umekua. Inaelekea zile "sumu" zangu anazoongeleaga mchambawima na wewe zimekuingia. happy new year.
2. Mushikiwabo kashasema na wewe umekiri kuwa "FDLR does not pose military threat to rwanda". if that is the case, why does Rwanda advocate dealing with FDLR militarily as opposed to diplomatically as suggested by kikwete? Huoni kuna kujichanganya hapo? if FDLR does not pose military threat to Rwanda, then to whom does it pose so much of a threat mpaka Rwanda itake majeshi ya EAC yawapige?
3. Hakuna wanyarwanda wowote ambao wanashikiliwa mateka na FDLR, that is a lie, and a very stupid one. How many times Rwanda imevamia DRC kwa kigezo cha kuwapiga FDLR? je ni mara ngapi ilirudi na raia wake waliokombolewa mikononi mwa hao FDLR iliyowapiga? Siku zote Rwanda ikienda DRC kinachotokea huwa ni mauaji ya kimbari dhidi ya wahutu, refer to the mapping report. Mauaji ambayo huwa yanafichwa na marekani kutokana na alliance yake na serikali ya kagame. Most of the FDLR now ni vijana wadogo tu, hawawezi kuwa wamewekwa mateka na wazee umri wa kagame. Hao FDLR wanaorudi Rwanda kwa ahadi za nyumba na mashamba wamewezaje kurudi? walitoroka?
4. FDLR wana mpango wa kurudi Rwanda kama chama cha siasa, lakini sio chini ya utawala wa kagame. Siasa gani ambayo watafanya FDLR chini ya kagame? Mfano: hivi wakianza maandamano kudai wauaji wa kibeho massacre wakamatwe itakuwaje? wakifanya maandamano kutaka wahutu wasio na hatia waliokufa mwaka 1994 chini ya RPF watambuliwe na kukumbukwa itakuwaje? wakitaka prosecution ya askari wa RPF waliofanya mauaji dhidi ya wanyarwanda toka mwaka 1990 mpaka 1994 washitakiwe itakuwaje? FDLR haiwezi kurudi kwa conditions za sasa za kisiasa nchini Rwanda. Hiyo ni sawa na wakati ule useme kuwa ANC warudi south africa kufanya siasa chini ya utawala wa botha ambao ulikuwa na siasa za apartheird! Yani ANC iende kinyume na kila kitu wanachosimamia, waamini kuwa watu weusi ni mbwa halafu warudi south africa wakae kwa amani!
5. Mwisho nakubali kuwa baadhi ya wanachama wa FDLR wamefanya uhalifu DRC. Uhalifu huo wa baadhi ya members sio uhalifu wa kundi zima. Kama ambavyo kuwa member wa RPF hakumfanyi mtu automatically kuwa kama kagame au Nyamwasa. Hata mimi ninavyoadvocate wahalifu wa RPF wachukuliwe hatua hatusemi RPF wote mpaka kina Oda gasinzigwa nao ni wauaji.
 
jMali

mimi sina haja yakusoma huu utumbo kwani umevuruga hapo mwanzoni,eti FDLR ni masalia ya jeshi halali la rwanda!kama ni hivyo kati ya jeshi lililo jiengua kutoka jeshi halali la congo kama M23 na FDLR iliyofukuzwa kutoka rwanda kutokana na mauaji waliyofanyia watusi nilipi halali hapo???

1. "FDLR" haikufukuzwa rwanda kutokana na mauaji iliyowafanyia watutsi. Kagame na RPA walikuwa wanapambana kijeshi na serikali halali ya Rwanda toka mwaka 1990 mpaka 1994 Tanzania tulipowaweka pamoja kwa mazungumzo ya amani pale Arusha. Sio kweli kuwa kagame alipindua "FDLR" kwa sababu ya mauaji, alichofanya kagame na RPA ni hitimisho la vita yake ya miaka minne, ndio maana baada ya kuchukua madaraka, alivunjilia mbali makubaliano ya Arusha na kufanya alivyotaka yeye.
2. Sababu ya kuweka FDLR kwenye hizo quotation marks sehemu ya 1 hapo juu ni hii. FDLR ilianzishwa mwaka 2000. FDLR hawakuwapo 1994. Waliofukuzwa ni FAR, kipengele kimojawapo ndani ya FDLR ambao ni wakimbizi wa kihutu. Chanzo cha FDLR ni mauaji ya kimbari dhidi ya wahutu as documented by the UN's mapping report.
 
