Mambo unayoweza kuyafanya kwa fedha kiasi cha Laki tano

Dalali Bunju

Member
Feb 10, 2014
44
65
Ameandika MASANJA MKANDAMIZAJI

AKILI YAKO UTAJIRI WAKO:

Lakini , Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji. Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua SIMTANK la lita 5000 ( ndoo 250 za lita 20) ambal inaweza kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila SIMTANK unalouza.

Laki tano hii hii inaweza kulima Ekari 2 za Maharage pale Simanjiro na baada ya Miezi Minne ukavuna si chini ya Million 3 ambazo zitaexpand kilimo chako MARA 6 zaidi ya Mwanzo na Kuexpand Kipato chako mara 6 zaidi ya Mkupuo wa kwanza. Laki Tano hii ina uwezo wa kulima Matikiti Maji Ekari 2 na zikakupa si chini ya Milion 2 na nusu baada ya SIKU 90!

SHIDA NI: Kila mtu anataka akae mjini AONEKANE SAMAKI SAMAKI, aonekane Muvi Mlimani City, Apost akiwa Escape 1, Apige Snapchat akiwa 777 ... Kila mtu anataka aonekane MDARISALAMA. Yuko mjini.

MDADA yupo radhi aishi mjini kwa kuuza mwili wake kuliko kwenda Ruaha Mbuyuni Kuinvest kulima Vitunguu... Ataonyesha saa ngapi CROP TOP yake Mpya kutoka YAHYA BOUTIQUE? Sistaduu alime vitunguu?? Hapana, bora atafute Danga la Laki 2 akalale nalo.

Big Up kwa wadada wote wajanja WALIOINVEST KWENYE KILIMO., kila Jumamosi wakati wewe unaona sifa kwenda HIGH SPIRIT LOUNGE Wadada wenzako wako RUVU wamekodi mashamba wanalima mpunga, unashangaa Huyu mdada anafanya nini kumbe mwenzio analima.

KUDOS kwa wanaume wenzangu ambao wamegundua siri kwamba kuuza Sura hakulipi ma wameinvest Shamba, kila weekend wanapotea kwenda kusimamia nyanya na pilipili Bagamoyo.

Utaendelea kuwashangaa wenzio wanatajirika na kudhani kila mtu anauza UNGA hapa mjini, Kilimo ndio unga mpya... nnadhani mkandamizaji amenuunua ile BMW X6 kwa episode za ORIJINO COMEDY? Thubutu, nenda MBARARI umkute amejaa Matope akipalilia Mpunga wake ndo utajua na wewe kwa nini unapanda Bajaji mpaka
NI HAYO TU KWA LEO.
 
Hii inaitwa makavu live ( Kwa sauti ya Joti )
 
Haya mambo bwana ukiyasoma kwenye maandishi, utayaona ni rahisi kweli kama vile bushman alivyokuwa anaichambua report ya CAG, kwa kukopa namba, hiiunaitoa huku, unaiweka hapa mambo yanajipa!!! Baba ingia uwanjani, ndio utaona kumbe ni shughuri!!! Na tatizo lenu huwa hamuongelei kabisa risk zilizopo kwenye kilimo, hasa kwenye haya mazao ya muda mfupi!!, nyanya, bamia, tikiti, vitunguu, kuwa yakishaaiva, ni kukubaliana tuna bei yasoko, kwani huwezi yatunza, tofauti namazao mengine!! Juzi kuna mdau humu, alisema alilima tikiti kama la milioni 2.5,akalileta sokoni, hapo alikula hasara ya milioni 2!!!kilimo sio rahisi ki hivyo.
 
Ni kweli sio rahisi kwa pesa hiyo.
Lakini safari moja huzaa nyingine kuliko kukaa kabisa.
Ukianza hata ukifeli una faida ya kupata kitu kinaitwa uzoefu.
 
