Mambo ya Aibu!!

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
951
Kuna mambo binafsi akifanya mwenzangu najisikia noma, aibu na yananikosesha raha kuliko:

Upo sehemu ya starehe. Meza ya karibu nawe kuna wanaume wawili na wanawake mmoja ya wanaume anaonekana pombe zimemlemea anasimama na kuanza kumkumbatia mwanamke wake, anamwacha, anamkumbati wa mwenzie, wenzie wanamtulia, anapiga kelele,anataka kutoa uume wake anasema "kama hamnionyeshi chooni nakojoa hapahapa".. HIVI Kama wewe ni mwanaume unajisikiaje mwenzio anapifanya vituko vya jinsi hii?!

Upo eneo la starehe, meza ya pili wapo wanaume na wanawake, mazungumzo yanaendelea, unasikia mmoja ya wanawake kila kajambi kadogo kakiongelewa anaangua kicheko cha nguvu na kwa sauti ya kushtua kadamnasi.."eheeeee,uuuwiiii, pole weee!" Anafanya hivyo kila dakika na anataka kila mara akicheka agonge viganja na wanaume wote aliokaa nao hapo...kama we ni Mwanamke unajisikiaje?

Au upo baa, meza ya pili kuna wanaume na wanawake, mara mmoja anasimama kwenda chooni, wale waliobakia mmoja wa wanaume anasikika akiwaambia wenzie, "mshikaji huyu limbukekeni sana, leo anazo tumnyeee mpaka atie akili" anamwamasisha mmoja wa wanawake "we Mercy akija jamaa jifanye umempenda huwa limbukeni sana anachanganyikiwa sana kwa ma demu!"...Hunajisikiaje kusikia mwanaume akimfanyia mwenzie mambo kama haya!?
 
Kuepuka kuona na kukutana na aibu hizi kaa nyumbani kwako tu. Maana walevi hawana aibu!
Kinachoshangaza ni kwamba wakati wanaingia wanakuwa kimyaaaaaaaaaa! ngoja apate mbili utaona anaanza kupiga kelele na kucheka kwa nguvu, halafu anaongea mpk unaona koromeo, Loh! kwa kweli Pombe si chai!!
 
inahusu nini hadi nijisikie vibaya hata akitoa haja kubwa ni yeye bana
 
hayo ndio mazungumzo ya bar hakuna mengine
 
Kama upo kwenye kampani ya watu wa namna hiyo, badilika. Tafuta kampani ya watu wenye utu wao wawe wamelewa au hawajalewa.Wapo!
 
utu watu haupimwi kwa kwenda baa au kukaa na mlevi ndio maana maadili ya dini yanakataza pombe
 
mambo ya baani hayo kaka hapo sio restourant cha kufanya ni kujaribu kuwa makini ukiona mtu anazidiwa unamsave mapema asije leta dhahama
 
Si utakuwa na maisha very uncomfortable jamani? Omba Mungu usisikie wanayokusema wewe, utajuuta!
 
Hivi ndio huko kwenye baa huwa yanaendelea haya....kweli tuna safari ndefu!!!
 
Niaibu kweli nakumbuka tulienda harusini kukawa na pombe basi kuna mdada alifakamia pombe usingizi ukamchukua kwenye kiti mara mikojo inamtoka bila kujijua nikashanga inakuwaje mtu hajui kipimo chake kisa ni zabure ndio unataka kumkomoa
alonunua....Aibu tupu..
 
Tatizo watu wengi wanapenda vya bure. Ndiyo maana akipewa offer mwingine hata kama ana dose anaikatisha ilimradi anywe pombe za bure. Jambo la muhimu ni kuwa na control binafsi, ukilewa na kufanya viroja kila mtu akikuona anakunyoshea kidole. Hivyo ni lazima unywe kulingana na uwezo wako au kumudu kinywaji. Zaidi ya hapo utakuwa kiroja kila unapokwenda kwenye starehe na wenzio.
 
Mimi sina marafiki ambao tunapishana tabia, yani siwezi kuwa na rafiki mlevi au asiye jiheshimu mbele za watu :biggrin1:
 
inahusu nini hadi nijisikie vibaya hata akitoa haja kubwa ni yeye bana

Tatizo wamezoea baa za uswazi hata mpira ukichezwa makelele week
Mara moja moja tuwe tunaenda mahotel makubwa makubwa hata goli likifungwa watu tunapiga makofi matatu tu :becky:
Au siyo Smile ?
 
Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu mnatengeneza ulevi na riziki nzuri. Hakika katika hayo ipo Ishara kwa wanao tumia akili. (An-Nahl: 67)
Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa. (Al-Maaida: 90)
Hakika Shet'ani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha? (Al-Maaida: 91)
Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Kilicho chepesi. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake mpate kufikiri-- (Al-Baqara: 219)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…