Hata mimi naunga mkono FDLR irudi Rwanda kwa njia ya mazungumzo.
Kwani kukiwa na mazungumzo baina ya pande zote mbili kuna hasara gani?
Kama wao wenyewe wamekubali kurudi kwa njia ya maelewano, Je kuna ubaya gani kwa upande wa Rwanda?
Na wao pia wana haki ya Kusikilizwa na kurudi Nchini kwao, mbona M23 imeua wengi kule DRC na sote tunatambua kuwa ni Jeshi la Rwanda?
Naungana na Rais Kikwete, Rwanda ikae meza moja na FDLR ili warejee nchini kwao kwa njia ya maelewano na si vita.
Hao FDLR wakirudi kwa njia ya kawaida ambayo Rwanda inataka basi tushuhudie maiti zingine zikitupwa zaidi.
 
Kuna challenge nyingi sana kwenye National Building. Both external and internal especially kwenye nchi ya Rwanda RPF waliwaondoa hao the so called freedom fighters according Jmali and Company.

Kuna madhara ukimnyang'anya MTU ugali mdomoni. Ukaenda kumuacha msituni ambapo hana tena support aliyokuwa kaizoea. Lazima atafute njia ya kutoka tena apate ile support yake ya zamani.

Na FDLR inatumiwa kwa maslahi ya mda mchache na serikali ya Tanzania baada ya hapo akija President mwingine ambaye sio Membe ofkoz. Nyimbo za kuwaonea FDLR huruma hutozisikia tena. Na wakina Jmali and co ndo mwisho wao tena.

Wale interahamwe waliokuwa wana relax Kenya na kula bata sasa ivi kwisha habari yao. Hata hapa this is the year whereby all genocide symphathisers who are hiding in magomeni and several other hideouts, time is clocking down and its getting dark.

Tunajenga nchi ya uchumi Wa kati(middle income economy). That's the goal and we shall achieve that no matter the setback.

There is nothing we are facing which is so new.

We have been there done that.

WE CALL THEM CHALLENGES OF NATIONAL BUILDING.

1. Tanzania ni nchi mojawapo tu ya nchi za SADC. Hivyo sio sawa kudhani kuwa Tanzania peke yake ndio "inatetea" FDLR. Hata rais akiwa ezekiel wenje, bado nchi nyingine za SADC "zitatetea" FDLR.
2. Tanzania haitetei uhalifu wowote ule uwe umefanywa na members wa FDLR au vinginevyo. wewe wataje hao genociders waliojificha magomeni uone kama serikali haitawatoa. FDLR have never commited any genocide against anybody. Kwa nini hakuna member hata mmoja wa FDLR aliyeshitakiwa ICTR iliyoundwa rasmi for genocide crimes, au hata gacaca courts ndani ya rwanda for that? The only genocide associated with FDLR ni ile mentioned by the UN's mapping report which says kagame and his forces committed genocide against hutus in DRC, that means against FDLR members!!!! Hao genociders ndio ambao wanatakiwa washughulikiwe! Kwa nini unawaita FDLR genociders bila ushahidi wowote? Kama FDLR ni genociders how come maelfu wamerudi na hawana kesi, including THE CO-FOUNDER OF FDLR, THE FORMER OVERALL COMMANDER OF FDLR, who also happened to be an ex-FAR General, bwana Rwakarabije who is now MKUU WA MAGEREZA RWANDA? Hiyo propaganda ya FDLR na genocide ni upuuzi ambao umeshashitukiwa siku nyingi.
3. Tanzania wishes you good luck in building that middle income economy you talk about. But you must also remember that having a stable economy requires peace not violent pacification. Take it from a peaceful country where judging by your perfect swahili you must have grown up in.
 
1. dah leo umenipa like, halafu sehemu nyingine umekubaliana....ama kweli umekua. Inaelekea zile "sumu" zangu anazoongeleaga mchambawima na wewe zimekuingia. happy new year.
2. Mushikiwabo kashasema na wewe umekiri kuwa "FDLR does not pose military threat to rwanda". if that is the case, why does Rwanda advocate dealing with FDLR militarily as opposed to diplomatically as suggested by kikwete? Huoni kuna kujichanganya hapo? if FDLR does not pose military threat to Rwanda, then to whom does it pose so much of a threat mpaka Rwanda itake majeshi ya EAC yawapige?
3. Hakuna wanyarwanda wowote ambao wanashikiliwa mateka na FDLR, that is a lie, and a very stupid one. How many times Rwanda imevamia DRC kwa kigezo cha kuwapiga FDLR? je ni mara ngapi ilirudi na raia wake waliokombolewa mikononi mwa hao FDLR iliyowapiga? Siku zote Rwanda ikienda DRC kinachotokea huwa ni mauaji ya kimbari dhidi ya wahutu, refer to the mapping report. Mauaji ambayo huwa yanafichwa na marekani kutokana na alliance yake na serikali ya kagame. Most of the FDLR now ni vijana wadogo tu, hawawezi kuwa wamewekwa mateka na wazee umri wa kagame. Hao FDLR wanaorudi Rwanda kwa ahadi za nyumba na mashamba wamewezaje kurudi? walitoroka?
4. FDLR wana mpango wa kurudi Rwanda kama chama cha siasa, lakini sio chini ya utawala wa kagame. Siasa gani ambayo watafanya FDLR chini ya kagame? Mfano: hivi wakianza maandamano kudai wauaji wa kibeho massacre wakamatwe itakuwaje? wakifanya maandamano kutaka wahutu wasio na hatia waliokufa mwaka 1994 chini ya RPF watambuliwe na kukumbukwa itakuwaje? wakitaka prosecution ya askari wa RPF waliofanya mauaji dhidi ya wanyarwanda toka mwaka 1990 mpaka 1994 washitakiwe itakuwaje? FDLR haiwezi kurudi kwa conditions za sasa za kisiasa nchini Rwanda. Hiyo ni sawa na wakati ule useme kuwa ANC warudi south africa kufanya siasa chini ya utawala wa botha ambao ulikuwa na siasa za apartheird! Yani ANC iende kinyume na kila kitu wanachosimamia, waamini kuwa watu weusi ni mbwa halafu warudi south africa wakae kwa amani!
5. Mwisho nakubali kuwa baadhi ya wanachama wa FDLR wamefanya uhalifu DRC. Uhalifu huo wa baadhi ya members sio uhalifu wa kundi zima. Kama ambavyo kuwa member wa RPF hakumfanyi mtu automatically kuwa kama kagame au Nyamwasa. Hata mimi ninavyoadvocate wahalifu wa RPF wachukuliwe hatua hatusemi RPF wote mpaka kina Oda gasinzigwa nao ni wauaji.
1.Haah!hizo like ni jinsi unavyobadili msimamo kulingana na comments unayotaka kuweka, mara nyingi tu, umekuwa ukiandika kuwa askali wa M23 ni askali wa RDF, surprisingly leo una kuja na clear definition ya M23, kumbe unafanyaga makusud..du?
2.Like ya Pili, again mara nyingi tu umepost kuwa wale wanaorudi wanauawa na serikali ya Rwanda,again surprisingly leo unakubali kuwa wale wanaorudi wanasaidiwa kurudi kwenye maisha ya kawaida.

Hivi inakuwaje kijana wa miaka chini ya ishilini, kazaliwa na kukulia kwenye misitu ya Congo,leo hii hataki kurudi kwao eti mpaka kuwepo na majadiliano, what does he/she know about Rwanda.Nikisema mateka naongelea hao watoto wadogo ambao hawana umri wakupigana, naongelea hao kina mama wajawazito ambao hawana access kwa matibabu.
haki yao iko Rwanda, na Rwanda haijasita kuwakaribisha, are you telling me that they are also there because they are fighting for freedom?
Hawa wapiganaji hawataki kuachana na innocent civilians and they are using them as a shield.
3.FDRL haina nguvu za kijeshi to the extent of overthrowing the government, lakini hate propaganda ndio hatutaki;
Rejea your definition, hawa nimarejea ya askali wa zamani wa Habyarimana, we fought and defeated them, so, they either come and join the government peacefull, otherwise they could have asked for negotiations before when they were still in power.
 
1. Mambo ya DRC ni mambo mtambuka hivyo kulingana na unajadili nini lazima definition zibadilike kulingana na kinachojadiliwa, haimaanishi kuwa M23 kuwa sehemu ya FARDC hawana askari wa RDF ndani yao. Na haimaanishi kuwa Laurent Nkunda kuwa askari wa FARDC hakuwa askari wa RPA. hakuna nilichochanganya hapo.
2. Hapo kwenye hoja yako ya mtoto wa miaka 20, naomba nikujibu kwa mfano mzuri sana:
Paul kagame aliingia uganda akiwa amebebwa mgongoni akiwa na miaka 3, karudi Rwanda ameshika mtutu akiwa na miaka 37. Kwa nini muda wote huo wazazi wake hawakurudi Rwanda bila masharti? Kwani wazazi wa kagame walifukuzwa au waliondoka wenyewe baada ya mapinduzi? Mbona majority ya watutsi have always been in Rwanda, what made them stay in Uganda for all that time? vile vikundi vya tutsi insurgency vilikuwa vinawatumia kina kagame as human shields au? vinawazuia wasirudi kwao for all that time? Mi nadhani hawakurudi kwa sababu whatever it was walichokimbia bado kilikuwapo ndio maana waka-settle uganda.
Na please don't give me that poor excuse kuwa habyarimana alikuwa hataki, habyarimana hakuwa na shida na watutsi kurudi alikuwa na shida na resources za kuwaweka hao watakaorudi. Hata huyu kagame anavyosema FDLR warudi bila masharti, sio kwamba watarudi kule walikokuwa zamani. Nyumba zao, mashamba yao tayari yameshagawiwa siku nyingi tu, hivyo kurudi kwao sio kama vile kuingia toilet, ni lazima RPF wameweka utaratibu, possibly makambi au sio?
3. waliozaliwa DRC ni wakimbizi wa kihutu ambao wazazi wao walikuwa wakiuawa na kagame na majeshi yake kwa visingizio mbalimbali. Watarudi vipi Rwanda kwa kagame yule yule aliyewafanya wao wawe wakimbizi? Kwani wazazi wao walivyokimbilia DRC walikwenda picnik? walikuwa wanakimbia mauaji ya RPF! Mauaji ambayo yako documented hata kwenye ripoti za UN, angalia hata documentary ya BBC (hata kama hutaki) imeonyesha footage ya kambi ya wakimbizi ilivyokuwa imesambaratishwa na RPF nchini DRC, mass graves, etc, hata mdada anayeongea kwenye ile documentary alikuwa mtoto aliyesalimika kwenye mauaji yale. Hivi yule dada unataka arudi Rwanda bila masharti kweli? Impossible!
4. FDLR haina nguvu za kijeshi we all agree on that. Lakini wana nguvu ya kisiasa. Unaweza kuita siasa zao propaganda na mmeziita hivyo kwa muda mrefu lakini hatimaye ukweli umeanza kujulikana sasa kuwa nani anafanya siasa na nani anafanya propaganda. Hebu tusaidie watu wa JF japo propaganda moja tu "negative" inayoenezwa na FDLR, JUST ONE!, popote pale ambapo FDLR ime-advocate mauaji ya watutsi or something like that, please just one...watanzania tumechoka kuambiwa tunatetea interahamwe bila ushahidi wa hao interahamwe kuwa interahamwe. Nyie mnaodai kuwa hamtaki ukabila ndio wa kwanza kuleta ukabila, unaposema "ni askari wa habyarimana, we fought and defeated them", unajipambanua kuwa wewe ni RPA, a tutsi-rebel group, that included Laurent Nkunda, bosco ntaganda, sultani makenga na magaidi wengine wa kitutsi waliojaa damu za wana-afrika mashariki, huoni haya? wakati huo wewe ulikuwa wapi kama sio Tanzania? kwa tanzania kuitisha mazungumzo kati ya "nyinyi" RPA na serikali ya Habyarimana mbona hakumdai Tanzania inaingilia mambo yenu kama mnavyodai sasa?
 