Haya mambo bwana ukiyasoma kwenye maandishi, utayaona ni rahisi kweli kama vile bushman alivyokuwa anaichambua report ya CAG, kwa kukopa namba, hiiunaitoa huku, unaiweka hapa mambo yanajipa!!! Baba ingia uwanjani, ndio utaona kumbe ni shughuri!!! Na tatizo lenu huwa hamuongelei kabisa risk zilizopo kwenye kilimo, hasa kwenye haya mazao ya muda mfupi!!, nyanya, bamia, tikiti, vitunguu, kuwa yakishaaiva, ni kukubaliana tuna bei yasoko, kwani huwezi yatunza, tofauti namazao mengine!! Juzi kuna mdau humu, alisema alilima tikiti kama la milioni 2.5,akalileta sokoni, hapo alikula hasara ya milioni 2!!!kilimo sio rahisi ki hivyo.

"If you tell a poor man the trials of getting rich, he will decide to remains poor! "
 
Laki tano, uanze biashara ya maji?!! Kwanibiashara ya maji ni tank tu ndio linatakiwa? Chanzo cha hayo maji, kiko wapi, kisima? Unacho? Kama ni ya mamlaka ya maji, kibali unacho? Yaani hiyo laki tano, kama hata unatumia majiya mamlaka itaishia kwenye vifaa tu, kabla hata ya hilo tank.
 
"If you tell a poor man the trials of getting rich, he will decide to remains poor! "
Sio kwa amount hiyo unayoisema laki tano?!! Mimi nipo kwenye shughuri hizi za kilimo, nazifahamu sana!! Sio rahisi hivyo, bora nibaki poor, bila deni la mtu, kuliko nikachukue pesa kwa mtu, ambayo itaenda kuzama, nibaki poor, na madeni juu!! Kwanini taasisi za fedha kwenye mikopo ya kilimo wanakuwa wagumu kutoa pesa?!!
 
Masanja unajificha kwa maneno msururu na dini uwongo na kweli!

Ukweli wako wa ngada utajulikana tu one day!

Muulize yule dada wa vibubu sasa hivi anaozea jela!

Everything will come to light!

Watch this space my niggas!
Halafu hao ndio wanakuja kuwa jaza watu upepo!! Eti laki tano, uanzie kilimo, biashara ya maji?!!
 
Masanja unajificha kwa maneno msururu na dini uwongo na kweli!

Ukweli wako wa ngada utajulikana tu one day!

Muulize yule dada wa vibubu sasa hivi anaozea jela!

Everything will come to light!

Watch this space my niggas!
Umenikumbusha yule Dada kule insta kulikuwa hakutoshi, kila siku mtu anaweka 200,000-500,000/- kwa kibobo, hakii kina mama tulipata tabu sana. Unajiulizs anafanya kazi gani ? Kumbe duuuh!

Watu tukakomaa na kujibana hadi vihela vya mboga mweeeh kumbe mwenzetu anafanya mishe za madawa ya kulevya na mumewe puuuumbaaaaavuuuu zake. Japo alitumotivate kupiga kazi ila ..mwisho wa kuvunja kibobo mwenzio ana million mpaka 60-70 huko! Aiseeeee not fair kabisa.

Swala la masanja ...kilimo siyo rahisi kama maandishi ya kutype nyuma ya keyboard! Yeye anajua sana hustle alizopitia, aache kudanganya watz...kuwa laki tano unakodi sijui heka ngapiiii...haya mbegu unanunua na sh ngapi? Madawa? Hizo hekari huwez hudumia mwenyewe lazima uweke watu! Wale washibe walale....aiseee asiwachanganye.

Alichoandika hapo NI UONGO MTUPUUUUU.......hakifanikiwi katika uhalisia.

Laki tano unalima heka moja tu! Na unaweza pata faida ama usipate!

1. Kukodi shamba
2. Kulima shamba
3. Kuweka matuta
4. Mifereji ya maji
5. Kununua mbegu
6. Kutengeneza kitalu
7. Kuhamisha mbegu
8. Kuweka mbolea
9. Usiku kumwagilia
10. Kupiga sawa
11. Kuvuna
12. Kununua chakula cha wakulima
13. Kuwalipa wakulima
14. Kutafuta mteja na kukubaliana nae shambani
15. Umetumia 500,000/
16. Unapata 700,000. Na hujawalipa wakulima. Pumbaaaaaaavuuuuu zako masanja acha uongo tuliolima tunaeleewa bhanaaa

Asante kwa kunikumbusha kilimo. Ntarudi soon huko ha h ha haaaà
 
Back
Top Bottom