Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,423
- 80,138
MAMBO UNAYOTAKIWA UYAJUE KWENYE NDOA.
Anaandika, Robert Heriel
i. Ndoa ni taasisi nyeti inayounda serikali ndogo iitwayo Familia.
ii. Serikali(familia) lazima iwe na muundo wa utawala na mamlaka.
Nature imempa Mwanaume nafasi ya kuwa Mtawala.
Hivyo Baba ndiye Mtawala, Rais, alafu Mama ndiye Makamu au msaidizi wa Rais.
iii. Katika miaka mitatu ya mwanzoni katika kuunda serikali, Ni muda wa kujenga UMOJA, upendo thabiti, kubadilisha baadhi ya tabia ili kufanya serikali iwe na nguvu.
Kwa vile mmetoka katika makuzi tofauti, miaka mitatu ya mwanzo Ipo kwaajili ya kila mmoja kuchuja tabia ambazo hazifai na kuzipa nguvu Tabia ambazo zinafaa.
iv. Ni lazima matarajio ya kila mmoja wenu yafahamike hasa katika hatua za awali.
Matarajio ndio yatatoa future ya ndoa yenu.
Matarajio hayo myajadili Kwa pamoja kuona kama Yana uhalisia au hayana.
iv. Kupitia hayo matarajio, mtakayopata majibu na kuona yanauhalisia, yawekeeni malengo, mipango na mikakati ili kutimiza. Hiyo ndio itakuwa ndoto yenu.
iv. Baada ya kujua malengo yenu kama wanandoa. Wekeni Sheria na Kanuni za familia yenu. Baba ndiye awe incharge, kiongozi au Mtawala.
Sheria hizo zitungwe kuhakikisha zinalinda na kutunza malengo, maadili na hadhi ya familia yenu.
iv. Undeni mabaraza na mikutano ya familia. Vikao vya mwezi, Robo Mwaka au kikao kikuu cha Mwaka cha familia.
V. Kila changamoto itakayojitokeza, jitahidini kuishughulikia Kwa UMOJA Kwa nguvu, Msiwe Watu wa kulaumiana.
Mfano, Mkeo anachangamoto ya uchoyo.
Fanya uchunguzi kisha uwe na uthibitisho kuwa Mkeo ni mchoyo.
Kupitia vikao elezeni changamoto zinazowakabili na ambazo zinaweza kuitia doa serikali yenu.
Mfano, katika kikao cha familia cha mwisho wa mwezi unaweza kusema ukiwa wewe na Mkeo/Mumeo. Utasema;
" Tumetoka hapa(unataja) tumefika hapa(unataja Mafanikio) na tunampango wa kufika pale. Lakini kuna mambo ambayo ni changamoto tunapaswa kuyafanyia kazi, mfano, Mimi Kama Mwenyekiti au kiongozi wa familia nilikuwa na changamoto ya kuchelewa kurudi nyumbani, Katibu wangu(MKE wangu) akajitahidi Sana kunisaidia niache Tabia Hii ambayo haikuwa nzuri, hata hivyo Wakati mwingine ni Kutokana na majukumu ya utafutaji, pia nilikuwa na tatizo la kuchat chat nikitongoza Wanawake wengine😊. Hilo pia Katibu Mkuu(MKE wangu) alinisaidia Sana. Kiukweli limepungua ingawaje haikuwa kazi rahisi. Nipende kukusifu Katibu wangu(MKE wangu) Kwa jitihada kubwa ulizozifanya. Nafikiri hata wewe umeona mabadiliko. Si ndio?
Utamwacha ajibu.
Lakini hata Mimi nimeona mabadiliko makubwa Kwa Katibu wangu, Hana Ile Tabia ya kuwanyima Watu vitu, siku hizi amekuwa mkarimu na naona mabadiliko haya yanakuwa kwa Kasi Sana. Ninauhakika ndani ya miezi sita ijayo changamoto Hii tutashirikiana kuitokomeza. Kama Katibu ukiweza kuishughulikia changamoto yangu Kwa upendo nami nikatoa ushrikiano basi bila Shaka hata hili halitatushinda. Muhimu na moyo na Nia ya kutaka Kubadilika.
Huo ni mfano wa namna ya Kudili na changamoto za kitabia ndani ya ndoa zinazohatarisha mipango ya ndoa.
Huna haja ya kumtukana MTU, huna haja ya kumpiga MTU, huna haja ya kumchukia MTU. Panapo upendo hakuna matusi wala mapigano.
vi. Baba ni kiongozi wa Familia lakini haimaanishi amfanye MKE mtumwa.
MKE ni msaidizi na pambo la familia lakini haimaanishi awe mzigo Kwa mumewe au amfanye mumewe ndiye Msukule wake. Yaani kila kitu afanye Baba, nop! Familia Bora haijengwi hivyo.
Serikali ya familia inajengwa Kwa kushirikiana ila nafasi ya Rais/kichwa cha nyumba inaheshimiwa.
Ni vizuri Mwanamke Kabla hujaolewa, uwe Makini zaidi kuchagua kichwa au Rais atakayekuongoza Maisha yako yote.
vii) Mali na mapato
Chochote kitakachopatikana ndani ya familia ni chenu wote. Ni Mali ya familia. Kauli Tata zinazolenga ubinafsi zidhibitiwe ndani ya nyumba, Hali yoyote ya ubinafsi idhibitiwe.