jMali maendeleo ya nchi huletwa na watu ambao ni willing kuiendeleza na a peaceful environment to conduct economic activities and also an environment which attracts foreign investors with enough capital, sijui unavyosema kuwa Hamna peace unamaanisha nn wakati unajua kuwa Kigali and Your country Rwanda is in peace and people move freely and conduct their economic activities. Hizi blah blah za JF sijui FDLR hivi vile hazibadilishi momentum towards creating an economic power house in the great lakes which attracts all its neighbours to come and invest in future whether in education, health and many other economic potentials. It will reach a time when FDLR Won't b relevant according to the future situation. A group has been hiding in bushes for two decades if you take one of its leaders and drop him in the capital Kigali, they will just paralyse bcoz things have changed longtime. Hata wewe najua ukifika Kigali deep inside unasema these guys are doing something. Only that yo mind and heart is still hardened.
 
Last edited by a moderator:
jMali

mimi sina haja yakusoma huu utumbo kwani umevuruga hapo mwanzoni,eti FDLR ni masalia ya jeshi halali la rwanda!kama ni hivyo kati ya jeshi lililo jiengua kutoka jeshi halali la congo kama M23 na FDLR iliyofukuzwa kutoka rwanda kutokana na mauaji waliyofanyia watusi nilipi halali hapo???

Mkuu, nakufananisha na askari aliyeuwa mtuhumiwa kwa risasi na yeye akanyongwa na mahakama...😛eace:
 
3.FDRL haina nguvu za kijeshi to the extent of overthrowing the government, lakini hate propaganda ndio hatutaki
;
Rejea your definition, hawa nimarejea ya askali wa zamani wa Habyarimana, we fought and defeated them, so, they either come and join the government peacefull, otherwise they could have asked for negotiations before when they were still in power.
That's a huge problem. Propaganda zikiwa hazina nafasi nyumbani, huwa zinapigwa ugenini.
Mbona Tanzania tunamkosoa rais openly? Hata South, Kenya, Uganda ....
 
That's a huge problem. Propaganda zikiwa hazina nafasi nyumbani, huwa zinapigwa ugenini.
Mbona Tanzania tunamkosoa rais openly? Hata South, Kenya, Uganda ....
Hapa hujaelewa,am telling you kikianzishwa chama cha Kisiasa kianze kufundisha ni jinsi gani wa chagga wanaonewa na hawapati nafasi kubwa serikalini kama makabila mengine).
Chama hicho kikifundisha ukabila badala ya utanzania,am telling you serikali yoyote itayokuwepo haitaweza kukubali hilo.
Uki critisize sera hapo sawa, ndio maana kuna mfumo wa vyama vingi.
Other wise trying to attract majority using ethnic,religion etc,hakuna serikali yoyote inayoweza kukubali.
 
Back
Top Bottom