Ile Tabia ya kusema Mali ya Mwanamke ni yamwanamke haitoweza kujenga familia Bora. Au Ile Tabia tuliyonayo wanaume ya ubinafsi, mfano mwanaume anasema; Sitaki Tabia Hii kwenye nyumba yangu"
Kiutawala haijakaa vizuri, haijengi isipokuwa inabomoa. Kauli hiyo inapaswa kutolewa Kwa Watu wasiohusika na serikali yenu. Lakini MKE wako na watoto huwezi waambia hivyo. Huko ni kutengeneza Ufa utakaoangusha ukuta miaka ijayo.
Kwa mfano utasema;
" Sote tunafahamu sheria tulizojiwekea katika nyumba yetu. Sheria zinazoipa familia yetu hadhi na heshima kubwa ndani ya jamii yetu. Hatutavumilia yeyote kuona akivunja Sheria hizi. Mimi kama Baba au mwenyekiti nitamshughulikia ipasavyo Kwa maslahi mapana ya familia"
Lazima familia iwe na sheria ya mapato na matumizi pamoja na udhibiti WA fedha na ukaguzi wa fedha za familia.
Tabia ya kupuuza Mali au mapato ya familia inaweza kuiangusha familia.
Kupitia mapato na Mali familia nyingi zimeanguka.
Baba wengi wamejiingiza kwenye shughuli hatari zilizoathiri familia, wakifanya mambo hayo Kwa Siri.
Mama wengi wamejikuta wakitapeliwa au kuingia katika madeni na kuingiza familia katika ugumu.
Watoto wamejiingiza katika tabia hatarishi kama udokozi, umalaya, na hata ushoga kisa Kupata Pesa.
Ni vizuri Mali zote za familia zikaratibiwa Kwa sheria za familia.
Mfano, iundwe sheria za manunuzi ya familia na vitu vya wanafamilia kama vile nguo au viatu au saa au kitu chochote.
Haitoruhusiwa MTU kuvaa kitu au kuwa na kitu pasipo maelezo yanayojitosheleza kuhusu nguo au kitu hicho.
Suala la mapato na Mali lisiwe siri, na iwe ni kosa na uhujumu, na usaliti Kwa yeyote atakayeficha fedha au Mali yoyote ndani ya familia.
VIII) wizara ya mambo ya nje.
Wazazi wa Pande mbili, Ndugu, jamaa na marafiki. Wekeni sheria kuhusu namna mtavyoingiliana na watu wa nje. Wapo watakakokuwa kwenye jumuiya yenu, ndizo familia mlizotoka, na wapo ambao ni wambali kabisa.
Lazima iwepo sheria ya kuingiliana na watu hao.
Muingiliano wowote ule utadhibitiwa na Kanuni isemayo" Family First"
Muingiliano wowote wenye dalili yoyote ya kudhuru familia utadhibitiwa Kwa ukaribu na nguvu zote tangu ikiwa hatua za awali.
Sheria za muingiliano na watu wengine italenga kunufaisha familia na wanafamilia na sio kuitia serikali hasara.
Muingiliano wowote wenye ishara zozote z hasara utaondolewa. Na Kanuni zote zitendwe Kwa Haki.
ix) kuruhusu na udhibiti wa Programu, propaganda na mawasiliano.
Kutakuwa na namna ya kudhibiti na kuruhusu baadhi ya Programu na propaganda zenye mrengo wa kutoa chachu na Kuathiri wanafamilia kufikia malengo. Kujenga hadhi, maadili na kutimiza matarajio ya familia.
Baba ambaye ndiye mwenyekiti ni lazima awe na Akili na Upeo wa kutosha kutengeneza agenda na Programu zenye lengo la kuifanya familia iwe tulivu na salama.
Kutokana na nguvu ya Mama Kwa Watoto, ni lazima Baba atumie nguvu kubwa kuiteka Akili, mtizamo, falsafa na Imani ya Mama ili agenda zote zifike na kueleweka Kwa Watoto kurahisi.
Tunafahamu Lugha ya Baba mara nyingi ni ngumu kueleweka Kwa Watoto. Ila Lugha ya Mama Ndio Lugha ya Watoto.
Kumdhibiti Mama, na kumfanya Mama awe na heshima Kwa Baba nu Mafanikio ya muda wote na yauhakika ndani ya Familia.
Programu za nje iwe kwenye media, vyombo vya habari, mitandao ya kijamii lazima kama familia mjue namna ya kuidhibiti na kuwafundisha Watoto jinsi ya kuitumia.
Hata hivyo kila umri ni muhimu kuangaliwa Kwa ukaribu. Upo umri ambao Mama atapaswa kukaa na Binti yake kumuambia Black and white halikadhalika na Baba Kwa kijana wake.
Hivyo ni jukumu la Baba kujikita katika kum-shape MKE/Katibu Mkuu ili kila hatua Isiwe na dosari.
X) Kukabiliana na Adui.
Zipo changamoto na wapo maadui.
Sio kila adui ni changamoto. Ila kila changamoto ni fursa ya kujifunza.
Ila wapo maadui ambao wapo kwaajili ya kukuangamiza au kuiangusha Familia.
Misingi ya kukabiliana na changamoto na adui hujengwa kila Siku, lakini foundation kuu hujengwa miaka ya awali.
Adui mkubwa Kwa wanaume ni tamaa ya Wanawake. Hali inayotupelekea kujikuta katika mashimo marefu yanayotuletea maanguko ya familia zetu, kuleta maradhi ndani katika familia n.k.
Sijasema kuwa Wanawake hawachepuki Ila nazungumzia Sisi wanaume ndio kidogo tumewazidi Wanawake Kwa mbali.
Adui huyu lazima mjue namna ya kukabiliana naye katika njia ya Amani yenye utatuzi.
Subiri nipumzike Kwanza, nitaendelea..
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam